joseph Goebble
Member
- Oct 11, 2014
- 8
- 3
Wakuu shikamoni,
Paa la nyumba yangu limeliwa vibaya na wadudu ambao siwafahamu, siyo mchwa, wako kama mende weusi wembamba kidogo kwa mende, wanapokuwa kwenye mbao wanakuwa viwavi (caterpilar) wanakula mbao ndani kwa ndani huku wakiacha matundu kama yanavyoonekana kwenye picha.
Wakishakula ndio wanageuka kuwa kama mende. wakila mbao inakuwa kama bua la muhindi yaani ndani ni hollow na linatoa unga wa njano.
Hawa wadudu wanakula mbao nzima na kuiacha kama unga wa njano.
Nimejaribu kupulizia dawa tofauti tofauti nilizokuwa napewa na wauzaji wa maduka ya pembejeo lakini haijasaidia, nimeona nijaribu hapa labda kuna mtu ameshakutana na kesi kama yangu anaweza akanipa uzoefu.
Hawa wadudu wanapokula mbao inalia kama msumeno unakata mbao.