Msaada wa ushauri biashara gani hasa nifanye kwa 30m capital

Msaada wa ushauri biashara gani hasa nifanye kwa 30m capital

Namlaumu sana huyo aliyekupa mkopo, alitakiwa akubane sana useme unaenda kufanya biashara gani mapema kabla hajakupa.
 
Hiyo nyumba yako iko sehemu gani mpaka upate return ndogo hivyo?? Nyumba nzima unapata 150,000/- p.m???

Ushauri wangu.
Kama nyumba yako na kiwanja chako kiko sehem potential, try to invest in that land. With 30m, unaweza kujenga vyumba vya kupanga au fremu kama nne au tano, kwa kutumia materials nzuri but cheap..
Fremu moja ikikodisha kwa 100,000/- x5 frames = 500,000/- per month. X 12 months = 6m per year

Kwa rooms za kupanga, unajenga chumba na sebule, self contained, with kitchen,.. 4 of them . ukikodisha each @200,000/- x 4= 800,000/- per month x 12 = 9,600,000/- per year.

If interested, check me for the plans and advice on the best materials for that job.
 
Au kwa kuwa unayo ardhi tayari, invest in poultry. Jenga mabanda ya kuku ya kisasa na makubwa...fuga kuku wa nyama na mayai..na ma bata mzinga
With in four months, you will be richer than rich.
 
Lakini ni kilimo ambacho kinalipa kabisa, u invest 5m return ni 4m+ Kwa acre moja na Kwa muda mfupi tu wa less than 4 month.

Mkuu naomba ufafanue zaidi. Sijaelewa kwamba una invest 5m per acre kwa tikiti maji?
 
Mkuu naomba ufafanue zaidi. Sijaelewa kwamba una invest 5m per acre kwa tikiti maji?
Sorry mkuu nadhani nilichanganya but i meant investment ya 5m kwenye vitunguu na unaweza kupata return ya 4M.
 
Hiyo nyumba yako iko sehemu gani mpaka upate return ndogo hivyo?? Nyumba nzima unapata 150,000/- p.m???

Ushauri wangu.
Kama nyumba yako na kiwanja chako kiko sehem potential, try to invest in that land. With 30m, unaweza kujenga vyumba vya kupanga au fremu kama nne au tano, kwa kutumia materials nzuri but cheap..
Fremu moja ikikodisha kwa 100,000/- x5 frames = 500,000/- per month. X 12 months = 6m per year

Kwa rooms za kupanga, unajenga chumba na sebule, self contained, with kitchen,.. 4 of them . ukikodisha each @200,000/- x 4= 800,000/- per month x 12 = 9,600,000/- per year.

If interested, check me for the plans and advice on the best materials for that job.
serio...nashukuru sana kwa ushauri wako, ukweli eneo hilo ni potential sana na si kwamba nafanya jokes, na ukweli lipo kwenye long term plans zangu kwani i have inside info kanisa flani ambalo ni wamiliki wa eneo opposite na eneo langu wana mpango wa kujenga chuo in 5 years time, kuhusu bei ya rent kuwa ndogo ni kweli na hii ni kwa sababu ya circulation ya pesa sasa hivi kwa Mkoa wa Kigoma ni kidogo sana, wafanyakazi amabo most ndiyo wapangaji wazuri hakuna, mashirika mengi yamemaliza operation zao kitambo, waliowengi mnajua makambi ya wakimbizi yamefungwa kitambo sasa.
Lakini i still stand the best chance kufanya hayo huku Dar es Salaam ambako ndiko nime-reallocate kwa sasa. kwani eneo ninalo ishi bado kuna eneo lipo wazi kuweza kujenga mabanda ya kuku ya kutosha, challenge ambayo na face kwa sasa ni kuwa nahitaji kisima cha maji, nahitaji kujenga fence kuzunguka eneo lote na vyote jumla lazima viende zaidi ya 7M. Kwenye changamoto ya maamuzi, kwani naona bora nichukue eneo la ekari 2 ambalo kisimsingi linasubiri tu malipo na kuanza opeartion, ila capital investment ni kubwa sana, ingawa in long run naona kabisa there is green/bright future ahead. hasa kwenye ufugaji wa kuku, kilimo cha matunda (mapapai, machungwa na maembe mafupi), kilimo cha nyanya, hoho, matango nk.
Nitaku-PM kwa taarifa zaidi juu ya ujenzi rahisi hata kwa mabanda ya kuku na servant quarter. Asante kiongozi
 
