Msaada: Wadudu wamekula mbao za dari, paa linataka kudondoka. Mtaalamu wa dawa anisaidie ushauri

Huyo anayesumbuliwa na mchwa kazi anayo
1. inabidi pesa imtoke hasa kufanys termite treatment.
2. mbao zote zipkwe dawa upya huko darini.
3. Nyumba yote ichimbwe mtaro ķuizunguka na dawa iwekwe.
4. kama milango nayo yaliwa matundu ya driliwe na dawa iwekwe
5.Ukitaka quotation kazi utáfanyiwa
 
Mafuta ya taa au oil chafu au diesel... ni kweli zinaua wadudu waliokwisha toboa mbao za dari? Hili janga linawasibu wengi.

-Kaveli-
 
Nina ushahidi wa nyumba mbili tuliotumia dizeli kwa zaidi ya miaka kumi hazijaguswa na mdudu yeyote mpaka leo.JARIBUNI !

Je kwa mbao ambazo tayari zimeshaliwa mdudu ameshaingia... tiba ni nini?

-Kaveli-
 
Wadau jibu kamili halikupatikana?
Hata kama zimeliwa tayar suruhisho ni hiyo hiyo diesel wadudu aiza watakimbia au watakufa humo humo ndani kwa kukosa hewa baada ya kupaka diesel coz nina ushahidi na hicho kitu...ilikuwa kwenye mbao za sofa zile nyepesi kila niki amka asubuhi nakuta vumbi la mbao chini kumbe wadudu wanachakata mbao tu ila nilipo apply diesel siku ona tena wale wadudu.
 
Mkuu kupaka oil kwenye paa lililokwisha kuezekwa ni mziki mnene.
Oil hupakwa kabla ya kuezeka paa.
 
Mkuu tafuta oil chafu na upakae hzo mbao na enjoy life
Mkuu siyo kila oil chafu ni muarobaini wa mchwa.

Oil chafu ya petrol engine si chochote si lolote kwa mchwa na dumuzi, hudumu kwa muda mfupi sana kisha hupoteza makali na wadudu kuanza kubungua.

Oil chafu ifaayo ni ya disel engine, ukipakaa hiyo ukaikoleza sawasawa, hudumu muda mrefu sana.
 
Diesel unapaka kwenye sofa ndani au unafanyaje mkuu?
 
libadili kwanza uweke jipya lisije likakutoa roho mkuu.
 
Nimepuliza dawa Dudumizi hajasaidia bado nawasikia wakatafuna mbao tafadhali je mtoa mada ulioata suluhisho
 
Nami kuna wadudu flan wanakula mbao za dari hatari japo nilinunua ambazo ziko treated, unacheki unga unamwagika tu na wanasikika wanapokuwa wanatafuna ndani kwa ndani, mpaka kero, mwenye ushauri tafadhali.
Ulipata suluhisho ndugu
 
Mkuu nahitaji unipe bei
 
Huwezi unguza nyumba?
 
Wakuu nami yamenikuta, naomba msaada niwafanyaje hawa wadudu, naona wanaanza kutoboa nje ya mbao ya kitanda.
Hapo diesel itasaidia?
 
Wadudu wapuuzi sana hawa, nimeua wawili jana manually ila kwa mbinde sana.. Dawa ni kujua lifespan yao ujue uvumilie muda gani sema kingine ni manene sana yatakuwa yanazaliana kwa kasi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…