Msaada wa Kisheria

Msaada wa Kisheria

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Jirani yangu alifungua kesi kuwa nimeingia kwenye shamba na kukata miti analodai ni lake ( ambalo nililinunua toka kwa mwanae aliyerithi kutoka kwa baba yake na huyo aliyenishitaki . Mahakama ikasema kwa vile kuna ubishani juu ya umiliki, Mahakama ikatoa amri kuwa aende mahakama ya ardhi itoe uamuzi nani mmiliki halali.
Leo ameingia kwenye shamba hilo na kukata miti yangu (wakati aliamriwa afungue kesi ya madai DLHT)

Katika senario hii nichukue hatua gani?
 
Nenda polisi kamshitaki kwa kosa la uvamizi na uharibifu wa mali yako. Huku ukisubiri mahakama ya ardhi kutoa uamuzi wa mmiliki halisi.

Suali kwako:-
1) Alie kuuzia kakupa land certificate ya umiliki?.

2) Umeshafanya uhaulishaji(kuweka jina lako kuwa mmiliki).

3) Warka( Land certificate) ya mauziano ilikuwa na jina la nani?.

4) Alikuuzia shamba lote au kipande?. Kama kipande alikuwekea mipaka yake?.
 
Pole sana mkuu. Ni kinyume na maadili ya Kiwakili kutoa ushauri bure lakini kwasababu mimi ni Mkristo Mkatoliki na leo ni Jumapili, basi nitakupa ushauri bure kama sadaka [emoji28]

Ni kosa yeye kukata miti wakati Mahakama ya kawaida iliamuru akafungue kesi kwenye Mahakama yenye mamlaka ambayo ni Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya. Lakini kikanuni, kesi yoyote ni lazima ianzie Baraza la Ardhi la Kata kwa ajili ya usuluhishi, likishindwa kuwasuluhisha litatoa hati ambayo mlalamikaji ataitumia kufungua kesi kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya.

Iko hivi, Mahakama ya kawaida imemuamuru aende kwenye Mahakama ya Ardhi kwasababu, ili mtu adai haki kwenye ardhi, ni lazima umiliki wake uthibitike kwanza, na ni Mahakama ya Ardhi pekee yenye mamlaka ya kufanya hivyo. Kwasababu bila umiliki kuthibitika, ipo hatari ya kumpa haki mtu ambaye hakustahili.

Mahakama ya Ardhi ikishamthibitisha mmiliki halali kati yako na huyo mlalamikaji, basi mmiliki halali ataitumia hukumu ya Mahakama ya Ardhi kufungua kesi ya uvamizi na uharibifu (Criminal trespass).

Hadi sasa, kati yenu hakuna aliyethibitishwa kuwa mmiliki halali. Cha kufanya omba fasta nakala ya hiyo hukumu inayowataka muende kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya, uende nayo polisi kama kielelezo, watakusaidia kumzuia.

Aidha, siyo lazima aende yeye kufungua kesi Baraza la Kata au la Wilaya, hata wewe unaweza kwenda kwasababu una interest over the plot of land. Anaweza akatulia akaendelea kukata miti hadi ikaisha. Ila nikutie moyo tu kwamba hata akiikata ikamalizika, kesi ikisikilizwa ukaonekana wewe ndiye mmiliki halali, unaweza kufungua kesi ya madai ukalipwa fidia.

Asante. Nitarudi tena.
 
Fanya vitu kwa utaratibu wala usiweke hisia, rudi kwa waliowapa ushauri, pia katoe taarifa Police, mtendaji ndo hatua nzuri ya awali na wanakuwa na busara sana.

Ila hayo mambo ya kununua Mashamba ya mtoto aliyepewa na Baba bila maandishi ni mateso, na life time struggles.

Tafuta aman na kama huyo Mzee mwaweza zungumza ni better kuliko ku pursue legal path, unaweza teseka zaidi ndugu.
 
