Msaada wa ushauri kwa mjane unahitajika

Msaada wa ushauri kwa mjane unahitajika

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
14,804
Reaction score
10,715
Wakuu, nimetakiwa kumsimamia mama mjane juu ya haki zake. Mama huyu aliolewa mwaka 1997 huko Mpanda na mume aliyekuwa na watoto wanne wakubwa. Baada ya mwaka mmoja mume aliyekuwa mfanyakazi alipewa redundance.

Wakaamua kuhamia DSM. Alitangulia mwanamume akatafuta nyumba ya kupanga. Wakati huo walikuwa na mtoto mdogo ambaye alifariki baadaye. Mume alimfuata mke wakaja kuishi DSM ambapo walizaa mtoto mmoja aliye sekondari hata sasa.

Mume alipata kazi ya korokoroni aliyokuwa akiendelea nayo hadi mauti ilipomkuta.

Wakiwa DSM walifanikiwa kujenga nyumba huko mbagala ambapo walikuwa wakiishi hadi mauti yalipomfika mume. Kazi ya mwanamke ni mganga wa tiba za asili.

Shida ni kuwa watoto wale wa mama wa kwanza pamoja na shehe (mume alikuwa mwislamu) wanadai kuwa nyumba waliyoijenga ni mali ya watoto pamoja na vitu vingine vyote. Huyu mama wanasema akabidhiwe kwa ndugu zake wao wauze nyumba watoto wagawane pesa. Wanasema huyu mama akaolewe tena huko kwao ilhali kajijengea nyumba na mumewe ili waishi hati mpaka mauti yawafike.

1. Je, sheria ya kiislamu inasemaje juu ya hili? Huyu mama aliyetumia muda na nguvu zake kujijenga na mumewe ni sahihi afukuzwe hapo?

2. Sheria za nchi zikoje katika hili? Mwanamke keshanyang'wa hati za nyumba na watoto, ingawa anao ushahidi tosha kuwa hiyo nyumba kaijenga na mumewe.

3. Leo ndio kuna kikao cha ukoo cha maamuzi, nahitaji msaada wa haraka katika hili.

Belo Daudi Mchambuzi zumbemkuu
[MENTION] Yericko Nyerere[/MENTION] Bujibuji Makoye Matale, Kaa la Moto, Sikonge Eiyer FaizaFoxy

MREJESHO

Wakuu nashukuru sana kwa msaada wenu wa ushauri. Baaada ya jana kufika kwa mjane yafuatayo yalifanyika:

>> Alikuja shehe kusimamia hili zoezi la kugawa mali. Shehe huyu alitumia hekima ya hali ya juu kunusuru mambo.

>> Samani zote za ndani aliachiwa marehemu kwa ushauri wa shehe baada ya baadhi ya ndugu katika kuchukua kila kitu.

>> Mpango wa kuuza nyumba aliukataa shehe akidai maadam mama yupo na mwanae wataendelea kuishi hapo. Kisha akaelekeza kuwa suala la nyumba ni la kisheria, hivyo utayarishwe muhutasari utakaoteua msimamizi wa mirathi kisha upelekwe mahakamani. Taratibu nyingine zitafuata huko.

>> Alisisitiza kuwa anafanya hivyo kwa vile hataki kuanza kuitwa kwenye kesi za unyang'anyi wa mali za mjane. Pia alimuuma sikio mjane kuwa msimamizi wa mirathi ni mjane mwenyewe labda kama ataamua vinginevyo.

>> Wakati haya yakifanyika alifanya mgawanyo wa vyumba kwa watoto wote wa marehemu. Nyumba kubwa ina vyumba vitatu na sebule. Chumba kimoja cha mjane, viwili vya mtoto wa mjane. Nje kuna nyumba ya vyumba vitatu vinavyojitegemea (behewa). Watoto watatu wa marehemu kila mmoja akapewa chumba kimoja wakati shauri la mirathi likisubiriwa.

>> Mjane aliridhia maamuzi haya na hivyo taratibu za matatizo zinasubiriwa. Lengo la shehe ni kuleta mshikamano kati ya mama na watoto. Maamuzi haya yamezua chuki kubwa kwa baadhi ya watoto wa marehemu.

>> Huu mwelekeo mnauonaje wakuu?

Katika tukio jingine mtoto wa mjane (bado ni mwanafunzi) yuko mahututi. Aliugua kichaa ghafla siku ya pili ya msiba. Baada ya dada yake (wa mama mwingine) kufika alimchukua pembeni na kumwambia aache kujidai analia kwa uchungu sana, kisha akampitishia viganja vya mikono yake usoni mithili ya kumfuta machozi. Tangu dakika hiyo binti huyu wa mjane alianza kuchekacheka hovyo na kuongea maneno ya ajabu ajabu. Sijamuona huyu binti kwani wamempeleka kwa sangoma. Nimepanga kwenda kumjulia hali nakuangalia namna nyingine ya kumsaidia

Cc. Nguto, Buntungwa, GEBA2013, Power to the People, Majigo, rodrick alexander, Doppelganger, Makoye Matale, Yericko Nyerere, Daudi Mchambuzi, Sikonge, Eiyer, FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
Nyumba ni ya mke na watoto wa ndoa. Hao wengine aliwazaa kwenye ndoa ya kwanza au? Sijui sheria za kiiaslamu zinasema nini hapo.
 
