Msaada wa mawazo: Kubadilisha nyumba ya makazi kuwa gesti

Msaada wa mawazo: Kubadilisha nyumba ya makazi kuwa gesti

Dodoma moja

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Posts
307
Reaction score
182
Poleni na majukumu wakuu, naombeni mawazo yenu binafsi nimefanikiwa kujenga nyumba ya room 3 zote master, sitting room kubwa, dinning, jiko, stoo na public toilet na kwa sasa nimeshaipaua nategemea kuingia kwenye hatua ya finishing. Baada ya kufika hatua hii likaja wazo kuwa huko mbeleni nije kuibadilisha nyumba hii kuwa gesti kwa kuwa mazingira hayajanifurahisha sana lakini kwa gesti yanafaa sana hivyo nina mpango wa kuishi angalau miaka mitatu mbele panapo uzima then nipageuze sehemu ya biashara. Lakini nimeona nije nipate mawazo yenu wadau wa ujenzi hasa ninapoingia katika hatua hii ya finishing niifanye vipi ili nitakapoanza mchakato wa kuibadilisha kuwa gesti house nisitumie gharama kubwa sana katika ukarabati maana najua kutakuwa na sehemu za kubomoa na kuongeza vitu.
Nawasilisha.
 
Nadhani ukiwatafuta mafundi ujenzi unaowaamini, ukawapeleka site, ukawaonyesha nyumba na malengo yako ya baadae, wanaweza wakakushauri vizuri zaidi kuliko sisi tusioifahamu nyumba, achilia mbali ramani yake, wala mkoa na center iliyopo.
 
Back
Top Bottom