Saidy Januzaj
Member
- Apr 13, 2014
- 69
- 10
naombeni mnifahamishe full system yakununua kitu online kupitia ebay na vp utakipata kitu hico...please wajuzi nisaidieni
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwanza fungua account ya ebay ambapo ktk ac hiyo utaweka anuani yako ya kupokelea bidhaa.
Pili, fungua account ya malipo kwa mtandao ya PayPal ambapo utaunganisha debit/credit card yako (ATM card number na iwe imewezeshwa kununua online kupitia VISA au MasterCard).
Tatu, unapoingia ebay kuna bidhaa zinazouzwa kwa mnada (bid) na zile zinazouzwa kwa fixed price (buy now). Ukichagua bidhaa yenye bid utajikuta unashindana na wenzio hadi ukiwashinda kwa dau la juu basi utakua umejicommit kuinunua hiyo bidhaa na lazima uinunue kwani usiponunua utafunguliwa kesi na ebay ambayo inaweza kukupa negative feedback ktk account yako na pia ukiendelea utafungiwa kununua ebay. Kuhusu bidhaa ya buy now, hiyo ni nzuri kwani utakuta hadi shipping cost imewekwa na kama haijawekwa pia hautajua lakini estimations zitakuwepo pale.
Nne, ukisha jicommit kununua kitakachofuata ni seller atakutumia invoice nawewe utatakiwa kulipa kwa PayPal na utachagua anwani gani bidhaa itumwe.
Tano, seller atakutumia mzigo wako na ata upload tracking number kwenye PayPal na ebay, na wewe utaweza kufuatilia kujua mzigo wako umefika wapi hadi utakapoupokea.
Hayo na mengine kwa mfano incase mzigo haujafika au umekuja kinyume na ulivyokuwa, kuna Resolution Center ktk PayPal unaweza kufungua case na mtasuruhishwa na mkishindana paypal itaamua kesi yenu kama ni hela urudishiwe au la, maana hadi mda huo seller atakua hajapewa hela yake.
Nikali ninayo mengi ya kukwambia lakini sitayamaliza kwa muda huu. Ukiwa na swali zaidi utaniuliza.
Nawasilisha
ahsante sana kunifahamisha vya kutosha(konzogwe)..ila hapo kwenye kutumiwa mzigo sijafahamu vizuri..hebu niambie wew kama ushawahi kununua bidhaa ebay ulitumia njia zipi hadi mzigo ukakufikia..yaani ni wapi ulikwenda kuuchukua huo mzigo...pls nifahamishe zaidi
Kwa kawaida seller atakwambia njia zipi anatumia kulingana na nchi aliyopo,mfano Marekani kuna USPS (united states postal service), UPS Expedited, DHL and EMS. Hizo zote isipokuwa USPS ni international shipping companies na zipo karibu nchi zote.
Sasa basi, kwa kutegemea company gani inasafirisha mzigo wako ndo itadetermine wapi utapokelea mzigo, Mfano mimi nikitumiwa kwa DHL huwa wananiletea hadi nyumbani/ofisini maana wao hawatumii anuani za P.o. Box, wanataka anuani watakayokuletea hadi mlangoni, utaandika jina lako, ofisi gani upo au mtaa gani, nyumba namba ngapi, jiji na nchi ulipo unamalizia na namba za simu. Na kama utatumia anuani ya P.o.Box kuna garama inaitwa remote area charge USD30 itaongezeka, na wakiona vipi watakupigia simu ukachukue kwenye ofisi zao zitakazokuwa karibu. Huo utaratibu wanao pia UPS ila EMS wao wanatumia hata P.o. Box hivyo utachukulia kwenye sanduku lako la posta.
USPS, China Post, HongKong Post na mashirika mengine ya posta ya taifa huwa yanaleta kwa kupitia anuani za P.o.Box ila huwa zinachelewa ukilinganisha na express kama DHL,EMS na UPS.
Mimi huwa napokea mizigo karibu kila mwezi kwa kila aina ya shipping company hadi Bandari (sea freight), maana huwa naimport vitu vikubwa na vidogo yakiwemo magari na mitambo mbalimbali.
Kama una maswali zaidi endelea kuniuliza maana JF ni msaada wetu hata mimi nimesaidiwa sana hapa JF.
C2c na b2b ndo nini
Sijaelewa kwa hapo
Asante sana
Your of great help
Hivi izo online store ulizotaja apo kama vile ipmart, ahappydeal na nyinginezo mbona watu hawazitumii au hazipo safe
Kweli elimu tatzo
So unaweza ukanunua mzigo mkubwa kwa ajili ya biashara kutoka ebay wa ka vile 10 millions alafu ukawashipped mpaka kwako
Au hio unaitaji uende kwenye b2b online stores
Na kama ndio yawezekana ipi ni online store kwa ajili ya b2b na ambayo ipo safe
Thanks in advance
Mi naomba kujua kuhusu kodi. Nasikia vitu kama simu lazima ulipe kodi. Je, hiyo kodi italipwa point ipi? Mfano, Mimi nipo Tabora, mzigo utakaa TRA dar hadi nilipe kodi au utashikiliwa Tabora
Kama utakuja kwa DHL, ukifika airport Dar watakupigia simu kuomba TIN namba yako (na hili swala la TIN ni mhimu kama unaimport vitu), pia watakwambia mzigo wako unadaiwa ushuru kiasi gani then ww utawapa go ahead waprocess na wakimaliza utakuja kulipia hapohapo Tabora au popote watakapo kuletea mzigo ndo hapo unalipia.
Kwa posta pia utalipia kwenye posta ya sanduku lako wala huna shida ya kwenda Dar
Kama utakuja kwa DHL, ukifika airport Dar watakupigia simu kuomba TIN namba yako (na hili swala la TIN ni mhimu kama unaimport vitu), pia watakwambia mzigo wako unadaiwa ushuru kiasi gani then ww utawapa go ahead waprocess na wakimaliza utakuja kulipia hapohapo Tabora au popote watakapo kuletea mzigo ndo hapo unalipia.
Kwa posta pia utalipia kwenye posta ya sanduku lako wala huna shida ya kwenda Dar