Pole sana mkuu. Ni kinyume na maadili ya Kiwakili kutoa ushauri bure lakini kwasababu mimi ni Mkristo Mkatoliki na leo ni Jumapili, basi nitakupa ushauri bure kama sadaka [emoji28]
Ni kosa yeye kukata miti wakati Mahakama ya kawaida iliamuru akafungue kesi kwenye Mahakama yenye mamlaka ambayo ni Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya. Lakini kikanuni, kesi yoyote ni lazima ianzie Baraza la Ardhi la Kata kwa ajili ya usuluhishi, likishindwa kuwasuluhisha litatoa hati ambayo mlalamikaji ataitumia kufungua kesi kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya.
Iko hivi, Mahakama ya kawaida imemuamuru aende kwenye Mahakama ya Ardhi kwasababu, ili mtu adai haki kwenye ardhi, ni lazima umiliki wake uthibitike kwanza, na ni Mahakama ya Ardhi pekee yenye mamlaka ya kufanya hivyo. Kwasababu bila umiliki kuthibitika, ipo hatari ya kumpa haki mtu ambaye hakustahili.
Mahakama ya Ardhi ikishamthibitisha mmiliki halali kati yako na huyo mlalamikaji, basi mmiliki halali ataitumia hukumu ya Mahakama ya Ardhi kufungua kesi ya uvamizi na uharibifu (Criminal trespass).
Hadi sasa, kati yenu hakuna aliyethibitishwa kuwa mmiliki halali. Cha kufanya omba fasta nakala ya hiyo hukumu inayowataka muende kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya, uende nayo polisi kama kielelezo, watakusaidia kumzuia.
Aidha, siyo lazima aende yeye kufungua kesi Baraza la Kata au la Wilaya, hata wewe unaweza kwenda kwasababu una interest over the plot of land. Anaweza akatulia akaendelea kukata miti hadi ikaisha. Ila nikutie moyo tu kwamba hata akiikata ikamalizika, kesi ikisikilizwa ukaonekana wewe ndiye mmiliki halali, unaweza kufungua kesi ya madai ukalipwa fidia.
Asante. Nitarudi tena.