Msaada wa ushauri wa biashara ya usafirishaji wa abiria kwa basi

Msaada wa ushauri wa biashara ya usafirishaji wa abiria kwa basi

Alex777

Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
30
Reaction score
4
Habari wana JF,

Samahanini kaka &,Dada mlioko humu, ila nalikua naomba ufafanuzi Kwa Mwenye ufahamu juu ya swala hili.

Mimi ni mfanyabiashara, na ninamshukuru Mungu ameniwezesha kupanda kiwango cha juu. Ahimidiwe Yeye Mungu. Wa Baba zangu Ibrahim Isaka na Yakobo!

Niko kwenye mazungumzo na kamouni Fulani ya utengenezaji mabasi ya abiria (mabasi yakusafiri safari za mbali "mikoani")

Nimejikuta naipenda biashara hii, na Upendo wangu juu ya hii biashara ya usafirishaji, imenifanya niingie kwenye mazungumzo yakutaka kuagiza mabasi kadhaa.

Ila naomba ushauri wenu Ndugu.

Kwa wenye uzoefu haswa. Kweli nitoe tsh 260ml Kuingiza bus Kwa route za mbali kweli na likanipa faida? (260ml ikarudi na faida)

Au Kwa wenye uzoefu zaidi wa biashara mnaweza kunipa ushauri Kwa mtaji huu ni biashara ipi mbali na usafirishaji ambayo naweza kuwekeza ikanilipa?

Ahsante.
 
kwanza kabisa ni lazima ukate comprehensive insurance hilo moja pili nunua yutong bei iko chee tatu usifikirie faida fikiria Huduma bora za luxury so siti ambazo basi litakuja nazo toka China ndio hizo hizo usizifanyie modifications eti upate watu wengi
 
kwanza kabisa ni lazima ukate comprehensive insurance hilo moja pili nunua yutong bei iko chee tatu usifikirie faida fikiria Huduma bora za luxury so siti ambazo basi litakuja nazo toka China ndio hizo hizo usizifanyie modifications eti upate watu wengi

kweli kabisa afikirie ubora huduma kwanza ndio awaze faida. maana kama huduma mbovu itakuwa vigumu kupata faida labda basi liwe linatembea njia isio na ushindani. abiria wengi siku hizi wana panga safari zao vizuri na wanapokwenda stand wanajua kabisa anapanda basi fulani kwa vile lina huduma nzuri kadhaa na uhakika wa safari pia. Ni abiria wachache sana ambao wanakwenda stand wakiwa hawana idea ya basi watakalopanda.
 
Kama unayo hiyo pesa fanya mpango uanze biashara nyingine. Biashara ya bus kipindi hiki tena uanze na bus moja sikushauri.
 
Kama unayo hiyo pesa fanya mpango uanze biashara nyingine. . . Biashara ya bus kipindi hiki tena uanze na bus moja sikushauri.

Naomba unifananulie basi Ndugu ole, changamoto zake haswa ni zipi?

Na kama waweza tambua mzunguko wake Wa fedha kwenye hii biashara ukoje!
 
Ndugu yangu wa damu ameishia tu kuzipaki pembeni basi 2 mpyaa Yutong

Biashara ya mabasi ya mikoani ina ushirikina sijawai kuona. Nilikua siamini km haya mambo yapo aseee nakumbuka skuiyo tunatoka Dodoma to Dar gari yetu ilikua inaondokaga saa 12:30 asubui sambamba na basi flani naliifadhi jina. Ndugu yangu tumetoka Dodoma mjini kufika sehem flani inaitwa mbande gari ilikua na abiria 35 lkn gafla tukaona ina abiria 10 tu. afu kila abiria anacheka cheka tuuu km mgonjwa wa akili. Kwakweli ile hali haisimliki mkuu.

ila napenda kukutia moyo tu kuwa unaweza kufanya biashara hiyo km unamitaji ya aina mbili.

1- Mtaji anzia
2- Mtaji endeshea

Mtaji anzia ndo iyo pesa ya manunuzi ya gari Milioni 280.

