Simshauri huyu kutoa mimba kwasababu ameshamsaliti jamaa yake, basi ajifungue tu na kuhusu ndoa yao watayazungumza jamaa akijakumaind basi hamna ujanja. Hayo ndio madhara ya kukaa mbali na mwenzi wako inauma sana.
Najaribu kutafakari kwa umakini sana kuhusu ili sakata la huyu bidada,
naona mambo ni magumu kweli,
kutoa mimba ni dhambi na uuaji,
kutoka nje ya ndoa yako na kufikia kuzaa napo ni dhambi mbele ya mwenyezi mungu!,
Nachoweza kusema hapo ni kwamba,
Tukiangalia na uhalisia wa maisha yetu tunayoishi kwa sasa (hapa bongo)
haya mambo yanatokea/yameshawahi kutokea sana kwenye familia nyingi tu,
kwa mfano, unaweza kukuta familia ina watoto 4, lakini mmoja akawa sio zao la baba na mama!!!!!
Hii ina maana kwamba huyu dada amefanya kurudia makosa ambayo wengi tumekuwa tukiyafanya,
Yawezekana kabisa alizoea huo mchezo na mwishowe akaja kuona,
ni halali tu kutembea na mme wa mtu, kwa kuwa hata wengi wanaomzunguka katika maisha yake wanafanya hivyo pia!!!
USHAURI:
Ajaribu kutafakari kama bado anampenda mumewe,
na kama bado anampenda kweli, basi aitoe hiyo mimba ili anusuru ndoa yake!
Aachane na vitisho vya huyo mwanaume mwizi, kuwa asiitoe hiyo mimba!kwani huo ni upuuzi tu!
Lakini kama huyu dada hana mapenzi ya dhati na huyo mumewe, na hamwitaji tena katika maisha yake basi anaweza kuendelea kuitunza hiyo mimba!Na kusubiri kumlea mtoto!!
NI MCHANGO WANGU TU WAUNGWANA!!!