Msaada: Wadudu wamekula mbao za dari, paa linataka kudondoka. Mtaalamu wa dawa anisaidie ushauri

Msaada: Wadudu wamekula mbao za dari, paa linataka kudondoka. Mtaalamu wa dawa anisaidie ushauri

Binafsi nilitumia dawa fulani inaitwa dudu killer (kama sijakosea spelling), wadudu wote walihama.

Iko hivi, baada ya kupaua (kabla sijaweka gypsum board) hao wadudu weusi walianza kupekecha mbao, nilienda duka la dawa za mifugo nikanunua hiyo dawa, nikachanganya na maji kidogo (kwa uwiano nilioshauriwa na aliyeniuzia) then nikatumia pump ile ya kubeba mgongoni inayotumiwaga mashambani kunyunyuzia dawa za kuua wadudu waharibifu. Nilipomaliza tu kunyunyuzia wadudu wote walikimbia.

Nilitumia Arusha, sijajua utakuwa mkoa gani.

Kila la kheri Mkuu.
Barikiwa sana mkuu nitajaribu hii. Ungenipa formula ya jinsi ya kuchanganya itapendeza sana. Na ukieza kutuma picha ya chupa ya hiyo sumu itakua umetusaidia wengi
 
Walikisaga kitanda changu sina hamu nao hao usiku nilikua nasikia wenyewe tuu wanavosaga chaga za kitanda.
 
Barikiwa sana mkuu nitajaribu hii. Ungenipa formula ya jinsi ya kuchanganya itapendeza sana. Na ukieza kutuma picha ya chupa ya hiyo sumu itakua umetusaidia wengi
Kwa bahati mbaya nipo nje ya Arusha kwa sasa, ila ntajaribu kuangalia kama ntampata mtu wa kunitumia picha ya hizo dawa then niweke hapa.

Kuhusu kufanya kazi, kwangu Mimi imefanya kazi, nilitumia mwezi wa pili mwaka huu na siku hiyo hiyo wadudu wote walitoweka na hawakurudi tena.

Pole sana, naelewa maumivu ya kuharibikiwa na kitu ulichotumia nguvu na gharama kukisimamisha. Ila itakaa poa.
 
Muongozo kuhusu Kiasi cha mafuta ya taa, oil chafu na chumvi ya mawe

Nenda kwenye gereji za gari au pikipiki, chukua oil chafu, nzuri ya pikupiki. Weka mafuta ya taa ili isiwe nzito, weka chumvi kuifanya iwe sumu na ipenye kwenye mbao. Hutasikia tena hao wadudu wakipekecha mbao.
 
Nenda kwenye gereji za gari au pikipiki, chukua oil chafu, nzuri ya pikupiki. Weka mafuta ya taa ili isiwe nzito, weka chumvi kuifanya iwe sumu na ipenye kwenye mbao. Hutasikia tena hao wadudu wakipekecha mbao.
Nmefwnya hivyo ulivyoelekeza lakini wadudu bado wako kazini
 
Hawa wadudu ni jipu aisee. Nipo napaka oil chafu mbao zangu, maana nilikuwa nishapaua. Sasa sijui itafanya kazi au kazi itaendelea
 
Engine oil iliyotumika, inaweza kuwa suluhisho kwa tatizo lako, inavyoonesha ulitumia mbao ambazo huwa wanasema ni treated lakini mbao hizo haziwi treated ipasavyo. Cha kufanya chukua oil chafu na brash ya rangi, paka kwenye mbao kama vile unavyopaka rangi hakikisha pia unanyunyiza kwenye matundu, itasaidia sana. Oil chafu hukimbiza hata nyoka!
Wale jamaa(wauzaji) wanaweka maji yenye rangi ya kijani tu ambayo sio dawa, wanatia watu hasara
 
Oil chafu inasaidia sana, kitu ambacho wengi wanasahau ni kwamba unapokata mbao, ile sehemu uliyokata pia unatakiwa upake vinginevyo labda ziwe ni mbao za kulowekwa au kuchemshwa kwenye dawa ambapo ile dawa inakuwa imefyonzwa na mbao mpaka sehemu ya ndani (wadudu wanakosa pa kuanzia kula hizo mbao)

Miaka ya nyuma kidogo ilikuwa inatumika sana dudu killer, sijui kama bado zipo. Sisi kwetu tuliitumia mwaka 2002 kwenye mbao za kupaulia paa, mpaka sasa ni miaka karibu 22 mbao hazijaguswa hata kidogo na hao wadudu

Kipindi cha baridi, wadudu wa mbao huwa wanaongezeka zaidi tofauti na kipindi cha joto(sijui huwa wanatokea wapi, wakianza kula mbao usiku huwezi kulala, ni afadhali hata kelele za Chura)
 
Back
Top Bottom