kinywanyuku
JF-Expert Member
- Jul 13, 2015
- 3,746
- 2,924
Wanajukwaa naomba kujuzwa kuhusu kilimo cha karoti, 1.mbegu ipi nzuri? 2.Je huwa zinaandaliwa kitaluni kama vitunguu, 3.msimu mzuri kuanza kulima zao hili. Ni hayo tu ahsanteni sana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wanajukwaa naomba kujuzwa kuhusu kilimo cha karoti,1.mbegu ipi nzuri? 2.Je huwa zinaandaliwa kitalun kama vitunguu,3.msimu mzuri kuanza kulima zao hili.ni hayo tu ahsanteni sana
Karoti inapandwa mojakwa moja, unapana stari hadi mstari cm15, pia katika mstari una sia mbegu kidogo kidogo baada ya kuota zikifikisha majani 5 ngoa na kuziacha ktk umbali wa cm5 toka mche hadi mche, kumbuka mistari yako ichore kukata tuta(kwa upana) sio kwa urefu. zaidi uliza
Inategemeana na ukanda ulipo wewe kama ni baridi au joto na pia kama unasubiri tu mvua au kuna maji mda wote kwanza uko wapi kama vip ni PM nikuelekeze
ahsante ukingoa mche na kuhamisha sehem nyingine unakubali kuota?
karoti haihamishi kama nyanya na vitunguu, ukiing'oa tupa tu, haitapona ukiipanda
Karoti isipopata maji au unyevu inakauka, inategemea na eneo lako lakini kawaida mwagilia asubuhi na jion kama maji ni shida na eneo sio kavu sana chagua mda mmoja wa kumwagilia asubuhi au jion vizuri asubuhi,
Ahsante
wadau naombeni msaada kuhusu karoti zangu,nimelima mwezi wa nne mwaka huu mpaka sasa naona hazijakomaa zimetoka zimebanana halafu ni nyembamba,kuhusu mbolea niliweka UREA na DAP naomba nisaidien nifanyaje ili ziwe nene tayari zimeota lakini nyembamba halafu zimebanana
Ndugu yangu nikupe pole kwa tatizo ulilopata. Kwanza kabisa nikufahamishe namna ulitakiwa kufanya ili mavuno yako yawe bora.
Baada ya kuandaa shamba siku ya kupanda unarusha mbollea na umesema ulifanya hivyo. Kisha unarusha mbegu na hapa ndio huwa kuna tatizo. Tatizo ni urushaji naomba ufahamu kuwa siyo kila mtu anaweza rusha mbegu maana inahitaji utaalamu ili wasibanane.
Tatizo la shamba lako ulirusha mbegu zikasongana ndio maana hazivimbi.
Sijajua shamba lako ni la ukubwa gani na kiasi cha mbolea aina ya urea ulirusha lakini pia mapema ulipaswa kupunguza zile dhaifu ila sasa nikushauri hivi;
Zikibanana zaidi ktk shamba langu mimi huwa naweka mbolea ya kutosha ya urea huwa inafanya zivimbe vizuri.
Kwa swala la muda nadhani bado hazijachelewa sana huwa zinachukua muda kutegemeana na hali ya hewa na pia kama zimebanwa sana zitachelewa. Asante
asante ndugu kwa kunielekeza wkt narusha nilikuwa nachota kiganjan halafu nachora mstari na kidole nazinyunyulizia kwenye mstari halafu nafukia mstari halafu naruka sm 15 narushia zingine
Hapo ulikua sawa, ila baada ya kuota ulitakikiwa kung'olea na kuziacha cm 5 kutoka mche hadi mche ktk mstari mmoja