Hawa watoto sijui nani kawaloga eti kwenda form five kwao ndio dili. Nina uncle wangu mwaka jana alipangiwa chuo cha MUST course ya umeme eti akataka kubadilisha kwenda form five kashauriwa na baba yake, mimi nikamwambia wewe jaribu kubadilsha ndio utanijua mimi ni nani. Uncle akanisikiliza akaenda MUST kufika kule nikamuombea abadilishe course asome civil kwa sababu tayari kuna watu wamesoma umeme kwenye familia akapata. Leo hii ananipigia simu anafurahia maisha ya chuo na anatarajia kulamba hela ya IPT muda sio mrefu.
Kifupi watu bado hawaelewi kuhusu hizi elimu za vyuo vya kati wao wanadhani five na six ndio dili, hawajui zama zimebadilika.
Ushauri wangu kwako usikubali mjukuu akupande kichwani, mshauri umuhimu wa kwenda chuo tena uzuri ni chuo cha afya, tumia democrasia kumshauri ikishindikana tumia nguvu tena ikiwezekana mwambie akienda form five hutomlipia ada, atakuja kukushukuru baadae.