Msaada wa kitaalamu wa matibabu

Msaada wa kitaalamu wa matibabu

the locksman

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2012
Posts
1,102
Reaction score
355
Kuna ndugu yangu anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi,tumejaribu kutumia dawa tulizoandikiwa na daktari,alionyesha dalili za kupona lakini hali imerudia tena.
Leo kuna dawa tumeambiwa tununue inaitwa VINCRISTINA, naomba kama mtu anafahamu hii dawa kwa ugonjwa huu,anisaidie kwa ushauri.
 

Attachments

  • vincristina.JPG
    vincristina.JPG
    2.1 KB · Views: 118
Ni Vincristine sio vincristina, hiyo ni cytotoxic drug, inatumika maranyingi kutibu aina fulani ya cell za mwili zinazozaliana bila utaratibu/mpangilio kama ilivyo katika saratani au magonjwa ya ngozi kama Psoriasis.

Inakupasa kufanya uchunguzi wa kina kuona ini na figo zako zinafanya kazi kwa usahihi
 
Ahsante kwa ushauri mkuu,maneno ya kitibabu ni shida kwetu wengine.
Kwa hiyo picha unaona ni ugonjwa gani huo?
 
Ahsante kwa ushauri mkuu,maneno ya kitibabu ni shida kwetu wengine.
Kwa hiyo picha unaona ni ugonjwa gani huo?

Picha nimeshindwa kuikuza na kupata clear view yake, ila naona kama ni vidole vya mkono!
 
Ndio hapo ni sehemu ndogo tu nimekata kwenye mkono,umeenea mwili mzima usoni,mikono na miguu.
 
Back
Top Bottom