Aiseee sawa buana pole kwa janga lililokukuta.
Tuliwahi lala Pangani kijiji kimoja before kuingia Saadan tulifika usiku muda ambao haturuhusiwi kuvuka mbugani, pale kuna hoteli mbili moja tulikuta imejaa ya pili ilikuwa kwenye ukarabati, na zingine ni guest houses zilizopo hapo kijijini, nikawashauri wenzangu tupaki beach tulale, Binafsi sikulala usiku kucha nilikuwa naangaza huku na huko walau nione chochote, i mean kitu au kiumbe chochote kisichoeleweka. Siku hiyo nilipanga nione yooteeee ambayo huwa nayasikia kwa stories juu ya fukwe za bahari.
Bila kumention maisha ya Nungwi beaches kule huwa tunakesha sana, hapa sijapaongelea maana huwa watu ni wengi wanaokesha. Pia mi huwa naenda (tunaenda )mara kwa mara Peponi Beach resort ni beach ambazo hazina watu tunakesha sijawahi ona mauza uza yoyote yale.