Msaada wa mawazo anayeju taasisi ya kifedha inayotoa mikopo kwa wakulima.

Qualifier

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2012
Posts
1,252
Reaction score
405
Ndugu wana jamvi, nimekuja hapa uwanjani petu huku nikijua kabisa kuwa humu ndani ya JF kuna wataalamu wa kada zote na ninaamini hakuna hoja inayotelewa humu akakosekana mtaalamu mwenye majibu sahihi, achilia mbali wale watoto wetu wanao suburi majibu ya mitihani ambao huwa wanaanza kejeli badala ya kuchagia kwa lengo la kumsaidia mtoa maada. Mimi ninampango wa kuanzisha kilimo cha kisasa cha migomba, ninakusudia kufungua shamba kubwa lisilo pungua ekari 50 nifunge mitambo ya umwagiliaji, nijenge green house kwa ajili ya tissue culture nk ,. Tatizo ni kwamba sina mtaji, shamba ninalo na lina hati ya kumiliki. Je nitaasisi gani ya kifedha inaweza kunipa mkopo kiasi cha Million 100? Je! Nitumie tararibu gani kuupata mkopo huo na kutumi hati za shamba kama modgej? Ninaamini wazo langu litawagusa wataalamu waliomo humu na kunisaidia kupata ufumbuzi NINAOMBA KUWASILISHA
 
Nenda TIB wanatoa hiyo mikopo ya wakulima
 
milioni 100 marejesho muda gan

TIB wana dirisha la kilimo nenda, ila inaanzishwa bank ya wakulima out of hilo dirisha la kilimo.

Other than that that nenda kwa local community bank kama ipo katika eneo lako, TIB wame channel hiyo mikopo kupitia hizo community banks, ila wanatoa max 50million kwa riba ya 2% kwa mwezi x 12 inakuwa 24% kwa mwaka
 
Mkuu local community banks ni benki gani?
 
pride tanzania rfw ltd-ni kampuni tanzu ya pride tanzania itoayo mikopo vijijini kwa kuamngalia mazao maalum na mazao aina mbalimbali waone hawa jamaa wako nondo
 
pride tanzania rfw ltd-ni kampuni tanzu ya pride tanzania itoayo mikopo vijijini kwa kuamngalia mazao maalum na mazao aina mbalimbali waone hawa jamaa wako nondo

Hiyo ya pride mpaka vikundi kuanzia watu 20, alafu wanaanzia mkopo wa Tsh 200,000
 
hapana ni watu 10 n ipo ikopo ya muda mfupi ya watu watano hii ni kwa ajili ya wakulima wadogo waliopo vijijini amount ni sh 300000 kwa mkopo wa kwanza mkulima mkubwa nenda benki uwe na hati ya nyumba mjini na biashara inayoeleweka
 
Kimpango, TIB hapo kwenye biashara inayoeleweka ndo magumashi yanaanza kuna bank statement, kuna sijui idadi ya wateja na contact zao, cashflow ndo hiyo kwenye statement nafikiri, Tin na company registration then utaambiwa vya miaka 3 kuendelea....... Bora kuanza mdogo mdogo au ujiunge kikundi
 
hapana ni watu 10 n ipo ikopo ya muda mfupi ya watu watano hii ni kwa ajili ya wakulima wadogo waliopo vijijini amount ni sh 300000 kwa mkopo wa kwanza mkulima mkubwa nenda benki uwe na hati ya nyumba mjini na biashara inayoeleweka

Acha uongo mkopo rfw unaanzia laki mbili na vikundi ni sawa kuanzia kumi
 
hapana ni watu 10 n ipo ikopo ya muda mfupi ya watu watano hii ni kwa ajili ya wakulima wadogo waliopo vijijini amount ni sh 300000 kwa mkopo wa kwanza mkulima mkubwa nenda benki uwe na hati ya nyumba mjini na biashara inayoeleweka

Biashara ndio wanaanzia laki tatu
 
Biashara ndio wanaanzia laki tatu
nabishana na mkopaji? sina hisa na kampuni lakini kikubwa ni mikopo inatolewa kuanzia laki 3 mpaka milioni nne kwa wakulima wenye shida wafike oficini kwao wataelezwa zaidi
 
Tatizo pride wanataka marejesho+akiba kila wiki na mmoja wenu asipoleta rejesho mnamchangia,utakuta mpaka unamaliza mkopo gharama ishakuwa mala mbili ya mkopo, nenda vikoba mtaani kwako. Ila kuna kampuni ya vikoba eti wanatoa mikopo kwa njia ya mtandao hebu google
 
We mkopaj mi BM ya branch manager wa tawi mojawapo la pride rfw,pole sana kama umekuja kupotosha
 
nabishana na mkopaji? sina hisa na kampuni lakini kikubwa ni mikopo inatolewa kuanzia laki 3 mpaka milioni nne kwa wakulima wenye shida wafike oficini kwao wataelezwa zaidi

Kaka nisaidie hilo tawi ambalo rfw kwa mkulima wanatoa kuanzia lak tatu had milioni nne,we mkopaji ila mi ni mfanyakaz labda itatusaidia kujua tawi hilo hiyo policy wameitoa wapi? Au ukir kuwa unadanganya,maana atakwenda mtu.ataambiwa kitu tofaut atakuja kupost kitu kibaya kwa shirika letu,mikopo ipo ya ujenz na.sio kwa mataw yote,ipo mikopo pia ya aina tofaut lakin kwa kilimo nopppp,we mkopaj mi afsa wako,nitajie tawi plzzzz
 
We mkopaj mi BM ya branch manager wa tawi mojawapo la pride rfw,pole sana kama umekuja kupotosha

bm ya branch manager wa tawi...teh teh teh .. pride wana hasara sana
 
bm ya branch manager wa tawi...teh teh teh .. pride wana hasara sana

Mkuu hayo ni matatizo ya kiuandishi nilitaka kuandika yaan branch manager au hata hilo ni tatizo mkuu,njoo na hoja acha kuparamia mambo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…