Kwa kawaida seller atakwambia njia zipi anatumia kulingana na nchi aliyopo,mfano Marekani kuna USPS (united states postal service), UPS Expedited, DHL and EMS. Hizo zote isipokuwa USPS ni international shipping companies na zipo karibu nchi zote.
Sasa basi, kwa kutegemea company gani inasafirisha mzigo wako ndo itadetermine wapi utapokelea mzigo, Mfano mimi nikitumiwa kwa DHL huwa wananiletea hadi nyumbani/ofisini maana wao hawatumii anuani za P.o. Box, wanataka anuani watakayokuletea hadi mlangoni, utaandika jina lako, ofisi gani upo au mtaa gani, nyumba namba ngapi, jiji na nchi ulipo unamalizia na namba za simu. Na kama utatumia anuani ya P.o.Box kuna garama inaitwa remote area charge USD30 itaongezeka, na wakiona vipi watakupigia simu ukachukue kwenye ofisi zao zitakazokuwa karibu. Huo utaratibu wanao pia UPS ila EMS wao wanatumia hata P.o. Box hivyo utachukulia kwenye sanduku lako la posta.
USPS, China Post, HongKong Post na mashirika mengine ya posta ya taifa huwa yanaleta kwa kupitia anuani za P.o.Box ila huwa zinachelewa ukilinganisha na express kama DHL,EMS na UPS.
Mimi huwa napokea mizigo karibu kila mwezi kwa kila aina ya shipping company hadi Bandari (sea freight), maana huwa naimport vitu vikubwa na vidogo yakiwemo magari na mitambo mbalimbali.
Kama una maswali zaidi endelea kuniuliza maana JF ni msaada wetu hata mimi nimesaidiwa sana hapa JF.