Msaada wa ushauri biashara gani hasa nifanye kwa 30m capital

KasomaJr

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
367
Reaction score
141
Habari wana JF,
Nakuja mbele zenu kuomba ushauri kwenu, ushauri wenu uzingatie mambo yafuatayo.

CAPITAL/LOAN:
Nimeamua kuchukua Loan ya 30M bank flani na nyumba yangu nimeamua kuweka rehani kabisaaa kwa kujua kabisa kama sitaweza kulipa nyumba yangu itachukuliwa, nimefanya hivyo kwa kuzingatia return nayoipata kwenye yumba hiyo ni kidogo sana, 150,000/= per month, a 3 bedroom, one ni master, ina kitchen na sitting room, ipo eneo ambalo ni potential sana na ina kiwanja kikubwa kwa maana ya kwamba hiyo ni nyumba ya uani, mbele kuna kiwanja kikubwa cha kuweza kujenga hata ghorofa/hotel yenye uwezo wa kuwa na rooms 15-20.

INTEREST/DREAM/CALLING
Ukweli wa moyo wangu naamini kabisa katika kilimo ingawa nimewahi kufanya attempt moja amabyo haikufanikiwa katika kilimo ya matikiti maji huko Manyara, lakini najua kabisa tatizo ilikuwa usimamizi mzuri (kwani vijana niliowaweka hawakuwa serious na kazi na mimi nilikuwa kwenye michakato ya kwenda nje kikazi, hivyo muda mwingi nikautumia kufuatilia visa na nk). Hivyo katika suala hili nataka kujua ni kilimo gani kinaweza kunipa return haraka na ni risk free ili kuweza kuanza kulipa loan.

Hivyo basi naomba ushauri kwa kuzingatia haya yafuatayo pia;
1. Kuanzisha green house nyumbani kwangu kwakua bado nina eneo la kuweza ku-accomodate
2. Kununua shamba maeneo ya Mwasonga kiasi cha ekari 2 kwa ajili ya shughuri za ufugaji kuku wa kienyeji, samaki hata bwawa moja, greenhouse na kilimo cha matikiti maji
Hapa nitaomba uzoefu wa gharama kama za kuchimba kisima, fensing ya wire na vitu vingine muhimu.

BIASHARA YA STATINARIES/INTERNET CAFE
Nimewaza kufanya biasha hii na nimeifanyia utafiti kwa kiasi flani, nilitaka kuweka internet cafe maeneo ya Ferry kigamboni lakini ambayo ingekuwa modern kidogo, na capita investment ilikwenda karibu 12M lakini nikifanya analysisi ya return naona kama ni ndogo sana ukilinganisha na capital investment. Hivyo naomba ushauri kwenye eneo hili kwa mutu amabe anao uzoefu wa kutoksha. Kwenye eneo hili business mix yangu ilikuwa ni pamoja na
1. Printing
2. Photocopying
3. M-PESA/Tigo Pesa/ Airtel Money
4. Air ticketing
5. Kuatafuta kazi za nje za printing/ supply ya stationaries
6. Internet cafe ambayo itakuwa na wireless lakini ikiwa controlled na mambo ya downloads na time
Si kuwa na mpango wa kuweka stationaries nyingi hata kidogo

BIASHARA YA USAFIRISHAJI/ NA MAZAO
Nimepewa ushauri kwamba biashara ya chakula inalipa sana, yaani kuuza unga, maharage, sukari, mafuta nk...na hii wife yeye anai support ingawa moyo wangu haunipi hata kidogo, na katika hili tulipaswa tununue hata carry au Noah kwa ajili ya kusambaza mizigo kwa wateja lakini wakati huo huo gari itumike kibishara kwa maana kwamba kama ni Carry basi itaweza kufanya shughuli za kubeba mizigo ya wateja nje ya biashara yetu, na kama ni Noah basi iwe mult-pupose kwa maana ya kwamba itatumika kwa biashara yetu na familia pia.

Jamani am confused, nahitaji msaada wenu kwa kujua na kuzingatia JF ni kisima cha maarifa, kimejaa watu makini, weledi na wenye uzoefu mkubwa kabisa katika maisha haya.
Asanteni na mungu awabariki sana.
 