Mkuu ntakupa ushauri wa aina 2
1. Tafuta frem kubwa sehemu mtafute pharmacist aje akufanyie assessment ongea nae vizuri mpe kiasi cha pesa lets say 1 million tumia cheti chake kwenda TFDA na yy akikusaidia upate kibali cha kufungua pharmacy kwa gharama ya 20 millions zen 10 millions weka backup capital. Eneo hilo liwe ni sehemu ilichangamka sana tafuta wafanyakazi ambao watafanya kazi shift ya day and night. Pasifungwe all year long unaweza ingiza zaidi ya 200,000 per day.
N.B uwe karibu sana kwa uangalizi na pia uelewe madawa hii itakusaidia kutokuibiwa sana
2. Tafuta sehemu ilichangamka kodisha jenga car wash. Weka shimo kwa ajiri ya services za hapa na pale pump kama kawaida na tank za maji. Ama chimba kisima. Aisee utapiga ela jamaa angu ww fanya matangazo tu kwenye radio uchwara hapa mjini ,weka na oil lubricants, na vifaa vya hapa na pale yani mtu akitaka kufanya simple car services na mafundi wako wawili watatu. Oooh btw usisahau na fridges za vinywaji baridi na snaks kwa wateja wanaosubiri magari yao yakifanyiwa usafi.

Kila la kheri amigo!
 
Asante sana kiongozi, bonge la ushauri wa maana Mzee Franky,
Nimeku check inbox mtu mzima. Thanks a million times Kwa bonge la advise.
 
Habari wana JF,
Nakuja mbele zenu kuomba ushauri kwenu, ushauri wenu uzingatie mambo yafuatayo.

CAPITAL/LOAN:
Nimeamua kuchukua Loan ya 30M bank flani na nyumba yangu nimeamua kuweka rehani kabisaaa kwa kujua kabisa kama sitaweza kulipa nyumba yangu itachukuliwa, nimefanya hivyo kwa kuzingatia return nayoipata kwenye yumba hiyo ni kidogo sana, 150,000/= per month, a 3 bedroom, one ni master, ina kitchen na sitting room, ipo eneo ambalo ni potential sana na ina kiwanja kikubwa kwa maana ya kwamba hiyo ni nyumba ya uani, mbele kuna kiwanja kikubwa cha kuweza kujenga hata ghorofa/hotel yenye uwezo wa kuwa na rooms 15-20.

INTEREST/DREAM/CALLING
Ukweli wa moyo wangu naamini kabisa katika kilimo ingawa nimewahi kufanya attempt moja amabyo haikufanikiwa katika kilimo ya matikiti maji huko Manyara, lakini najua kabisa tatizo ilikuwa usimamizi mzuri (kwani vijana niliowaweka hawakuwa serious na kazi na mimi nilikuwa kwenye michakato ya kwenda nje kikazi, hivyo muda mwingi nikautumia kufuatilia visa na nk). Hivyo katika suala hili nataka kujua ni kilimo gani kinaweza kunipa return haraka na ni risk free ili kuweza kuanza kulipa loan.

Hivyo basi naomba ushauri kwa kuzingatia haya yafuatayo pia;
1. Kuanzisha green house nyumbani kwangu kwakua bado nina eneo la kuweza ku-accomodate
2. Kununua shamba maeneo ya Mwasonga kiasi cha ekari 2 kwa ajili ya shughuri za ufugaji kuku wa kienyeji, samaki hata bwawa moja, greenhouse na kilimo cha matikiti maji
Hapa nitaomba uzoefu wa gharama kama za kuchimba kisima, fensing ya wire na vitu vingine muhimu.

