Msaada: Wadudu wamekula mbao za dari, paa linataka kudondoka. Mtaalamu wa dawa anisaidie ushauri

Msaada: Wadudu wamekula mbao za dari, paa linataka kudondoka. Mtaalamu wa dawa anisaidie ushauri

JAMANI NANI KAPAKA OIL CHAFU DARLINI NA AKAFANIKIWA KUPAMABANA NA HAWA WADUDU WARA MBAO? YAANI AKAONA WADUDU WAMEACHA KULA MBAO
 
Wakuu kwa dawa ya paa kuna dawa inaitwa dko 30c nicheki pm nikuunganishe na manufactures...upate kwa bei ya jumla

Kwa furniture au milango tumia aldrin au gammaline au gladiator hizi dawa pia njooni dm nitawaunganisha na mtu
 
JAMANI NANI KAPAKA OIL CHAFU DARLINI NA AKAFANIKIWA KUPAMABANA NA HAWA WADUDU WARA MBAO? YAANI AKAONA WADUDU WAMEACHA KULA MBAO
ukitaka uwaweze vizuri chukua Oil chafu changanya na petrol,Oil chafu inasaidia kuzuia mdudu asile mbao sasa ukiipakaa inaishia juu juu ila ukiichanganya na petrol inaingia hadi ndani ya mbao....jaribu uje unipe jibu
 
HAITAUNGUZA NYUMBA KWA KULIPILUWA NA JOTO LA BATI
 
Wakuu shikamoni,

Paa la nyumba yangu limeliwa vibaya na wadudu ambao siwafahamu, siyo mchwa, wako kama mende weusi wembamba kidogo kwa mende, wanapokuwa kwenye mbao wanakuwa viwavi (caterpilar) wanakula mbao ndani kwa ndani huku wakiacha matundu kama yanavyoonekana kwenye picha.

Wakishakula ndio wanageuka kuwa kama mende. wakila mbao inakuwa kama bua la muhindi yaani ndani ni hollow na linatoa unga wa njano.

Hawa wadudu wanakula mbao nzima na kuiacha kama unga wa njano.

Nimejaribu kupulizia dawa tofauti tofauti nilizokuwa napewa na wauzaji wa maduka ya pembejeo lakini haijasaidia, nimeona nijaribu hapa labda kuna mtu ameshakutana na kesi kama yangu anaweza akanipa uzoefu.

Hawa wadudu wanapokula mbao inalia kama msumeno unakata mbao.

View attachment 230852
View attachment 230853
Hii imenifumbua macho hata mie ninayejiandaa kupaua. Napaswa kuwa nao makini Hawa wauza mbao
 
Wakuu kwa dawa ya paa kuna dawa inaitwa dko 30c nicheki pm nikuunganishe na manufactures...upate kwa bei ya jumla

Kwa furniture au milango tumia aldrin au gammaline au gladiator hizi dawa pia njooni dm nitawaunganisha na mtu
Mambo vp mkuu? Mimi paa la nyumba limeshambuliwa na wadudu nmetumia dawa nyingi ambazo zinachanganywa na maji ikiwemo DDV, Colt lakini bado wanasumbua naomba msaada kwa wanaouza dawa za kuangamiza hawa wadudu
 
Nmemtafuta jamaa mmoja anasema wenyewe wanafanya treatment kwa kutumia gesi
Mkuu unaweza nisaidia contact za huyu jamaa, naona hawa wadudu wameshavamia darı niwawahi mapema kabla hawajaniachia msiba
 
Mkuu unaweza nisaidia contact za huyu jamaa, naona hawa wadudu wameshavamia darı niwawahi mapema kabla hawajaniachia msiba
Binafsi nilitumia dawa fulani inaitwa dudu killer (kama sijakosea spelling), wadudu wote walihama.

Iko hivi, baada ya kupaua (kabla sijaweka gypsum board) hao wadudu weusi walianza kupekecha mbao, nilienda duka la dawa za mifugo nikanunua hiyo dawa, nikachanganya na maji kidogo (kwa uwiano nilioshauriwa na aliyeniuzia) then nikatumia pump ile ya kubeba mgongoni inayotumiwaga mashambani kunyunyuzia dawa za kuua wadudu waharibifu. Nilipomaliza tu kunyunyuzia wadudu wote walikimbia.

Nilitumia Arusha, sijajua utakuwa mkoa gani.

Kila la kheri Mkuu.
 
Back
Top Bottom