Msaada wa Kisheria

Msaada wa Kisheria

Chrost

Member
Joined
Aug 17, 2022
Posts
38
Reaction score
24
Salaam,Mnamo mwaka 2003 kulitokea Bomoa bomoa katika maeneo ya Jeshi la wananchi kambi ya Changanyikeni 691 kj.
Raia walituhumiwa kuvamia maeneo ya jeshi na kujenga bila kibali

Baada ya nyumba hizo kubomolewa baadhi ya waliobomolewa (waliokuwa na uwezo wa kuchangia pesa kwa ajili ya wakili) walifungua kesi ambapo baada ya kesi kuunguruma kwa miaka 16,Jeshi liliamuliwa na mahakama kuwalipa fidia waliobomolewa.

Utata unaanzia hapa
Jeshi lililipa fidia kwa wale waliobaki mpaka mwisho wa kesi wale walioshindwa kutoa pesa ya wakili wakawekwa pembeni Swali langu hapa hii KISHERIA Imekaaje?

Tulijaribu kuwafata wale walioshinda Kesi na kulipwa, kwa bahati mbaya Hawatoi ushirikiano !

Wajuzi wa Sheria hii imekaaje?

Je tunaweza fanya kitu tukapata haki yetu?

Kama inawezekana Je ni hatua zipi zifuatwe?

ASANTENI,Home of Great Thinkers.
 
Nyie ni victims tu hamkuwa parties msingeweza kulipwa
 
Kafungueni fresh suit ila nina wasi wasi mtakuwa nje ya muda ,itabidi muombe extension of time kama mna hoja za msingi za kuchelewa kufungua kesi
 
Hapa umeniacha mkuu
Mahakama haiwezi kukupa ambacho hujakiomba,pelekeni malalamiko/madai yenu mahakamani ila tafuta wakili mzuri akusimamie au akupe muongozo wa procedures za kufuata
 
Wenzako wenye pesa ilichukua miaka 16 kupata haki yao, je wewe ambaye umezinduka juzi tu utaweza kuikomboa haki ya baba yako kwa miaka mingapi?
Achana nayo, usikariri kuwa awamu hii jeshi litashindwa tena
 
Mahakama haiwezi kukupa ambacho hujakiomba,pelekeni malalamiko/madai yenu mahakamani ila tafuta wakili mzuri akusimamie au akupe muongozo wa procedures za kufuata
Asante Mkuu
 
Salaam,Mnamo mwaka 2003 kulitokea Bomoa bomoa katika maeneo ya Jeshi la wananchi kambi ya Changanyikeni 691 kj.
Raia walituhumiwa kuvamia maeneo ya jeshi na kujenga bila kibali

Baada ya nyumba hizo kubomolewa baadhi ya waliobomolewa (waliokuwa na uwezo wa kuchangia pesa kwa ajili ya wakili) walifungua kesi ambapo baada ya kesi kuunguruma kwa miaka 16,Jeshi liliamuliwa na mahakama kuwalipa fidia waliobomolewa.

Utata unaanzia hapa
Jeshi lililipa fidia kwa wale waliobaki mpaka mwisho wa kesi wale walioshindwa kutoa pesa ya wakili wakawekwa pembeni Swali langu hapa hii KISHERIA Imekaaje?

Tulijaribu kuwafata wale walioshinda Kesi na kulipwa, kwa bahati mbaya Hawatoi ushirikiano !

Wajuzi wa Sheria hii imekaaje?

Je tunaweza fanya kitu tukapata haki yetu?

Kama inawezekana Je ni hatua zipi zifuatwe?

ASANTENI,Home of Great Thinkers.
Hata kama mko wengi, kila mmoja lazima a defend his/her case. Lazima uende upigwa maswali/ujitetee, kama hukutokea kutetea haki yako, basi hukumu ikitoka haikuhusu hata kama aliyeshinda mmefungana mipaka na ardhi inayobishaniwa inajumuisha na ya kwako
 
Back
Top Bottom