Mtaji endeshea tafuta tena kiasi km milioni 120 ivi kwa kuwa ili ufanye biashara bila stress itakubidi ukate bima ya kuitwa comprehensive insurance. Hii lazima ikugharimu si chini ya robo ya gharama ya manunuzi ya gari kwa mwaka.

kitu ambacho wakati mwingine ni pasua kichwa.
 
kwanza kabisa ni lazima ukate comprehensive insurance hilo moja pili nunua yutong bei iko chee tatu usifikirie faida fikiria Huduma bora za luxury so siti ambazo basi litakuja nazo toka China ndio hizo hizo usizifanyie modifications eti upate watu wengi

Mimi ni Mfanya Biashara, na sio mfanya biashara.

Ukiwa Mfanya Biashara unapozungumzia faida, inamaana kwamba BIdhaa zinakua na Ubora Wa Juu.

Ubora hilo ni jambo #1

NAOMBA IELEWEKE....
 
Inasisimua sana hii Mkuu. Tafadhali sana malizia. Abiria 25 walikwenda wapi? Hao 10 mliobaki nao mliwafanyaje?
 
Alex777,


Usinunue basi kwa cash.
Bima si lazima Comprehensive.
Usinuue basi jipya.
Kwa fedha hiyo waweza pata basi nne
Muhimu chunga jiko.(usibadili wapishi 2 katika kila jiko).
Tafuta wapambe stand>>Uza jina.
Jenga Urafiki na wapambe/Ma agent/wapiga debe...Hawa ndio wanauza jina la gari.
Siku moja moja waburudisha hasa ziki za uzinduzi.
Unazindua basi moja,moja.
Uwe na team ya maintanance hii kazi yake ni kwa usiku tu.
Mafundi,wataalamu wapo makazini ,wawezxa ongea nao kuja
kufanya consultation ya jiko mara moja moja usiku.
kwenye team ya wanao handle cash weka mademu.
ma inspector wawe wapambe na masela.
Utapata cash mpaka utaona maumivu.
baada ya hapo lete gari mpya .
 
Kwakuwa umedhamiria kufanya hii biashara. Unaweza ukaanza na TATA wanakupa kwa mkopo unapiga route ambazo hazina mabasi mengi then unakuwa unapata experience zaidi. Usinunue kwa cash. Unawalipa kwa mwezi makubaliano mlowekeana. Africa carriers wana hii huduma.
 
Ushirikina ktk biashara haukwepeki cha mcngi nunua ktk hp price, toa pesa ya kuanzia then lipa kwa instalment mkuu biashara ndo inavyokwenda kulipa cash kuna faida na hasara zake pia.
 
Kwa ufupi hii biashara ni nzuri tena sana, mtu asikukatishe tamaa kwamba hailipi au kwa kisingizio chochote, kuna mambo ya msingi ukiyafanya hayo umetoka comrade.

(Kwa wenye mawazo ya finyu wanaweza sema ni uchawi Noo!!)
 
Unaweza ukawa mgonjwa wakaja watu kukutembelea wengi watakupa ushauri mzuri wengine watakwambia huwezi pona.
 
Mkuu kwa kuanzia sikushauri uingie kwenye mabasi makubwa. 280mill uliokuwa nayo kuna option nyingi hasa kama unataka kuingia kweye biashara hii.... kwanza inategemea wewe mwenyewe unaishi wapi? Ila kama upo Dar es salaam nakushauri kama ifuatavyo. 100mill unapata hose namaanisha kichwa na tera lake, mil 90 unapata coaster 2, milioni tisini yako nyingine kaa nayo kwanza anagalia biashara zinaendaje kwanza.

Coaster kwa town trip zinalaza 100000/= hapo hudaiwi kitu na gari linalala na mafuta. Lori hesabu huwa inategemea unaenda wapi mkuu, cha muhimu jenga urafiki na transport agents wa Dar hapo na uwe na dereva wa ukweli, speed max 80km/h. Kama hutaki coaster ziwe na town trip unaweza kupaki mahali na kukodisha for long trip mfano misiba, harusi, na watu wa semina au shughuri tofauti cha muhimu ziwe na full AC, kama una rafiki maeneo ya migodini chonga naye uangalie uwezekano wa kuzikodisha kwenye migodi, inalipa sana na gari hazichoki.