Nenda polisi kamshitaki kwa kosa la uvamizi na uharibifu wa mali yako. Huku ukisubiri mahakama ya ardhi kutoa uamuzi wa mmiliki halisi.

Suali kwako:-
1) Alie kuuzia kakupa land certificate ya umiliki?.

2) Umeshafanya uhaulishaji(kuweka jina lako kuwa mmiliki).

3) Warka( Land certificate) ya mauziano ilikuwa na jina la nani?.

4) Alikuuzia shamba lote au kipande?. Kama kipande alikuwekea mipaka yake?.
Mkuu, huu ni upotoshaji.

Jifunze kuheshimu taaluma za watu. Soma post yangu #8 kwa faida yako na ya wengine.

Nakubaliana na wewe hapo uliposhauri aende Polisi, kwengine kote umepuyanga.
 
Uko mzuri msomi,! Kipengele unachosema achukue nakala ya hukumu kwenda nayo police Ili kuzuia uharibifu inayoendelea kwenye miti - nadhani haiwezi kimsaidia sana. Kuna authority inasema iwapo Kuna hot dispute on the ownership criminal trespass can not be instituted. Ni kwamba akifungua kesi Baraza la ardhi atapeleka maombi ya temporary injunction under certificate of urgency ambapo atapewa stop order dhidi ya anayekata hiyo miti yake.
 
Pole sana mkuu. Ni kinyume na maadili ya Kiwakili kutoa ushauri bure lakini kwasababu mimi ni Mkristo Mkatoliki na leo ni Jumapili, basi nitakupa ushauri bure kama sadaka [emoji28]

Ni kosa yeye kukata miti wakati Mahakama ya kawaida iliamuru akafungue kesi kwenye Mahakama yenye mamlaka ambayo ni Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya. Lakini kikanuni, kesi yoyote ni lazima ianzie Baraza la Ardhi la Kata kwa ajili ya usuluhishi, likishindwa kuwasuluhisha litatoa hati ambayo mlalamikaji ataitumia kufungua kesi kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya.

Iko hivi, Mahakama ya kawaida imemuamuru aende kwenye Mahakama ya Ardhi kwasababu, ili mtu adai haki kwenye ardhi, ni lazima umiliki wake uthibitike kwanza, na ni Mahakama ya Ardhi pekee yenye mamlaka ya kufanya hivyo. Kwasababu bila umiliki kuthibitika, ipo hatari ya kumpa haki mtu ambaye hakustahili.

Mahakama ya Ardhi ikishamthibitisha mmiliki halali kati yako na huyo mlalamikaji, basi mmiliki halali ataitumia hukumu ya Mahakama ya Ardhi kufungua kesi ya uvamizi na uharibifu (Criminal trespass).

Hadi sasa, kati yenu hakuna aliyethibitishwa kuwa mmiliki halali. Cha kufanya omba fasta nakala ya hiyo hukumu inayowataka muende kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya, uende nayo polisi kama kielelezo, watakusaidia kumzuia.

Aidha, siyo lazima aende yeye kufungua kesi Baraza la Kata au la Wilaya, hata wewe unaweza kwenda kwasababu una interest over the plot of land. Anaweza akatulia akaendelea kukata miti hadi ikaisha. Ila nikutie moyo tu kwamba hata akiikata ikamalizika, kesi ikisikilizwa ukaonekana wewe ndiye mmiliki halali, unaweza kufungua kesi ya madai ukalipwa fidia.

Asante. Nitarudi tena.
UBARIKIWE SANA.
BASI NITACHUKUA OPTION YA : Hadi sasa, kati yenu hakuna aliyethibitishwa kuwa mmiliki halali. Cha kufanya omba fasta nakala ya hiyo hukumu inayowataka muende kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya, uende nayo polisi kama kielelezo, watakusaidia kumzuia.
If this does not work, then i will take the second option!
 
