Hili tatizo lilisha tatuliwa kwa kuezekea kenchi za chuma basi!!!!!!
Asikudanganye mtu .Huna jinsi ezua paa na weka chuma.
Gharama za chuma ni 100,000/-kwa kenchi katika span ya 40ft. Kwa kenchi moja.
Zinduka ndugu.
Fundi tusaidie siye wa huku mikoani namna gani tupake? (Msaada tafadhali)mimi ni fundi, ilikuwa rahisi kama ningekuwepo wakati wa kupaka hiyo dizeli, sio kupaka tu. kuna jinsi ya kufanya, mi nilijifunza kwenye kampuni ya wayugoslavia (partizansk put ya morogoro) wanatumia dizeli safi, mbao haichafuki na ina dumu
Aksanteni kwa ushauri.Ni Mbao za aina gani umetumia?kama ni Jamii ya crevilia au Mbao zenye Sukari ni bora kubadili Mbao zote za paa Kabila halijashuka.mimi nafanya kazi za carpentry,nimewahi kukutana na tatizo Kama Hilo almanusra nifunge Kiwanda sababu ilinichukua Mwaka mazima kufanya repair za bidhaa mbalimbali zilizokuwa zikirudishwa na wateja walionunua kwangu kwa kipindi cha miaka mitatu kabla na kukumbwa na tatizo hilo,nilijaribu dawa mbalimbali bila mafanikio mpaka nilipoamua kubadili mbao nilizotumia ndio ilikuwa suluhisho.Tabia ya huyo mdudu ni kwamba anakula mbao mpaka inapoisha ndio mwisho wa maisha yake,na ilivyo ni kama anajitengeneza tokana na mbao kama alivyo mdudu wa kokwa la embe,hivyo suluhu ya uhakika ni kubadili aina ya mbao ulizotumia,pole sana.
Hili Tatizo hata mimi limenikumba. Nasikitika kusema kuwa wauzaji wa hizi mbao wanasema ni Treated lkn kiuhalisia haziko treated, wanatutapeli hela zetu kwa kutuuzia mbao ambazo zimechovya kwenye dawa lkn hazija chemshwa na dawa.
Mti kwa kawaida una Starch au wanga ambao ndio kivutio kikubwa cha wadudu. Tunapo chemsha mbao tunaondoa hiyo starch na kufanya ubao/mbao kukosa starch ambayo ni chakula cha wadudu.
Hiyo Diesel na Oil chafu inaeeza kuzuia lkn ipamkwe mapema kabla ya mbao/ Kenchi kupigwa. Diesel na Oil Chafu inasaidia kukata supply ya oxygen endapo mdududu atataka kushambulia au akiwa ndani.
Dragnet IPO nyingi sana, hii inatoka Uingereza na siyo USA, inasambazwa na kampuni ya Juanco, Metro pia ni dawa nzuri.....nyingine ni Lamdacyhalothrin etcDragnet inatoka marekani...ni ngumu kuipata ajaribu DKO 30 c ipo kwenye hardware ni uhakika
Sorry, tutazitambuaje mkuu?Kweli kuna haja ya kuwa na namna yakutambua mbao ambayo imetibiwa vizuri ili kuweza kukwepa hizi hasara.
Nami sifahamu ndio maana nikaandika inabidi tujue namna ya kutambua .Sorry, tutazitambuaje mkuu?