Mi ningekushauri ubaki hukohuko kwenye kilimo kwakua ushajua ni wapi ulifanya kosa mpaka tikiti likawa halijakulipa.Ila ningekushauri utoke kivingine km vile tango.linalipa tena kwa mda mfupi yaani SK 45 isipokua unatakiwa usimamizi Wa karibu.kwa tikiti sasa hivi halilipi sn kwsbb limejaa sana sokoni.hata mi limenitoa kapa.
 
njoo kwenye dala dala iyo hela yako unapata HIACE MBILi na kwa mwezi mm nitakuwekea 4ml.kwa gari zote mbili .zaidi njoo pm
 
Mi ningekushauri ubaki hukohuko kwenye kilimo kwakua ushajua ni wapi ulifanya kosa mpaka tikiti likawa halijakulipa.Ila ningekushauri utoke kivingine km vile tango.linalipa tena kwa mda mfupi yaani SK 45 isipokua unatakiwa usimamizi Wa karibu.kwa tikiti sasa hivi halilipi sn kwsbb limejaa sana sokoni.hata mi limenitoa kapa.

Mwita asante sana Kwa ushauri wako, nitaufanyia kazi ndugu yangu.
 
mi nakushauri ulime ndizi za kupika (plantains) maeneo ya moro. tafuta kama ekari 20 karibu chanzo cha maji na ulikatie hati haiwezi zidi 10m.

kila ekari utapanda miche 800 kwa hiyo utakuwa na miche 16,000 ambayo itazaa mikungu 16,000 baada ya miezi 12. bei ya mkungu ni 5000 mpaka 20,000. kwa ekari ishirini utapata 80m kwa bei ya 5000. unalipa deni na zingine unaenda kulewa na vidosho.

faida ni kwamba utakuwa na ardhi (hard asset), competition ni ndogo tofauti na matikiti pia utapata collateral, bei ya chakula inakuwa kila siku.

changamotoo ni kuwa kuna magonjwa ya ndizi, kupanda na kumanage miche 16,000 sio lelemama, ikihitajika umwagilie halitakuwa jambo rahisi.
 
KasomaJr, umesahau kusema riba ya mkopo ni kiasi gani.
 
Last edited by a moderator:
Habari wana JF,
Nakuja mbele zenu kuomba ushauri kwenu, ushauri wenu uzingatie mambo yafuatayo.

CAPITAL/LOAN:
Nimeamua kuchukua Loan ya 30M bank flani na nyumba yangu nimeamua kuweka rehani kabisaaa kwa kujua kabisa kama sitaweza kulipa nyumba yangu itachukuliwa, nimefanya hivyo kwa kuzingatia return nayoipata kwenye yumba hiyo ni kidogo sana, 150,000/= per month, a 3 bedroom, one ni master, ina kitchen na sitting room, ipo eneo ambalo ni potential sana na ina kiwanja kikubwa kwa maana ya kwamba hiyo ni nyumba ya uani, mbele kuna kiwanja kikubwa cha kuweza kujenga hata ghorofa/hotel yenye uwezo wa kuwa na rooms 15-20.

INTEREST/DREAM/CALLING
Ukweli wa moyo wangu naamini kabisa katika kilimo ingawa nimewahi kufanya attempt moja amabyo haikufanikiwa katika kilimo ya matikiti maji huko Manyara, lakini najua kabisa tatizo ilikuwa usimamizi mzuri (kwani vijana niliowaweka hawakuwa serious na kazi na mimi nilikuwa kwenye michakato ya kwenda nje kikazi, hivyo muda mwingi nikautumia kufuatilia visa na nk). Hivyo katika suala hili nataka kujua ni kilimo gani kinaweza kunipa return haraka na ni risk free ili kuweza kuanza kulipa loan.

Hivyo basi naomba ushauri kwa kuzingatia haya yafuatayo pia;
1. Kuanzisha green house nyumbani kwangu kwakua bado nina eneo la kuweza ku-accomodate
2. Kununua shamba maeneo ya Mwasonga kiasi cha ekari 2 kwa ajili ya shughuri za ufugaji kuku wa kienyeji, samaki hata bwawa moja, greenhouse na kilimo cha matikiti maji
Hapa nitaomba uzoefu wa gharama kama za kuchimba kisima, fensing ya wire na vitu vingine muhimu.

