Qualifier
JF-Expert Member
- Dec 14, 2012
- 1,252
- 405
Ndugu wana jamvi, nimekuja hapa uwanjani petu huku nikijua kabisa kuwa humu ndani ya JF kuna wataalamu wa kada zote na ninaamini hakuna hoja inayotelewa humu akakosekana mtaalamu mwenye majibu sahihi, achilia mbali wale watoto wetu wanao suburi majibu ya mitihani ambao huwa wanaanza kejeli badala ya kuchagia kwa lengo la kumsaidia mtoa maada. Mimi ninampango wa kuanzisha kilimo cha kisasa cha migomba, ninakusudia kufungua shamba kubwa lisilo pungua ekari 50 nifunge mitambo ya umwagiliaji, nijenge green house kwa ajili ya tissue culture nk ,. Tatizo ni kwamba sina mtaji, shamba ninalo na lina hati ya kumiliki. Je nitaasisi gani ya kifedha inaweza kunipa mkopo kiasi cha Million 100? Je! Nitumie tararibu gani kuupata mkopo huo na kutumi hati za shamba kama modgej? Ninaamini wazo langu litawagusa wataalamu waliomo humu na kunisaidia kupata ufumbuzi NINAOMBA KUWASILISHA