BIASHARA YA STATINARIES/INTERNET CAFE
Nimewaza kufanya biasha hii na nimeifanyia utafiti kwa kiasi flani, nilitaka kuweka internet cafe maeneo ya Ferry kigamboni lakini ambayo ingekuwa modern kidogo, na capita investment ilikwenda karibu 12M lakini nikifanya analysisi ya return naona kama ni ndogo sana ukilinganisha na capital investment. Hivyo naomba ushauri kwenye eneo hili kwa mutu amabe anao uzoefu wa kutoksha. Kwenye eneo hili business mix yangu ilikuwa ni pamoja na
1. Printing
2. Photocopying
3. M-PESA/Tigo Pesa/ Airtel Money
4. Air ticketing
5. Kuatafuta kazi za nje za printing/ supply ya stationaries
6. Internet cafe ambayo itakuwa na wireless lakini ikiwa controlled na mambo ya downloads na time
Si kuwa na mpango wa kuweka stationaries nyingi hata kidogo

BIASHARA YA USAFIRISHAJI/ NA MAZAO
Nimepewa ushauri kwamba biashara ya chakula inalipa sana, yaani kuuza unga, maharage, sukari, mafuta nk...na hii wife yeye anai support ingawa moyo wangu haunipi hata kidogo, na katika hili tulipaswa tununue hata carry au Noah kwa ajili ya kusambaza mizigo kwa wateja lakini wakati huo huo gari itumike kibishara kwa maana kwamba kama ni Carry basi itaweza kufanya shughuli za kubeba mizigo ya wateja nje ya biashara yetu, na kama ni Noah basi iwe mult-pupose kwa maana ya kwamba itatumika kwa biashara yetu na familia pia.

Jamani am confused, nahitaji msaada wenu kwa kujua na kuzingatia JF ni kisima cha maarifa, kimejaa watu makini, weledi na wenye uzoefu mkubwa kabisa katika maisha haya.
Asanteni na mungu awabariki sana.

habar sitopenda kuongea saana but napenda kukushauri uwekeze upande wa afya mean matibabu yaaani u cant believ it . tena locate sehemu ya nje kidogo mbayo utahisi sekta hiio inaahitajikaa.
if u r intrest with this text me private i will gve u maujanjaa.....
 
Asante sana kiongozi, bonge la ushauri wa maana Mzee Franky,
Nimeku check inbox mtu mzima. Thanks a million times Kwa bonge la advise.

hapo pharmacyy mi nakupa % 100 za kufanikisha dont hasitate broo. nilikua nakujia huko but nimeshindwa how tu staat.
 
mkuu kumbe uko hapo Kigoma.. mi nakushauri wekeza kwenye tumbaku, kigoma pia kuna makampuni makubwa tu yanayonunua tumbaku.. tafuta wataalam wa kilimo uwaombe ushauri wakupe details za zao husika then ujipange. na kipindi hiki nadhani ndo wanaandaa mashamba..
 
Fanya biashara ya mbao kutoka njombe kuleta dar
 
Fanya biashara ya mbao kutoka njombe kuleta dar

hii biashara ni nzuri sababu mahitaji ni mengi.. watu wanajenge, furniture pia zinahitaji mbao... ila hii biashara ili upate faida nzuri inabidi ufanye magendo mkuu.. vile vibali vinakua na idadi ya kiasi cha mbao unazotakiwa kuvuna na ukishamaliza unatakiwa kukata kibali upya na kuna maovyo ovyo mengi sanaa.. ukikamatwa umezidisha mzigo utaisoma namba mkuu.. wanachukua mzigo wote. labda utafute mtu mwenye leseni ufanye nae biashara..
 
Huku kitaani kwetu nafanya biashara ya riba 10 kwa 15
 
kaka nipo mbezi beach nina best killing buznes innovation nipigie 0713774746
 
Back
Top Bottom