BIASHARA YA STATINARIES/INTERNET CAFE
Nimewaza kufanya biasha hii na nimeifanyia utafiti kwa kiasi flani, nilitaka kuweka internet cafe maeneo ya Ferry kigamboni lakini ambayo ingekuwa modern kidogo, na capita investment ilikwenda karibu 12M lakini nikifanya analysisi ya return naona kama ni ndogo sana ukilinganisha na capital investment. Hivyo naomba ushauri kwenye eneo hili kwa mutu amabe anao uzoefu wa kutoksha. Kwenye eneo hili business mix yangu ilikuwa ni pamoja na
1. Printing
2. Photocopying
3. M-PESA/Tigo Pesa/ Airtel Money
4. Air ticketing
5. Kuatafuta kazi za nje za printing/ supply ya stationaries
6. Internet cafe ambayo itakuwa na wireless lakini ikiwa controlled na mambo ya downloads na time
Si kuwa na mpango wa kuweka stationaries nyingi hata kidogo

BIASHARA YA USAFIRISHAJI/ NA MAZAO
Nimepewa ushauri kwamba biashara ya chakula inalipa sana, yaani kuuza unga, maharage, sukari, mafuta nk...na hii wife yeye anai support ingawa moyo wangu haunipi hata kidogo, na katika hili tulipaswa tununue hata carry au Noah kwa ajili ya kusambaza mizigo kwa wateja lakini wakati huo huo gari itumike kibishara kwa maana kwamba kama ni Carry basi itaweza kufanya shughuli za kubeba mizigo ya wateja nje ya biashara yetu, na kama ni Noah basi iwe mult-pupose kwa maana ya kwamba itatumika kwa biashara yetu na familia pia.

Jamani am confused, nahitaji msaada wenu kwa kujua na kuzingatia JF ni kisima cha maarifa, kimejaa watu makini, weledi na wenye uzoefu mkubwa kabisa katika maisha haya.
Asanteni na mungu awabariki sana.

SRS DILI ILA YAITAJI.MOYO WA UKAKAMAVU

NUNUA BANGI NVUTTO YA MOROGORO TAFUTA WACOMORRO WAPO KARIAKOO

WAKUPE.MTU.WAAKUKUPOKELEA BANDARINI

HAPA UNAPITA.SHURBA.UKO NA UKIFANIKIWA NI.MARA.TANO UNAACHA UNAMUaIiKA.DIAMOND.NA.YAMOTO WANAPIGA.NYIMBO NJE KWAKO WIKI Nzima

AMA NENDA COMORO FANYA MARKET RESEARCH YA NYAMA YA MBUZI NA NGOMBE NA VITUNGUU UTANIPENDA UKIPELEKA

MTAJI MIL 3 TU
 
Else njo kanisani kwetu tuziombee kwanza alafu fanya buss.na yesu utaipenda unatoa.million 3 unapata dili.ya mill.10

mungu afichi
 
Pesa kama hii akiipata mtu mtundu mtundu kwa siku lazima 300'000 ilale ...
CYBERTEQue
 
Last edited by a moderator:
SRS DILI ILA YAITAJI.MOYO WA UKAKAMAVU

NUNUA BANGI NVUTTO YA MOROGORO TAFUTA WACOMORRO WAPO KARIAKOOh

WAKUPE.MTU.WAAKUKUPOKELEA BANDARINI

HAPA UNAPITA.SHURBA.UKO NA UKIFANIKIWA NI.MARA.TANO UNAACHA UNAMUaIiKA.DIAMOND.NA.YAMOTO WANAPIGA.NYIMBO NJE KWAKO WIKI Nzima

AMA NENDA COMORO FANYA MARKET RESEARCH YA NYAMA YA MBUZI NA NGOMBE NA VITUNGUU UTANIPENDA UKIPELEKA

MTAJI MIL 3 TU

Shikamoo Pdidy
 
Last edited by a moderator:
Ebu jaribu kilimo cha vitunguu maji nasikia navyo vinalipa sana japo mimi sina uzoefu navyo.Lakini naamini wataalamu wapo humu watakupa maelezo zaidi.
 
Else njo kanisani kwetu tuziombee kwanza alafu fanya buss.na yesu utaipenda unatoa.million 3 unapata dili.ya mill.10

mungu afichi

Mpwa ukila vitu unakuwa na busara sana
 
KasomaJr, umesahau kusema riba ya mkopo ni kiasi gani.

Riba ni 19% Kwa mwaka Kwa declining method. Hii ina maana kwamba kila unapokatwa Kwa mwezi, kile kiasi kilicho baki ndicho kinapigiwa asilimia 19%, hivyo hivyo mpaka mkopo utakapo isha.
 
Last edited by a moderator:
Ebu jaribu kilimo cha vitunguu maji nasikia navyo vinalipa sana japo mimi sina uzoefu navyo.Lakini naamini wataalamu wapo humu watakupa maelezo zaidi.

