Mimi nilisumbuliwa miaka mingi sana,na nilipitia kipindi ambacho kilinitesa sana.
Kipind napangiwa O level kwenda kusoma hapo ndio ukawa mtihani kwangu nitaenda kuishi vipi,maaana nilikuwa nakoroma kama SIMBA.
Nilikutana na jamaa mmoja akaniambia ili upone tatizo hili lakupasa ulale KIFUDIFUDI.
Alinisisitizia ni zoezi gumu sana kama mtu hukuzoea kulala hivyo,ila kama unataka kupona basi lala hivyo.
Sikuwa na jinsi na lengo lilikuwa kupona,basi nikaanza kulala hivyo lakini nilipitia changamoto kubwa sana,yaani unashangaa umegeuka na kuanza kukoroma.
Basi ikawa tunashinda nikigeuka na kwasababu ukikoroma huwa unasikia mwenyewe naamka haraka na kulala KIFUDIFUDI.
Mpaka leo hui nimezoea na kipindi narud likizo nyumban walistaajabu kuona SIKOROMI KABISA nipo walipokuwa wananiuliza ni nani aliokupa hii dawa.
NB:MKUU JARIBU KULALA KIFUDIFUDI UTAFANIKIWA KABISA.