Kwa maoni yangu nashauri huyu rafiki yako amekurupuka sana kuanzisha mahusiano mapya huku akiwa bado yupo katika complicated relationship na huyu baba mtoto wake.
Hili ni jambo muhimu sana kuzingatia unapoanza uhusiano na binti, ni vema sana kujua alipotoka kimahusiano na alimalizana vipi na mtu aliyekuwa uhusiano wa mwisho.
Kuna mtu anamuacha mwenzake kimya kimya bila mazungumzo, majadiliano wala kumalizana kokote yaani akili za kitoto kabisa.
Matokeo yake anaanzisha mahusiano na mtu mpya ambaye anaingia na kukutana na mifarakano isiyo na mbele wala nyuma ambayo inavuruga hata amani ya uhusiano mpya.
Huyo ni mtu ambaye amepata nae mtoto. Anaweza kuwa ni mkorofi au wameshindwana ila alitakiwa wakae chini na watu wazima kisha wayamalize na kukubaliana juu ya malezi ya mtoto na namna watashirikiana.
Hizi ndio shida za kuvutana magetoni na kunyanduana kizembe kisha ujauzito juu mnaaza kuvurugana baadae sababu hamkwenda kiutaratibu na kwa kufuata misingi na taratibu zinazotakiwa kijamii kuishi pamoja.
Mwambie rafiki yako kabla hajaenda polisi akumbuke huyo anaekwenda mchukulia restraining order ni baba wa mtoto wake.
Pengine huyo mwanaume bado anamhitaji na sababu anamfanyia fujo ni hofu ya kutojua yeye, rafiki yako na mwanae wanakwenda wapi na kuishi na nani. Ni vema akamtafuta akiwa na wazee wakae wayazungumze na aeleweshwe ili yasijekutokea mengine.
Na nyie watoto wa kike siku hizi mna mambo ya kibwege sana kulala na mtu hujui hata familia na historia yake ipoje. Wengine ni vichaa wa akili huwa vinalala tu na kuibuka kipindi fulani fulani.
Sent using
Jamii Forums mobile app