Haya mambo bana .....

Nyumba ni ya walioijenga,hilo ni jambo la msingi kabisa,suala la nani wa kupewa ni la walioijenga kwani huwezi kumlazimisha mtu nani ampe mali yake

Kuhusu sheria za nchi nadhani zinawatambua wazazi na watoto pia

Kuhusu sheria za Kiislam ngoja waje wahusika watakuambia!
 
Nyumba ni ya mke na watoto wa ndoa. Hao wengine aliwazaa kwenye ndoa ya kwanza au? Sijui sheria za kiiaslamu zinasema nini hapo.

Nalifaham hili sakata. Wanawake tunanyanyasika sana jamani.
Ni hivi, alikuwa na mke mwingine ambaye walitalikiana ndipo akamwoa huyu aliye naye. Huyu mke wa kwanza ndiye mwenye watoto watatu.

Ile nyumba kaijenga huyu mama na mumewe. Sasa akifukuzwa ili watoto ambao ni watu wazima) waimiliki nyumba yeye ataishi wapi? Au haki ya mwanamke ni pale tu mume awapo hai?
 
Nyumba n ya mzazi mpaka hapo atakopo amua ampe mtoto yupi au wagawane.watoto hawana mamlaka endapo mzaz mmoja yupo hai.
 
Tukiambiwa tuandike wosia tunasema tunajichuria kifo. Hata kama mtu una viatu tu anfika nani apewe kuepusha shida kama hizi hasa kama kuna familia mbili.
 
Tukiambiwa tuandike wosia tunasema tunajichuria kifo. Hata kama mtu una viatu tu anfika nani apewe kuepusha shida kama hizi hasa kama kuna familia mbili.

Kifo kipo palepale, inabidi wazazi wabadirika kwa hili
 
A. Kama jina kwenye hati miliki ya nyumba ni la Marehemu pekee basi nyumba ilikuwa yake.

B. Kama watoto wa awali walikuwa wa ndoa na Waislam basi na wao wana-haki ya urithi.

C. Kama huyu "mkewe" wa sasa ni wa ndoa na ni Muislam basi ana haki ya urithi.

D. Kama "C" ni ndiyo, basi na mtoto ana haki ya urithi.

E. Yule mtoto aliyefariki ndiyo kishafariki na hayumo kabisa katika hili unless alikuwa na mali zake binafsi kabla hajafariki na zilikuwa zikitazamwa na huyu marehemu.

Hapo sasa linakuwa suala la hesabu za urithi tu kwa Kiislam.

Kinyume cha chochote kati ya hivyo, hapo inabidi tujuwe kama walikuwa wa ndoa au nje ya ndoa, Waislam au si Waislam ili tutoe msimamo wa Kiislam.

Hapo ndipo mtakapoona umuhimu wa Mahakama ya Kadhi. Kesi kama hii ikipelekwa mahakama hizi za kawaida itachukuwa miaka hata kumi au zaidi kumalizwa (kama itamalizwa) na itakuwa inakula fedha za walipa kodi bila hesabu.

Kwa maana hata hizo mahakama za kawaida zitahukumu mirathi Kiislam mpaka tu atapotokea mtu kusema kuwa huyo marehemu aliukana Uislam.
 
Pole sana Mkuu Nyenyere, pole pia kwa huyo mama.

Uhalali wa kumiliki mali upo kwa mwenye kuitafuta hiyo mali hapa namaanisha ni Mume na Mke waliojenga hiyo nyumba kwa pamoja, watoto si halali yao kumiliki hiyo nyumba isipokuwa kwa ridhaa ya wenye nyumba yaani baba na mama yao. Kwa vile baba kaaga dunia aliyebaki (mama) ndiye mmiliki halali, akipenda anaweza kuwamilikisha watoto au hata mtu yeyote akiona inafaa kufanya hivyo. Wale watoto wa mama mwingine wanaweza kupata sehemu ya mali ya baba yao kwa makubaliano na huyu mama (siyo kumnyang'anya hati ya nyumba).

Nini kifanyike:

1. Huyu mama asimame kidete adai kurudishiwa hati ya nyumba katika kikao hicho cha kifamilia, endapo hati haitarejeshwa basi aende mahakamani moja kwa moja kudai hati hiyo.

2. Marehemu hakuwa na nyumba pekee (I presume), akubali kugawa sehemu ya mali kwa watoto hao wa marehemu kwa ajili ya kujenga mahusiano mema ingawa halazimiki kuwagawia chochote.

