Siku nakuja kuchukuliwa nilikuwa ofisini naendelea na kazi, polis wakaenda kwa bosi na kumwambia kuwa katika upelelezi wao wanaomba wanichuke na mimi, hapo ndiko nikaondoka nao mpaka kituoni. Nikaa ndani kwa siku 3 then nikapata dhamana. Nilipotoka nika mtumia bosi sms kumuuliza kama kesho yake niende kazini, akasema niende kuonana na mwanasheria wake huko nitapewa utaratibu, akanipa namba ya huyo mwanasheria.
Nilipofika huko huyo mwanasheria akasema kuwa nina two options, either nili sign mwenyewe na kupata haki zangu zote ama kampuni ini terminate. Nikaomba muda wa kufikiria, nikaomba kukutana naye ili nimpe uamuzi wangu. Siku nakutana naye bosi wangu pia alikuja, nikawapa msimamo kuwa mimi sina kosa so kama wao wanaona nina kosa basi wani terminate. Siku wameniita kuchukua hiyo termination letter nikakuta imeandikwa 'Mutual Agreement ' yani mimi na kampuni tumeamua kwa pamoja, nikakataa ku sign na kuwaambia waniandikie barua ya termination kuwa wao ndiyo wanani terminate. Wakadai njia hiyo inachukua mda mrefu na process ni nyingi. So wakasema basi hawana jinsi watafanya hizo process then watani terminate. So mpaka sasa sijaitwa tena.
Cc :
Mung Chris