Msaada wa kitaalamu wa Kilimo cha Karoti

kinywanyuku

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2015
Posts
3,746
Reaction score
2,924
Wanajukwaa naomba kujuzwa kuhusu kilimo cha karoti, 1.mbegu ipi nzuri? 2.Je huwa zinaandaliwa kitaluni kama vitunguu, 3.msimu mzuri kuanza kulima zao hili. Ni hayo tu ahsanteni sana.
 
wanajukwaa naomba kujuzwa kuhusu kilimo cha karoti,1.mbegu ipi nzuri? 2.Je huwa zinaandaliwa kitalun kama vitunguu,3.msimu mzuri kuanza kulima zao hili.ni hayo tu ahsanteni sana

Inategemeana na ukanda ulipo wewe kama ni baridi au joto na pia kama unasubiri tu mvua au kuna maji mda wote kwanza uko wapi kama vip ni PM nikuelekeze
 
Karoti inapandwa mojakwa moja, unapana stari hadi mstari cm15, pia katika mstari una sia mbegu kidogo kidogo baada ya kuota zikifikisha majani 5 ngoa na kuziacha ktk umbali wa cm5 toka mche hadi mche, kumbuka mistari yako ichore kukata tuta(kwa upana) sio kwa urefu. zaidi uliza
 
ahsante ukingoa mche na kuhamisha sehem nyingine unakubali kuota?
 
Inategemeana na ukanda ulipo wewe kama ni baridi au joto na pia kama unasubiri tu mvua au kuna maji mda wote kwanza uko wapi kama vip ni PM nikuelekeze

nipo iringa mkuu natumia maji ya kisima kumwagilia
 
karoti haihamishi kama nyanya na vitunguu, ukiing'oa tupa tu, haitapona ukiipanda

vp kuhusu kumwagilia nasikia unamagilia leo,halafu kesho humwagilii unaenda kwa utaratibu huo mpaka zikue?
 
Karoti isipopata maji au unyevu inakauka, inategemea na eneo lako lakini kawaida mwagilia asubuhi na jion kama maji ni shida na eneo sio kavu sana chagua mda mmoja wa kumwagilia asubuhi au jion vizuri asubuhi,
 
Ahsante
 
wadau naombeni msaada kuhusu karoti zangu,nimelima mwezi wa nne mwaka huu mpaka sasa naona hazijakomaa zimetoka zimebanana halafu ni nyembamba,kuhusu mbolea niliweka UREA na DAP naomba nisaidien nifanyaje ili ziwe nene tayari zimeota lakini nyembamba halafu zimebanana
 
Ndugu yangu nikupe pole kwa tatizo ulilopata. Kwanza kabisa nikufahamishe namna ulitakiwa kufanya ili mavuno yako yawe bora.
Baada ya kuandaa shamba siku ya kupanda unarusha mbollea na umesema ulifanya hivyo. Kisha unarusha mbegu na hapa ndio huwa kuna tatizo. Tatizo ni urushaji naomba ufahamu kuwa siyo kila mtu anaweza rusha mbegu maana inahitaji utaalamu ili wasibanane.

Tatizo la shamba lako ulirusha mbegu zikasongana ndio maana hazivimbi.

Sijajua shamba lako ni la ukubwa gani na kiasi cha mbolea aina ya urea ulirusha lakini pia mapema ulipaswa kupunguza zile dhaifu ila sasa nikushauri hivi;

Zikibanana zaidi ktk shamba langu mimi huwa naweka mbolea ya kutosha ya urea huwa inafanya zivimbe vizuri.

Kwa swala la muda nadhani bado hazijachelewa sana huwa zinachukua muda kutegemeana na hali ya hewa na pia kama zimebanwa sana zitachelewa. Asante
 
mbegu nilirusha kwa mtindo wa kuchota kijiko kimoja kikubwa cha chakula naweka kiganjan halafu nachora mstari
 
asante ndugu kwa kunielekeza wkt narusha nilikuwa nachota kiganjan halafu nachora mstari na kidole nazinyunyulizia kwenye mstari halafu nafukia mstari halafu naruka sm 15 narushia zingine
 
Hapo ulikua sawa, ila baada ya kuota ulitakikiwa kung'olea na kuziacha cm 5 kutoka mche hadi mche ktk mstari mmoja
 
ahsante ndugu sasa hzi tayari zimeota zimeshndwa kutanuka kwa kuwa zimebanana nifanyaje ili niepuke hasara
 
Ndugu wana jamvi,Rejeeni kichwa cha habari hapo juu!!
Naomba msaada wa kitaalamu wa kilimo cha karoti, kuanzia kuandaa shamba, kwa hekta...
Nipo mbeya
 
Asante kwa mada nzuri naomba kuuliza kuna tatizo nikilima karoti bila kutumia mbolea za viwandani badala yake nikatumia samadi
 
Back
Top Bottom