Nipo maeneo ya Zanzibar nahitaji sana msaada kwa anaefahamu jinsi ya kukabiliana na hili tatizo la kuvimba na baadae kubanduka kwa rangi katika kuta za ndani ya nyumba
Inasababishwa na unyevu unyevu na kusababisha fangasi za ukuta; utatatua nyakati hizi, baada ya muda tatizo linarudi. Ila kuna kemikali zinauzwa kwenye maduka ya vifaa vya ujenzi, unaweza tumia ili kupunguza tatizo.
bandua plaster iliyoharibika kuna dawa iko km unga unachanganya na cement unapiga plaster alafu baada ya hapo unachukua aina hiyo ya dawa ya maji unapaka kabla ya kuskim na white cement
Kama plaster na skiming haikubanduka najuwa hao ni fangasi wanaosababishwa na unyevu nyevu, basi fanya hivi, nunu rangi inaitwa Binder paka harafu paka rangi harisi unayoipenda iwe nzito kidogo tatizo kwisha
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.