Msaada wa sheria ya ajali na mwanasheria

kedekede

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
5,313
Reaction score
7,714
Wana J-f
Poleni na majukumu,nina mdogo wangu wa kike alipata ajali na kukatwa mguu mmoja juu ya goti.Ajali ni kwamba alikuwa kituo cha daladala gari la mtu binafsi likapoteza muelekeo na kumgonga,matokeo yake hospitali hatimaye mguu ukakatwa.Yote tumemshukuru Mungu.Tulihangaika kumtibu na sasa anaendelea vizuri tu psycologically.
Tumefuatilia insurance na mawakili mbalimbali wamefuatilia lakini matokeo ni kwamba anatakiwa alipwe tu milioni 8.Sisemi malipo yoyote yale yanaweza kuurudisha mguu wake lakini nadhani kuna mambo nyuma ya pazia na hawa mawakili.Nadhan mguu wa bandia its more than 20m,mbona haya malipo hayaendani na madhara ambayo yametokea?au insurance haiangalii vitu hivyo wakati wa malipo?Hatuna uwezo wa kulipa wakili tena ila naomba kama kuna mwanasheria anifafanulie utaratibu na pia ikiwezekana atusimamie na malipo yawe baada ya kesi kuisha.Yeyote anaweza kuchangia lakini katika hili sihitaji masikhara kwa maumivu tuliyonayo.ukiona huna cha kuchangia kuliko kuniudhi nakuomba nisamehe tu pita.
 
pole sana kiongozi,muwe na moyo wa uvumilivu kwenye kufuatilia masuala maana yana nyuma ya pazia sana. ngoja waje wanasheria watujuze kwa faida ya wote
 
Kama utaweza kufika kwenye ofisi za TIRA, watakupa ufafanuzi mzuri na kuilazimisha iyo kampuni kukulipa kisawasawa.
 
pole sana kiongozi,muwe na moyo wa uvumilivu kwenye kufuatilia masuala maana yana nyuma ya pazia sana. ngoja waje wanasheria watujuze kwa faida ya wote
Asante Jembekillo Mungu yu pamoja nasi!
 
Headquarters
TIRA HOUSE, Block 33, Plot No. 85/2115, Mtendeni Street,
P. O. Box 9892,
DAR ES SALAAM - Tanzania
Tel:+255(022)2132537/2116120/2116131
Fax: +255(022)2132539
Email: coi@tira.go.tz
Website: www.tira.go.tz
Asante sana mkuu je hawa ni huru au ndio haohao wanajuana tena na insurance zote kwa hyo ni mambo ya nyuma ya pazia bado?samahan kwa usumbufu na asante sana tena!
 
Ni jukumu lao kusimamia Insurance companies kutenda haki kwa wateja wake. Na sidhani kama watakua hivyo.
 
much respect to u kaka kisu cha ngariba umetoa maelekezo murua kabisa. wanasheria pia mnasemaje tupeni ufumbuzi kupitia sheria
 
Juzi kati nikiwa katika hiace tuligongwa nyuma na landcruser impact ilikuwa kubwa tuliumia shingoni trafik alipima ajali pale baadae me na mwenzangu tukamfata trafiki kwamba atupe Pf3 tunahisi tumeumia.akatuandikia ili tuende hospitali sasa hapo nataka kujua hii kesi nalipwa vipi maana nimetumia pesa zangu hospitali na zile gari zimeachiliwa bila hata sisi kupigiwa simu kuhusu madai yetu.naombeni ushauri hapo unafanyaje
 
Wana J-f
Poleni na majukumu,nina mdogo wangu wa kike alipata ajali na kukatwa mguu mmoja juu ya goti.Ajali ni kwamba alikuwa kituo cha daladala gari la mtu binafsi likapoteza muelekeo na kumgonga,matokeo yake hospitali hatimaye mguu ukakatwa.Yote tumemshukuru Mungu.Tulihangaika kumtibu na sasa anaendelea vizuri tu psycologically.
Tumefuatilia insurance na mawakili mbalimbali wamefuatilia lakini matokeo ni kwamba anatakiwa alipwe tu milioni 8.Sisemi malipo yoyote yale yanaweza kuurudisha mguu wake lakini nadhani kuna mambo nyuma ya pazia na hawa mawakili.Nadhan mguu wa bandia its more than 20m,mbona haya malipo hayaendani na madhara ambayo yametokea?au insurance haiangalii vitu hivyo wakati wa malipo?Hatuna uwezo wa kulipa wakili tena ila naomba kama kuna mwanasheria anifafanulie utaratibu na pia ikiwezekana atusimamie na malipo yawe baada ya kesi kuisha.Yeyote anaweza kuchangia lakini katika hili sihitaji masikhara kwa maumivu tuliyonayo.ukiona huna cha kuchangia kuliko kuniudhi nakuomba nisamehe tu pita.
Kwanza natoa pole sana kwa masahibu yaliyowakuteni, ndio mambo ya maisha lakini. Nikija kwenye suala lako, hujafafanua vizuri kuhusu hiyo milioni 8 kama ilikubaliwa kulipwa na kampuni ya bima katika majadiliano nao au kwa amri ya mahakama (yaani hujasema kama malipo yalifikiwa nje ya mahakama bila kuwapo kesi ya madai au kwamba mlifungua kesi ya madai mahakamani).
Kama kulikua na kesi mahakamani na mahakama ndio ikatoa maamuzi hayo maana yake unachotakiwa kufanya ni kukata rufaa (uzingatie na muda wa rufaa kama bado unaruhusu) katika mahakama ya juu ili upinge hicho kiwango lakini ukiwa na sababu za msingi

Kama malipo haya yalifikiwa kwa majadiliano tu kati ya kampuni ya bima na nyie basi unaweza kwenda mahakamani kupeleka madai yako japo njia hii itarefusha sana suala lako na gharama (nimezingatia uliposema huna hela kwa sasa na pia upo songea).
Pia kama ushauri ulivyotolewa hapo awali, natumai uliwasilisha hoja yako TIRA, unaweza kutuambia nini walichokushauri.

Kuhusu mwanasheria, huwezi kumpata kwa makubaliano ya namna hiyo maana ni kosa kwake kufanya hivyo ila unaweza kwenda kwenye ofisi za taasisi zinazotoa misaada ya kisheria, wanaweza kukusaidia kwa wewe kuchangia gharama ndogo au kwa kutochangia kabisa.
 
Hiyo offer ya milioni nane alisaini? Kama alisaini na kulipwa maana yake alikubaliana na malipo hayo.

Kama hajasaini ni vyema uende Tira kama wengine walivyoshauri. Halafu nimeshangaa sana Mwanasheria kushindwa kukushauri kuhusu hilo!!

Ni vyema hoja zako utakazopeleka Tira ziwe nzito kwa sababu itakuwa reference ya maamuzi.
 
Back
Top Bottom