Kama upo mikoani kama Mwanza, Moro, Mtwara, Mbeya basi anza na vihiace kama vitatu hivi, bei ya hiace ni 27mil x 3 = 71mill,mhuwa vinalaza 50000, x 3 = 150000x 30 = 4500000/=-500000 (service) = 4000000/=, ndani ya miaka mitatu zinakuwa zimelipa uza zote anza tena au ongeza na jitahidi kumaintain zile za zamani kwa service na kufunga vitu vipya.

Nafanya hizi biashara nina idea kiasi fulani, sikushauri uanze na mabasi makubwa kama ndio unaingia kwenye game?
 
mkuu kwa kuanzia sikushauri uingie kwenye mabasi makubwa,,, 280mill uliokuwa nayo kuna option nyingi hasa kama unataka kuingia kweye biashara hii.... kwanza inategemea wewe mwenyewe unaishi wapi??? ila kama upo dar es salaam nakushauri kama ifuatavyo.... 100mill unapata hose namaanisha kichwa na tera lake,, mil 90 unapata coaster 2,, milioni tisini yako nyingine kaa nayo kwanza anagalia biashara zinaendaje kwanza...

coaster kwa town trip zinalaza 100000/= hapo hudaiwi kitu na gari linalala na mafuta....
lori hesabu huwa inategemea unaenda wapi mkuu,, cha muhimu jenga urafiki na transport agents wa dar hapo na uwe na dereva wa ukweli, speed max 80km/h
kama hutaki coaster ziwe na town trip unaweza kupaki mahali na kukodisha for long trip mfano misiba, harusi , na watu wa semina au shughuri tofauti cha muhimu ziwe na full ac, kama una rafiki maeneo ya migodini chonga naye uangalie uwezekano wa kuzikodisha kwenye migodi,,, inalipa sana na gari hazichoki..

kama upo mikoani kama mwanza, moro,mtwara, mbeya basi anza na vihiace kama vitatu hivi, bei ya hiace ni 27mil x 3 = 71mill,, huwa vinalaza 50000, x 3 = 150000x 30 = 4500000/=-500000 (service) = 4000000/=,, ndani ya miaka mitatu zinakuwa zimelipa uza zote anza tena au ongeza na jitahidi kumaintain zile za zamani kwa service na kufunga vitu vipya..

Nafanya hizi biashara nina idea kiasi fulani,,, sikushauri uanze na mabasi makubwa kama ndio unaingia kwenye game??

Ahsante sana aisee,

Hakika umenifungua macho yangu na nimepata kuelewa. Umenipa hesabu rahisi na yenye maana mno. Ahsante mno.

Kwahio;
Mfano Kwa makadirio., Lori LA mizigo hesabu yake ni kiasi gani kwa siku!

Na coaster za mgodini zinakodiwaje!

Na bus kubwa hesabu yake Kwa makadirio ni kiasi gani!
 
ahsante sana aisee,

hakika umenifungua macho yangu na nimepata kuelewa.. Umenipa hesabu rahisi na yenye maana mno.. Ahsante mno.

Kwahio;
mfano kwa makadirio., lori la mizigo hesabu yake ni kiasi gani kwa siku.?!

na coaster za mgodini zinakodiwaje!

Na bus kubwa hesabu yake kwa makadirio ni kiasi gani.?!
Si chini ya dola 2500 kwa wiki kwenda kigali.
Ukishatoa gharama zote.
 
Ahsante sana aisee,

Hakika umenifungua macho yangu na nimepata kuelewa.. Umenipa hesabu rahisi na yenye maana mno.. Ahsante mno.

Kwahio;
Mfano Kwa makadirio., Lori LA mizigo hesabu yake ni kiasi gani kwa siku.?!

Na coaster za mgodini zinakodiwaje.?!

