Msaada wa maoni kuhusu ununuzi wa kiwanja

Msaada wa maoni kuhusu ununuzi wa kiwanja

Manzile

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2020
Posts
701
Reaction score
1,900
Wakuu habari zenu.

Kuna kiwanja Kiko sehemu nzuri sana kimetangazwa kuuzwa.

Mwenye kiwanja alishafariki, alikuwa anaishi na mwanamke lakini walitengana kabla marehemu hajafa, na baada ya kufariki familia ilimpa baadhi ya maeneo mke walietangana Ili aweze kumudu kuwahudumia watoto alioacha marehemu.

Huyu Marehemu ana watoto wengi Kwa wanawake tofautitofauti.

Kwa ishu kama hii inatakiwa document zipi kutoka Kwa muuzaji Ili eneo lisije kuniletea mgogoro baadae.
 
Msimamizi wa mirathi ndiye mwenye mamlaka ya mali za marehemu kuzigawa kwa would be beneficialies! short of that, kesho itakuleta matatizo akitokea mtu kudai kiwanja hicho.
 
Wewe kiwanja cha nini njoo huku
290245651.jpg
 
Tupeane deals, kama kuna vingine bei nzuri tuambiane
 
Kwa hiyo hapa mkuu nadeal na msimamizi wa mirathi?
Mtu akisha kufa mali zake zinakuwa under probate and administration law, short of that chote utakachokifanya kabla ya mirathi ni batili
 
Viwanja ambavyo n vya uridhi n vya kuachana navyo tuu ...migogoro yake haiishagi afu pia Vina usumbufu mwingi yan hautakua na Amani coz hapo ushasema ana watoto wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki kiwanja kipo sehemu nzuri sana ngoja niendelee kufuatilia taratibu ambazo hazitoniletea shida baadae ikishindikana naachana nacho ila sitaki nikipoteze
 
Hiko kiwanja lazima ujue kama kimepimwa au laa... Kina hati au kimewah kuombewa hati... Kina barua ya offer au laa... Kinamilikiwa kwa documents zipi hasa... All in all lazima umhusishe mwanasheria, lazima watoto wake na msimamizi wa mirathi wahusishwe ktk uuzaji ili kesho wasije kukugeuka...
 
Hiki kiwanja kipo sehemu nzuri sana ngoja niendelee kufuatilia taratibu ambazo hazitoniletea shida baadae ikishindikana naachana nacho ila sitaki nikipoteze
Sikio LA kufa halisikii dawa ,viwanja vipo vingi.
 
Hiko kiwanja lazima ujue kama kimepimwa au laa... Kina hati au kimewah kuombewa hati... Kina barua ya offer au laa... Kinamilikiwa kwa documents zipi hasa... All in all lazima umhusishe mwanasheria, lazima watoto wake na msimamizi wa mirathi wahusishwe ktk uuzaji ili kesho wasije kukugeuka...
Wote wapo, na kimepimwa
 
Viwanja ambavyo n vya uridhi n vya kuachana navyo tuu ...migogoro yake haiishagi afu pia Vina usumbufu mwingi yan hautakua na Amani coz hapo ushasema ana watoto wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo akimbie hata asigeuke nyuma.
Unaweza fata utaratibu na bado ukaja pata vikwazo huko mbele.
Unanunua kitu vizuri baadae kinakuja kuwa kero.
 
Back
Top Bottom