Kuna ndugu yangu anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi,tumejaribu kutumia dawa tulizoandikiwa na daktari,alionyesha dalili za kupona lakini hali imerudia tena.
Leo kuna dawa tumeambiwa tununue inaitwa VINCRISTINA, naomba kama mtu anafahamu hii dawa kwa ugonjwa huu,anisaidie kwa ushauri.
Ni Vincristine sio vincristina, hiyo ni cytotoxic drug, inatumika maranyingi kutibu aina fulani ya cell za mwili zinazozaliana bila utaratibu/mpangilio kama ilivyo katika saratani au magonjwa ya ngozi kama Psoriasis.
Inakupasa kufanya uchunguzi wa kina kuona ini na figo zako zinafanya kazi kwa usahihi