Na bus kubwa hesabu yake Kwa makadirio ni kiasi gani.?!

Mkuu malori ya mizigo yaendayo long safari huwa hayana hesabu kwa siku, ila linaposafili unafanya hesabu zako namaanisha mafuta kwenda na kurudi, mileage ya dereva na konda. Kama biashara nzuri kwa mwezi unaweza kulaza zaidi ya milioni 5 na service ya gari umeshafanya (usiwe mbaili kutengeneza gari na epuka ujanja ujanja kwenye maintenace).. gari likitoka safari ndefu linataka inspection nzuri.. Jitahidi tu kama umeamua kupiga kazi uwe bize na matranspoter ili ukienda na mzigo unarudi na mzigo, sometimes hawa matajiri wakubwa wanakuwa na tenda kubwa zinazotaka gari nyingi na yeye unakuta anazo chache, kwa hiyo huwa mnakubaliana anachukua magari tofauti tofauti anapiga stika zake mfanoo SAS au NAS ili awin tenda, hapa unapiga hela na ndani ya mwaka unaweza kushusha kitu kingine. Mfano oil com alikuwa na tenda ya tipper 200 Congo ilibidi nyingine akodi dar kwa mwaka mzima ( ila service juu yako na dereva wako, mafuta huwa juu yao).

Coaster mgodini kwanza inatakiwa iwe standard maana wanazifanyia inspection (ac na mikanda),, kupata hizi dili inabidi uwe mjanja mjanja siunajua tena tanzania yetu hii (rushwa) lazima mkubaliane na mtu,, wewe unaweza kulipwa 150000 per day na wanaingiza kwenye account kila mwezi ila wajanja watakakusimamia wanaweza kukuingizia 300000 na hiyo 150000 ya kwao. Mafuta huwa wanajaza wenyewe, dereva wakwako na service juu yako -- uzuri wake gari haichoki mapema maana safari ni fupi tu kila siku,,, na kucover 3000km service time inachukua muda, hii ukiiotea ukaingiza coaster zako 2 zinakutoa mrithi. Kiujumla kufanya biashara na migodi inalipa sana maana kwenye cash hawasumbui.

Hesabu ya basi kubwa za mikoani sina uzoefu nazo sana ila simple calculation unaweza fanya, mfano Dar - mwanza.
una abiria 65 x 40000 =2600000-200000 (posho) = 2400000 - 600000 (mafuta) = 1800000-300000(mengineyo) = 1500000 x 30 = 45000000 x 12 =540 mill (hizo hesabu ni za kukadilia na hapo nimekadilia basi liko full kuanzia Dar to Mwanza, hakuna abiria wa njiani, sometimes biashara inaweza kuwa ngumu labda ukawa na abiria 34-40 wanaokwenda moja kwa moja. Hapo pia hatujatoa hela za matairi na breakdown nyingine zinazoweza kutokea, hesabu za mafuta zinaweza kubadilika maana nimekadilia lita 300 kwa basi Dar - Mwanza).

KWA HIYO KWENYE HILI LA MABASI USIEGAMIE SANA HESABU ZANGU ILA FANYA UCHUNGUZI, ULAJI WA MAFUTA, POSHO, ABIRIA UNAOWEZA WAPATA WANAOENDA MWISHO WA SAFARI WAKIWA WAMEJAZA HAPO UTAPATA HESABU ZENYE MANTIKI KIDOGO MAANA NINA UELEWA MDODO KWENYE MABASI MAKUBWA YA SAFARI NDEFU,,

MUHIMU: Ishi vizuri na wafanyakazi wako, sometime wape vifavor wamepate hela mfano kama lori likienda BUKOBA na imekulipa hiyo safari kwa maana gari linaweza rudi tupu basi wape favor wabebe mzigo mdogo utakaowapa hata 500000/= kwenye basi unaweza kuwapa favor kwenye baadhi ya vimizigo atleast nje ya posho wapete hata 100000.
 
