Msaada wakuu nakoroma hadi kero

Msaada wakuu nakoroma hadi kero

Baba mausingizi unaota au?
Wadau mwenye ufahamu kwenye hili tatizo,nakoroma sana nikilala na hali hii siipendi sinywi pombe,siyo mnene,ila tatizo linanitesa kuna dawa au njia yoyote kupunguza tatizo hili pls nipo serious
 
.
Screenshot_2019-07-20-09-09-41.jpeg

Nimevikuta Alliexpress huko
 
Watakao amua kulala kifudifudi wahakikishe wanakula chakula cha usiku mapema, usilale ukiwa tumbo limejaa chakula...

Kuna kufa ghafla kwa ulalaji huo.

Ulalaji bora ni kulalia Ubavu wa kulia, kisha unageukia kushoto na kuibia ibia chali.

Jitahidi kulala kifudifudi lakini hakikisha hupotezi "network"

Mimi nilisumbuliwa miaka mingi sana,na nilipitia kipindi ambacho kilinitesa sana.

Kipind napangiwa O level kwenda kusoma hapo ndio ukawa mtihani kwangu nitaenda kuishi vipi,maaana nilikuwa nakoroma kama SIMBA.

Nilikutana na jamaa mmoja akaniambia ili upone tatizo hili lakupasa ulale KIFUDIFUDI.

Alinisisitizia ni zoezi gumu sana kama mtu hukuzoea kulala hivyo,ila kama unataka kupona basi lala hivyo.

Sikuwa na jinsi na lengo lilikuwa kupona,basi nikaanza kulala hivyo lakini nilipitia changamoto kubwa sana,yaani unashangaa umegeuka na kuanza kukoroma.

Basi ikawa tunashinda nikigeuka na kwasababu ukikoroma huwa unasikia mwenyewe naamka haraka na kulala KIFUDIFUDI.

Mpaka leo hui nimezoea na kipindi narud likizo nyumban walistaajabu kuona SIKOROMI KABISA nipo walipokuwa wananiuliza ni nani aliokupa hii dawa.


NB:MKUU JARIBU KULALA KIFUDIFUDI UTAFANIKIWA KABISA.
 
Back
Top Bottom