miminimama
JF-Expert Member
- Aug 2, 2018
- 703
- 1,840
Habari wanajukwaa.
Mnamo mwanzoni mwa September mwaka huu nilitengeneza kadi ya malipo ya mtandaoni(master card) kwa kutumia akaunti ya mix by yas.
Kadi ile ilikuwa kwa ajili ya malipo ya ticket ya ndege kupitia kampuni ya uwakala ya ndege. Baada ya kutengeneza hiyo kadi nikafanya malipo, hela ikakatwa kwenye akaunti ya mix by yas.
Ndani ya lisaa baada ya kufanya malipo ile virtual card ya mix by yas ikafutwa na kuwa expired ilikuwa kwa ajili ya malipo ya mara moja.
Wakala wa ndege wakaniambia niconfirm malipo ili nimalizie kufanya booking, sasa nitaconfirm vipi malipo na kadi imeshafutwa na kuexpire?
Nikashindwa kufanya hivyo. Hivyo booking yangu ikawa cancelled.
Wakala wa ndege wakanipigia simu ya kawaida na kunitumia email kuwa sijawa charged na chochote na kama kuna kiasi kimekatwa kwenye akaunti yangu basi automatically kitakuwa kwenye akaunti yangu ndani ya siku 7-14 za kazi.
Lakini mpaka leo hela haijarudi. Mix by yas wanasema hela imeenda nilipokuwa nafanya malipo ili wao warudishe muamala inabidi niwape ARN. Wakala wa ndege anasema hawawezi kutoa ARN sababu wao hawajakata hela yoyote na hawajapokea muamala wowote.
Hivyo kama nimekatwa niwasiliane na bank yangu ili wanirudishie.
Mix by yas nawaomba kama kuna number yoyote (referrence) kuwa hela imefika kwa wakala wa ndege wanipe ili niwatumie wakala wa ndege waangalie bank statement yao, mix by yas wanasema hawana namba yoyote wanachojua kuwa muamala umewafikia wahusika.
Huu mkanganyiko ni zaidi ya mwezi sasa. Sasa wataalam naombeni mnisaidie. Nifanyeje? Wakala wa ndege nimeshakata ticket kwao mara nyingi na ni watu genuine, na ni kweli nilitakiwa niconfirm malipo ili wakamikishe booking lakini nikashindwa kufanya hivyo kutokana na kadi kuwa expired and deleted na wao kucancel booking.
Hela yangu iko wapi?
Na naipataje?