Ni kweli hilo ni wazo zuri sana, nimekuwa kwenye mawasiliano na mjasiliamali mmoja mmarufu sana anaitwa Meshack Maganga, yeye anafanyia kilimo chake huko Iringa, tumefanya analysis yote vizuri kabisa, changamoto ni moja tu, kule unahitaji kukodi mashamba na pia usimamizi wake unapaswa kuwa wa hali ya juu na ambao kimsingi unakuhitaji mhusika Kwa 100% ya muda wako, Sasa nina pata hofu katika mazingira haya ya Mwanzo ku risk kiasi kikubwa hivyo hasa nikikumbuka uzoefu kwenye matikiti Maji niliyolima 2 acre huko Manyara na kuondoka mikono mitupu. Lakini ni kilimo ambacho kinalipa kabisa, u invest 5m return ni 4m+ Kwa acre moja na Kwa muda mfupi tu wa less than 4 month.
 
Umechukua mkopo kabla ya kujua unafanya biashara gani?

Si kweli kwamba sijui nini nataka kufanya exactly lakini hapa ni suala la uhakika wa kile nataka kufanya, kujua changamoto na matarajio yanaweza kuwaje ukilinganisha uzoefu wa watu wengine katika shughuli hiyo. Hivyo kifupi ni kutafuta knowledge zaidi kuweza kujua namna bora naweza kufanya katika machaguo yangu hayo. Na Kwa lugha nyingine ni kwamba hizo biashara nimeainisha ni kwamba zote lazima zitakuja kufanyika ila ipi ianze na namna gani itategemeana na taarifa ambazo nimeendelea kuzikusanya. Ingawa kilimo na ufugaji bado naamini ni priority kwangu.
 
mi nakushauri ulime ndizi za kupika (plantains) maeneo ya moro. tafuta kama ekari 20 karibu chanzo cha maji na ulikatie hati haiwezi zidi 10m.

kila ekari utapanda miche 800 kwa hiyo utakuwa na miche 16,000 ambayo itazaa mikungu 16,000 baada ya miezi 12. bei ya mkungu ni 5000 mpaka 20,000. kwa ekari ishirini utapata 80m kwa bei ya 5000. unalipa deni na zingine unaenda kulewa na vidosho.

faida ni kwamba utakuwa na ardhi (hard asset), competition ni ndogo tofauti na matikiti pia utapata collateral, bei ya chakula inakuwa kila siku.

changamotoo ni kuwa kuna magonjwa ya ndizi, kupanda na kumanage miche 16,000 sio lelemama, ikihitajika umwagilie halitakuwa jambo rahisi.

Asante Kwa ushauri wenye tija sana, hii ni idea mpya kabisa na nzuri.... Bila shaka hii ni risk free business, si
Mimi tu lakini wadau wengine wanapaswa kuchukua hii idea na ninadhani Si lazima iwe huko Morogoro, hata Dar kama tukawasiliana na wataalamu wa kilimo juu ya udongo na tukawa na uhakika wa Maji bila shaka ndizi zinaweza kulimwa Kwa baadhi ya maeneo.
 
SRS DILI ILA YAITAJI.MOYO WA UKAKAMAVU

NUNUA BANGI NVUTTO YA MOROGORO TAFUTA WACOMORRO WAPO KARIAKOO

WAKUPE.MTU.WAAKUKUPOKELEA BANDARINI

HAPA UNAPITA.SHURBA.UKO NA UKIFANIKIWA NI.MARA.TANO UNAACHA UNAMUaIiKA.DIAMOND.NA.YAMOTO WANAPIGA.NYIMBO NJE KWAKO WIKI Nzima

AMA NENDA COMORO FANYA MARKET RESEARCH YA NYAMA YA MBUZI NA NGOMBE NA VITUNGUU UTANIPENDA UKIPELEKA

MTAJI MIL 3 TU

Pdidy: Umeanza Kwa style ambayo siyo safi sana mkuu, biashara ya mihadarati hapana hiyo Si ungi mkono Kwa namna yoyote ile, ila hapa kwenye issue ya biashara ya nyama ya Mbuzi na vitunguu tunaweza kuongea na Kwa hakika naomba niku PM kuweza ku exchange idea na kuwa na live conversation juu ya hilo ni muhimu sana na ninaomba unipe ushirikiano. Asante sana.
 
Back
Top Bottom