3. Mama mjane anaweza kuwaona pia watu wa kituo cha msaada wa kisheria kwa akina mama (WLAC) ambao wanapatikana kupitia link hii: WOMEN’S LEGAL AID CENTRE

Nakutakia kila la heri katika kuhakikisha si tu kwamba haki inatendeka bali pia ionekane kuwa imetendeka.
 
Last edited by a moderator:
kwa sababu mama ni mganga wa kienyeji kwanini asitumie utaalamu wake kuwazuia wasiichukue
hapo nafikiri ni maelewano tu yanatakiwa na pia kuangalia sheria zinasemaje
kuhusu mahakama ya kadhi haina umuhimu wowote kwani kesi inapoenda mahakamani wanaangali hawa watu walifunga ndoa ya namna gani kama ya ni serikali,kimila,kikiristo au kiislamu maamuzi yanatolewa kulingana na sheria za ndoa iliyotumika
watu wasitumie visingizio hivyo kuanzisha mahakama ya kazi kwani waislamu wana uwezo wa kuanzisha mahakama yao bila kuingiliwa na serkali hila tunapinga njia ya kodi zetu kutumika kugharamia mambo ya dini wakati serikali haina dini
 
Asante sana mkuu Makoye Matale. Huyu mama kaijenga hiyo nyumba kwa kushirikiana na mumewe yeye akichangia pesa anazopata kwa karibu watu. Matatizo yalianza siku ya msiba ambao huyu mama alitakiwa kuhama ili wauze nyumba.
 
Hivi sasa hakuna kesi yoyote inayopelekwa mahakamani ambayo haitumii kodi zetu. Kumbuka hilo.
 
Hivi sasa hakuna kesi yoyote inayopelekwa mahakamani ambayo haitumii kodi zetu. Kumbuka hilo.
mahakama ya kadhi ni kwa ajili ya waislamu kodi zina changiwa na watu wote wa dini tofauti kwanini tulazimishwe kodi zetu ziendeshe mambo ya dini nyingine halafu waislamu wanalalamika bakwata ni chombo cha serikali sasa hiyo mahakama kwanini wanataka serikali hiyo hiyo iwaundie mahakama ya kadhi
 
Asante sana mkuu Makoye Matale. Huyu mama kaijenga hiyo nyumba kwa kushirikiana na mumewe yeye akichangia pesa anazopata kwa karibu watu. Matatizo yalianza siku ya msiba ambao huyu mama alitakiwa kuhama ili wauze nyumba.

Hao ni Wanyang'anyi, ni lazima washughulikiwe kwa mujibu wa sheria. Haiwezekani watu wengine watumie jasho lao kutafuta mali huku wengine wakipiga misele tu na kuketi kwenye vijiwe vya kahawa wakisubiri ndugu zao wafe ili wajichukulie mali kirahisi.
 
mahakama ya kadhi ni kwa ajili ya waislamu kodi zina changiwa na watu wote wa dini tofauti kwanini tulazimishwe kodi zetu ziendeshe mambo ya dini nyingine halafu waislamu wanalalamika bakwata ni chombo cha serikali sasa hiyo mahakama kwanini wanataka serikali hiyo hiyo iwaundie mahakama ya kadhi

Kwani kesi za Waislam, za kimila, za wakristo sasa hivi zinasikilizwa wapi kama si mahakama hizo hizo na fedha za kodi hizo hizo? Fikiri.
 
Mwisho wa siku, hata Waislaam wakishindana huko mahakama ya kadhi, watapelekana kwenye mahakama za Serikali.

Labda wa ukane Uislam wao. Lakini kitu kama hicho sahau.

Na hicho unachosema wewe ndiyo maana tunataka Mahakama ya Kadhi itambuliwe kikatiba ili kuzuwia mambo kama hayo ya kupelekana mahakama isiyo ya kadhi. Bila kuitambuwa mahakama ya kadhi kikatiba kesi zitaendelea kuchukuwa muda mrefu na kuitia gharama kubwa serikali kama ilivyo sasa.

Mahakama ya kadhi ni solution, kwani Waislam wataridhika kuwa kesi zao zinasikilizwa ki dini yao na pia ucheleweshaji utakuwa hakuna na hivyo kupelekea haki kupatikana kwa wakati na gharama ndogo kwa walipa kodi.

Kumbuka. Justice delayed is justice denied.
 
Ana haki kabisa maana kaijenga pamoja na mumewe. angekuwaameikuta hiyo nyumba ingekuwa shughuli hapo. Sasa mwambie aende kwenye kituo cha sheria kinachowatetea wanawake. Hata wakiichukua kwa sasa atapewa tu haki yake. Nadhani ni TAMWA. Hata akienda mahakamani yeye mwenyewe kushitaki mbona sheria inamtetea. Kikubwa mwambie awe tayari kupambana. Yaani awe strong, asiogope. Akiogopa au akikaa kinyonge watamwonea. Awe ngangari. Na wewe hapa umsaidie sana sana.

Back
Top Bottom