Msaada wa mchanganuo wa bei na miundombinu kuanzisha kituo cha mafuta (petrol station)

Msaada wa mchanganuo wa bei na miundombinu kuanzisha kituo cha mafuta (petrol station)

Nadhani gharama kubwa ipo kwenye kupata eneo/kiwanja. Kumbuka filling stations nyingi/zote zipo pembezoni mwa barabara, mfano tu kutoka Mbezi mwisho kuelekea Goba kuna station inajengwa, nimesikia jamaa wamenunua eneo kwa 600ml, ukijumlisha na gharama za ujenzi, ununuzi wa mashine, tanks etc lazima 1.2bl itakata tu.
Aisee... Angalau nimepata mwanga mkubwa. Asante.
 
wakuu, naona kuna shida hapa kuwa hakuna mtu ambaye ana ufahamu wa haya mambo kwa ufasaha.
kwa uwazi aliyesema milioni mia 7, alikuwa yuko sahihi zaidi, ila kwa mikoani hata mwenye mtaji wa milioni chini ya mia 2, anaweza
Naomba mniamini tu, nimewahi pitia hilo, nalifahamu, ngoja niweke mchanganuo hapa. Nitazame kwanza wapi niliweka.
 
Ingia ubia na mwenye kiwanja..
Jenga, endesha, faida mtagawana.
Sijui kuhusu maroli ya mafuta yapo mengi tu kukodi na wengine watakufuata
Tena wauza mafuta wa jumla wakiona unajenga shell wanakutafuta wenyewe.., si ajabu hata hizo pump watakupa na hata standby jenereta nalo utapewa na wewe utawalipa kidogokidogo..
Kwa sababu nao hutafuta masoko ya mafuta na vilainishi vyao..
Hakuna kinachoshindikana kwenye ulimwengu wa biashara...
 
Hii Ni tabia ya sisi watanzania, mtu anakurupuka na kusema tu billion mbili. Wala hajui Kama Kuna categories za vituo, ukubwa wa Tank, mode of operation etc.

Tunapenda kijifanya tunajua kila kitu na kukatishana tamaa.

Kimsingi Kuna two category filling station au kituo kidogo eneo lake lazima liwe so chini ya 600sqm. Walau liwe na pump mbili, ukubwa wa Tank itategemea na uwezo wa mmiliki lakini so chini ya 30,000 liters.

Kuna kituo kikubwa Petrol Service station ambacho eneo lake sio chini ya 2000sqm, pump zaidi ya nne, Kuna car service, restaurant/kiosk.

Kituo kikubwa kinagharimu Kati ya 300 - 400ml kukijenga kidogo Ni Kati ya 90m - 150m kulingana na upatikanaji wa eneo na material.

Matenk Ni Kama 15m lenye ujazo wa 20,000 pump 10 - 15m.

Mafuta unaweza kuingia ubia na wasambazaji ama ukanunua na kuuza.
Kila Lita ina margin Kati ya 65 - 130.

Hivyo unaweza kufanya hesabu zako hapo

Tusikashinane tamaa.

Kama hujui kaa kimya like unachokijua hata Kama Ni kidogo sema lakini kukatishana tamaa
 
Ingia ubia na mwenye kiwanja..
Jenga, endesha, faida mtagawana.
Sijui kuhusu maroli ya mafuta yapo mengi tu kukodi na wengine watakufuata
Tena wauza mafuta wa jumla wakiona unajenga shell wanakutafuta wenyewe.., si ajabu hata hizo pump watakupa na hata standby jenereta nalo utapewa na wewe utawalipa kidogokidogo..
Kwa sababu nao hutafuta masoko ya mafuta na vilainishi vyao..
Hakuna kinachoshindikana kwenye ulimwengu wa biashara...
Mkuu, umenipa mwanga mkubwa kiukweli. Nimeshaonza pakuanzia.
 
Back
Top Bottom