Uko mzuri msomi,! Kipengele unachosema achukue nakala ya hukumu kwenda nayo police Ili kuzuia uharibifu inayoendelea kwenye miti - nadhani haiwezi kimsaidia sana. Kuna authority inasema iwapo Kuna hot dispute on the ownership criminal trespass can not be instituted. Ni kwamba akifungua kesi Baraza la ardhi atapeleka maombi ya temporary injunction under certificate of urgency ambapo atapewa stop order dhidi ya anayekata hiyo miti yake.
asante. Ikishindikana ya polisi, then nitfuata ushauri wako under certificate of urgency with injunction
 
Attachments

Uko mzuri msomi,! Kipengele unachosema achukue nakala ya hukumu kwenda nayo police Ili kuzuia uharibifu inayoendelea kwenye miti - nadhani haiwezi kimsaidia sana. Kuna authority inasema iwapo Kuna hot dispute on the ownership criminal trespass can not be instituted. Ni kwamba akifungua kesi Baraza la ardhi atapeleka maombi ya temporary injunction under certificate of urgency ambapo atapewa stop order dhidi ya anayekata hiyo miti yake.
Asante.

Sikutaka kumpeleka huko kwenye kufungua kesi ya msingi (land application), zuio la muda (temporary injunction) na kuomba isikilizwe kwa haraka kwa kuweka hati ya dharura (certificate of urgency), kwasababu hizo ni hatua za mbele sana.

Yeye alitaka cha kufanya sasa kwasababu jamaa ameanza kuvuna miti.

Kwa sasa polisi wanaweza kumsaidia kwa kutumia nakala ya hukumu. Hapa itatumika busara na siyo Sheria, kwasababu so far, hata hao polisi hawamjui mmiliki halali.

Vinginevyo afanye kama nilivyoshauri mwishoni kwamba amuache aendelee kuvuna wakati huo afungue shauri la msingi, akishinda adai fidia.
 
Nenda polisi kamshitaki kwa kosa la uvamizi na uharibifu wa mali yako. Huku ukisubiri mahakama ya ardhi kutoa uamuzi wa mmiliki halisi.

Suali kwako:-
1) Alie kuuzia kakupa land certificate ya umiliki?.

2) Umeshafanya uhaulishaji(kuweka jina lako kuwa mmiliki).

3) Warka( Land certificate) ya mauziano ilikuwa na jina la nani?.

4) Alikuuzia shamba lote au kipande?. Kama kipande alikuwekea mipaka yake?.
 
Pole sana mkuu. Ni kinyume na maadili ya Kiwakili kutoa ushauri bure lakini kwasababu mimi ni Mkristo Mkatoliki na leo ni Jumapili, basi nitakupa ushauri bure kama sadaka
Hapa rafiki umeniacha hoi! Tunashauriwa kuwasaidia wenye uhitaji inapowezekana. Asante sana.
 
UBARIKIWE SANA.
BASI NITACHUKUA OPTION YA : Hadi sasa, kati yenu hakuna aliyethibitishwa kuwa mmiliki halali. Cha kufanya omba fasta nakala ya hiyo hukumu inayowataka muende kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya, uende nayo polisi kama kielelezo, watakusaidia kumzuia.
If this does not work, then i will take the second option!
Mkuu, nimefanya sana kwa wateja wangu kadhaa na ikafanya kazi. Polisi watatumia busara, hakuna Sheria inayowapa hayo mamlaka lakini busara inawataka kufanya hivyo.

Besides, huendi na maneno matupu, unaenda na nakala halali ya Hukumu ya Mahakama. Unawapa Polisi hela kidogo ya mafuta [emoji2], unaambatana nao hadi kwenye ofisi za Serikali ya Mtaa husika au Afisa Mtendaji, mlalamikaji anaitwa anaelezwa.

Wakishakuwepo Polisi jamaa atatuliza tu mshono [emoji28].
 
Mtoto shamba kapewa na babake harafu akakuuzia wewe!, kuna uthibitisho wa umiliki wa mtoto kumilikishwa hilo shamba?, maana yaonekana kama mtoto kauza shamba lisilo lake.
 
Back
Top Bottom