Msaada wa ushauri biashara gani hasa nifanye kwa 30m capital

Namlaumu sana huyo aliyekupa mkopo, alitakiwa akubane sana useme unaenda kufanya biashara gani mapema kabla hajakupa.
 
Hiyo nyumba yako iko sehemu gani mpaka upate return ndogo hivyo?? Nyumba nzima unapata 150,000/- p.m???

Ushauri wangu.
Kama nyumba yako na kiwanja chako kiko sehem potential, try to invest in that land. With 30m, unaweza kujenga vyumba vya kupanga au fremu kama nne au tano, kwa kutumia materials nzuri but cheap..
Fremu moja ikikodisha kwa 100,000/- x5 frames = 500,000/- per month. X 12 months = 6m per year

Kwa rooms za kupanga, unajenga chumba na sebule, self contained, with kitchen,.. 4 of them . ukikodisha each @200,000/- x 4= 800,000/- per month x 12 = 9,600,000/- per year.

If interested, check me for the plans and advice on the best materials for that job.
 
Au kwa kuwa unayo ardhi tayari, invest in poultry. Jenga mabanda ya kuku ya kisasa na makubwa...fuga kuku wa nyama na mayai..na ma bata mzinga
With in four months, you will be richer than rich.
 
Lakini ni kilimo ambacho kinalipa kabisa, u invest 5m return ni 4m+ Kwa acre moja na Kwa muda mfupi tu wa less than 4 month.

Mkuu naomba ufafanue zaidi. Sijaelewa kwamba una invest 5m per acre kwa tikiti maji?
 
Mkuu naomba ufafanue zaidi. Sijaelewa kwamba una invest 5m per acre kwa tikiti maji?
Sorry mkuu nadhani nilichanganya but i meant investment ya 5m kwenye vitunguu na unaweza kupata return ya 4M.
 
serio...nashukuru sana kwa ushauri wako, ukweli eneo hilo ni potential sana na si kwamba nafanya jokes, na ukweli lipo kwenye long term plans zangu kwani i have inside info kanisa flani ambalo ni wamiliki wa eneo opposite na eneo langu wana mpango wa kujenga chuo in 5 years time, kuhusu bei ya rent kuwa ndogo ni kweli na hii ni kwa sababu ya circulation ya pesa sasa hivi kwa Mkoa wa Kigoma ni kidogo sana, wafanyakazi amabo most ndiyo wapangaji wazuri hakuna, mashirika mengi yamemaliza operation zao kitambo, waliowengi mnajua makambi ya wakimbizi yamefungwa kitambo sasa.
Lakini i still stand the best chance kufanya hayo huku Dar es Salaam ambako ndiko nime-reallocate kwa sasa. kwani eneo ninalo ishi bado kuna eneo lipo wazi kuweza kujenga mabanda ya kuku ya kutosha, challenge ambayo na face kwa sasa ni kuwa nahitaji kisima cha maji, nahitaji kujenga fence kuzunguka eneo lote na vyote jumla lazima viende zaidi ya 7M. Kwenye changamoto ya maamuzi, kwani naona bora nichukue eneo la ekari 2 ambalo kisimsingi linasubiri tu malipo na kuanza opeartion, ila capital investment ni kubwa sana, ingawa in long run naona kabisa there is green/bright future ahead. hasa kwenye ufugaji wa kuku, kilimo cha matunda (mapapai, machungwa na maembe mafupi), kilimo cha nyanya, hoho, matango nk.
Nitaku-PM kwa taarifa zaidi juu ya ujenzi rahisi hata kwa mabanda ya kuku na servant quarter. Asante kiongozi
 
Mkuu ntakupa ushauri wa aina 2
1. Tafuta frem kubwa sehemu mtafute pharmacist aje akufanyie assessment ongea nae vizuri mpe kiasi cha pesa lets say 1 million tumia cheti chake kwenda TFDA na yy akikusaidia upate kibali cha kufungua pharmacy kwa gharama ya 20 millions zen 10 millions weka backup capital. Eneo hilo liwe ni sehemu ilichangamka sana tafuta wafanyakazi ambao watafanya kazi shift ya day and night. Pasifungwe all year long unaweza ingiza zaidi ya 200,000 per day.
N.B uwe karibu sana kwa uangalizi na pia uelewe madawa hii itakusaidia kutokuibiwa sana
2. Tafuta sehemu ilichangamka kodisha jenga car wash. Weka shimo kwa ajiri ya services za hapa na pale pump kama kawaida na tank za maji. Ama chimba kisima. Aisee utapiga ela jamaa angu ww fanya matangazo tu kwenye radio uchwara hapa mjini ,weka na oil lubricants, na vifaa vya hapa na pale yani mtu akitaka kufanya simple car services na mafundi wako wawili watatu. Oooh btw usisahau na fridges za vinywaji baridi na snaks kwa wateja wanaosubiri magari yao yakifanyiwa usafi.

Kila la kheri amigo!
 

Asante sana kiongozi, bonge la ushauri wa maana Mzee Franky,
Nimeku check inbox mtu mzima. Thanks a million times Kwa bonge la advise.
 


habar sitopenda kuongea saana but napenda kukushauri uwekeze upande wa afya mean matibabu yaaani u cant believ it . tena locate sehemu ya nje kidogo mbayo utahisi sekta hiio inaahitajikaa.
if u r intrest with this text me private i will gve u maujanjaa.....
 
Asante sana kiongozi, bonge la ushauri wa maana Mzee Franky,
Nimeku check inbox mtu mzima. Thanks a million times Kwa bonge la advise.

hapo pharmacyy mi nakupa % 100 za kufanikisha dont hasitate broo. nilikua nakujia huko but nimeshindwa how tu staat.
 
Bro mi nakushauri njoo kwenye mbao tu Hutaamini kabsa....ni pm ntakudirect kla ktu
 
mkuu kumbe uko hapo Kigoma.. mi nakushauri wekeza kwenye tumbaku, kigoma pia kuna makampuni makubwa tu yanayonunua tumbaku.. tafuta wataalam wa kilimo uwaombe ushauri wakupe details za zao husika then ujipange. na kipindi hiki nadhani ndo wanaandaa mashamba..
 
Fanya biashara ya mbao kutoka njombe kuleta dar
 
Fanya biashara ya mbao kutoka njombe kuleta dar

hii biashara ni nzuri sababu mahitaji ni mengi.. watu wanajenge, furniture pia zinahitaji mbao... ila hii biashara ili upate faida nzuri inabidi ufanye magendo mkuu.. vile vibali vinakua na idadi ya kiasi cha mbao unazotakiwa kuvuna na ukishamaliza unatakiwa kukata kibali upya na kuna maovyo ovyo mengi sanaa.. ukikamatwa umezidisha mzigo utaisoma namba mkuu.. wanachukua mzigo wote. labda utafute mtu mwenye leseni ufanye nae biashara..
 
Huku kitaani kwetu nafanya biashara ya riba 10 kwa 15
 
kaka nipo mbezi beach nina best killing buznes innovation nipigie 0713774746
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…