Msaada wa kukadiria gharama za ujenzi

Msaada wa kukadiria gharama za ujenzi

Habari wakuu .

Nataka kuanza ujenzi ule wa mdogomdogo atleast by the end of the year niwe nimepaua na kuweka grill kwenye madirisha na milango ya nje.

Ramani ina ukubwa wa m 15 x m 14 na ni nyumba ya vyumba 4, vyumba 2 ni self contained na vikolombwezo vyake vyote.

Uwanja ni tambarare na nataka kujengea tofali za kuchoma na mawe kwa msingi.

Sasa nishaurini niwe na kiasi gani kukamilisha hatua nilizozitaja hapo juu, japo kiasi cha kuanzia kipo atleast ya kukamilisha msingi around 3mln.

Ramani ya nyumba kwenye picha inafanana kama hivi na floor plni yake iko hapo chini.
View attachment 1714028View attachment 1714029View attachment 1714030
1. Unajengea mkoa gani? Mjini au kijijini? Bei za materials ya ujenzi na mafundi zinatofautiana sana kulingana na sehemu
2.Unajenga nyumba ya kuishi mwenyewe, kuipangisha au vipi? Unaihitaji (need) hiyo nyumba kwa sasa au unaitaka (want) tu? Au kuuliza kivingine, kwa mini unataka kujenga?
3. Kuna umeme na maji karibu?
4. Utaweka msingi (foundation) wa zege tu au zege lenye nondo au hakuna msingi kabisa isipokuwa hayo mawe?
5. Baada ya ukuta wa mawe (plinth wall), utaweka jamvi la zege (slab)? Na je utaweka zege la nondo (ring beam) kuzunguka kuta zote kuu?
6. Sijaweza kufungua ramani yako. Je kuta zako zina upana gani? Tofali moja au mbili za kuchoma? Utatumia cement/mchanga au tope kujengea hizo tofali?
5. Madirisha yapo mangapi jumla? Na milango (ya nje na ndani)? Size zake?
6. Utaweka linta yenye nondo kuzunguka kuta zote? Au sehemu za milango na madirisha tu?
7. Utatumia mbao au miti kupaulia? Treated au ya kawaida tu?
8. Utatumia bati za aina gani? Utaweka 'fisha' na gutter?

NB:
1. Nimeuliza hayo maswali kuibua tafakari tu, sio lazima uyajibu/yajibiwe hapa. Ni baadhi ya variables tu za gharama za ujenzi? Yanaweza pia kuwafaa wasomaji wengine.
2.Ujenzi "wetu" kwa sehemu kubwa haufuati viwango vya ujenzi. Kwa hivyo, sio rahisi mtu baki kukadiria ghahama zako za ujenzi. Kwa mfano, kwa ujenzi unaofuata viwango vinavyokubalika, ni rahisi mtu kukwamba gharama ni Shs xxxxx kwa mita ya mraba.
3. Kama gharama (uwezo) ni issue kubwa sana kwako, fikiria kupata mtaalamu akusaidie.....hasa hapo kwenye design ya jengo lenyewe. This may sound weird! But wakati mwingine tunakwepa kulipa wataalamu shs 1m au hata 2m, lakini tunaingia kwenye hasara au gharama za kuepukika za mamilioni zaidi. Au unakuta jengo limeishia njiani, miaka na miaka.
 
Katavi
 
Unaweza ukipanga vizuri update na fundi mzuri inatosha
Mkuu huwezi kujenga vyumba 4 ukamaliza na hiyo 25m , hapo anza kuorodhesha tuu material ya ujenzi, nimejenga nyumba nyingi na nimekua kwenye hii field ya ujenzi kwa miaka 7 sasa,
 
Inategemea na ukubwa wa kiwanja 13 m kwa 15 inatosha
 
Back
Top Bottom