Mkuu malori ya mizigo yaendayo long safari huwa hayana hesabu kwa siku, ila linaposafili unafanya hesabu zako namaanisha mafuta kwenda na kurudi, mileage ya dereva na konda... kama biashara nzuri kwa mwezi unaweza kulaza zaidi ya milioni 5 na service ya gari umeshafanya ( usiwe mbaili kutengeneza gari na epuka ujanja ujanja kwenye maintenace).. gari likitoka safari ndefu linataka inspection nzuri.. Jitahidi tu kama umeamua kupiga kazi uwe bize na matranspoter ili ukienda na mzigo unarudi na mzigo, sometimes hawa matajiri wakubwa wanakuwa na tenda kubwa zinazotaka gari nyingi na yeye unakuta anazo chache, kwa hiyo huwa mnakubaliana anachukua magari tofauti tofauti anapiga stika zake mfanoo SAS au NAS ili awin tenda, hapa unapiga hela na ndani ya mwaka unaweza kushusha kitu kingine... mfano oil com alikuwa na tenda ya tipper 200 Congo ilibidi nyingine akodi dar kwa mwaka mzima ( ila service juu yako na dereva wako, mafuta huwa juu yao).

Coaster mgodini kwanza inatakiwa iwe standard maana wanazifanyia inspection (ac na mikanda),, kupata hizi dili inabidi uwe mjanja mjanja siunajua tena tanzania yetu hii (rushwa) lazima mkubaliane na mtu,, wewe unaweza kulipwa 150000 per day na wanaingiza kwenye account kila mwezi ila wajanja watakakusimamia wanaweza kukuingizia 300000 na hiyo 150000 ya kwao... Mafuta huwa wanajaza wenyewe, dereva wakwako na service juu yako -- uzuri wake gari haichoki mapema maana safari ni fupi tu kila siku,,, na kucover 3000km service time inachukua muda,,,, hii ukiiotea ukaingiza coaster zako 2 zinakutoa mrithi.. kiujumla kufanya biashara na migodi inalipa sana maana kwenye cash hawasumbui..

hesabu ya basi kubwa za mikoani sina uzoefu nazo sana ila simple calculation unaweza fanya,,, mfano Dar - mwanza.
una abiria 65 x 40000 =2600000-200000 (posho) = 2400000 - 600000 (mafuta) = 1800000-300000(mengineyo) = 1500000 x 30 = 45000000 x 12 =540 mill ( hizo hesabu ni za kukadilia na hapo nimekadilia basi liko full kuanzia dar to mwanza, hakuna abiria wa njiani, sometimes biashara inaweza kuwa ngumu labda ukawa na abiria 34-40 wanaokwenda moja kwa moja.. hapo pia hatujatoa hela za matairi na breakdown nyingine zinazoweza kutokea, hesabu za mafuta zinaweza kubadilika maana nimekadilia lita 300 kwa basi dar - mwanza). KWA HIYO KWENYE HILI LA MABASI USIEGAMIE SANA HESABU ZANGU ILA FANYA UCHUNGUZI, ULAJI WA MAFUTA, POSHO, ABIRIA UNAOWEZA WAPATA WANAOENDA MWISHO WA SAFARI WAKIWA WAMEJAZA HAPO UTAPATA HESABU ZENYE MANTIKI KIDOGO MAANA NINA UELEWA MDODO KWENYE MABASI MAKUBWA YA SAFARI NDEFU,,

MUHIMU; ishi vizuri na wafanyakazi wako,, sometime wape vifavor wamepate hela mfano kama lori likienda BUKOBA na imekulipa hiyo safari kwa maana gari linaweza rudi tupu basi wape favor wabebe mzigo mdogo utakaowapa hata 500000/=
kwenye basi unaweza kuwapa favor kwenye baadhi ya vimizigo atleast nje ya posho wapete hata 100000..

Ahsante sana Kwa ufafanuzi mzuri, umenifumbua macho.

Umenishauri vyema mno. Naomba uni "Pm" tafadhari.
 
sanurai Vipi kuhusu biashara ya mafuta, yenyewe imekaaje haswa.?!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom