Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sio kwamba waliipata cm ya dada yako bali hizo sms wanazituma kwa computer, ni wezi hao wameibia mawakala wengi mnoYaani hata hatujui ndugu, na outsms kwenye simu ya Dada hizo hazipo
Kuna matapeli wamenipiga ambao hutumia #za tigo.
Story yenyewe iko hivi,
Nimepokea sms kutoka simu ya dada yangu ikinielekeza kutuma pesa 250,000 kwa mtu kwani anashida sana, na akanitumia namba ya huyo mtu na jina lake, muda mfupi baada ya ujumbe kuingia huyo mtu akanipigia kama nimepata ujumbe wa dada na kudai kuwa nimsaidie haraka, nikampigia dada kuconfirm hakupokea huku nikisumbuliwa na huyu MTU, nikaona isiwe tabu wacha nimsaidie, nikatuma Tigo pesa. Na ujumbe wa kuonyesha pesa imekwenda nikafoadi kwa dada. Dada alinipigia baada ya muda kuliza ule ujumbe nikamjulisha kilikuwa ni kitu kigeni kwake. Nikascreeshot nikamtumia kashangaa sana. Kwenda tigo ile namba haipatikani hata baada ya kupata ile pesa hakuna simu ya shukrani. Pesa katoa na simu haipatikani.
Baada ya muda nikapokea ujumbe mwingine kutoka kwa dadangu huyohuyo ukinitaka nimsaidie mtu mwingine 400,000 jina na nambayake, huyu wa sasa akapiga simu namba tofauti na ile ya kwanza hata sauti pia akijieleza kwa jinsi walivo karibu na Dada hivyo Dada kaniomba nimsaidie.
Kwa kuwa mchezo nilishaujua nilimuomba tuonane nimpe cash alinisihi sana nimtumie coz kabanwa hawezi toka nikaona isiwe tabu nimfate aliponielekeza nimpe mpunga. Kufika maeneo Yale simu imezimwa.
Nimelizwa jamani nitapaje jasho langu.
Pole sana mkuu. Umenikumbusha maumivu ya kupigwa na tapeli 6M, tapeli huyu nashindwa kumkamata kwan anakula na Polisi wa kituo cha Chuo na pale kwenye mabati.