Msaada wa kukadiria gharama za ujenzi

1. Unajengea mkoa gani? Mjini au kijijini? Bei za materials ya ujenzi na mafundi zinatofautiana sana kulingana na sehemu
2.Unajenga nyumba ya kuishi mwenyewe, kuipangisha au vipi? Unaihitaji (need) hiyo nyumba kwa sasa au unaitaka (want) tu? Au kuuliza kivingine, kwa mini unataka kujenga?
3. Kuna umeme na maji karibu?
4. Utaweka msingi (foundation) wa zege tu au zege lenye nondo au hakuna msingi kabisa isipokuwa hayo mawe?
5. Baada ya ukuta wa mawe (plinth wall), utaweka jamvi la zege (slab)? Na je utaweka zege la nondo (ring beam) kuzunguka kuta zote kuu?
6. Sijaweza kufungua ramani yako. Je kuta zako zina upana gani? Tofali moja au mbili za kuchoma? Utatumia cement/mchanga au tope kujengea hizo tofali?
5. Madirisha yapo mangapi jumla? Na milango (ya nje na ndani)? Size zake?
6. Utaweka linta yenye nondo kuzunguka kuta zote? Au sehemu za milango na madirisha tu?
7. Utatumia mbao au miti kupaulia? Treated au ya kawaida tu?
8. Utatumia bati za aina gani? Utaweka 'fisha' na gutter?

NB:
1. Nimeuliza hayo maswali kuibua tafakari tu, sio lazima uyajibu/yajibiwe hapa. Ni baadhi ya variables tu za gharama za ujenzi? Yanaweza pia kuwafaa wasomaji wengine.
2.Ujenzi "wetu" kwa sehemu kubwa haufuati viwango vya ujenzi. Kwa hivyo, sio rahisi mtu baki kukadiria ghahama zako za ujenzi. Kwa mfano, kwa ujenzi unaofuata viwango vinavyokubalika, ni rahisi mtu kukwamba gharama ni Shs xxxxx kwa mita ya mraba.
3. Kama gharama (uwezo) ni issue kubwa sana kwako, fikiria kupata mtaalamu akusaidie.....hasa hapo kwenye design ya jengo lenyewe. This may sound weird! But wakati mwingine tunakwepa kulipa wataalamu shs 1m au hata 2m, lakini tunaingia kwenye hasara au gharama za kuepukika za mamilioni zaidi. Au unakuta jengo limeishia njiani, miaka na miaka.
 
Katavi
 
Njooeni tegeta kwa ndevu nitakuuzia mbao bei pouwa sana mfano 2*4 treated nauza 5000 namba zangu za mawasiliano ni 0687371138
 
Chagua ushauri ulio na manufaa kwako nje ya hapo utaishia kubishana na wasio na ujuzi wa ujenzi.
 
Unaweza ukipanga vizuri update na fundi mzuri inatosha
Mkuu huwezi kujenga vyumba 4 ukamaliza na hiyo 25m , hapo anza kuorodhesha tuu material ya ujenzi, nimejenga nyumba nyingi na nimekua kwenye hii field ya ujenzi kwa miaka 7 sasa,
 
Mkuu huwezi kujenga vyumba 4 ukamaliza na hiyo 25m , hapo anza kuorodhesha tuu material ya ujenzi, nimejenga nyumba nyingi na nimekua kwenye hii field ya ujenzi kwa miaka 7 sasa,
Inategemea na ukubwa wa kiwanja 13 m kwa 15 inatosha
 
Ukubwa wa kiwanja au ukubwa wa nyumba mkuu? Kiwanja si sehemu yote itajengwa

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
Hapo mtu kashajiwekea gharama yake kichwani. Panga pangua hata mabati used anayapaka rangi.
Mradi tu aonekane amejenga nyumba ya kisasa.
Hawezi kukuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…