Msaada wana JF naibiwa

ethicx

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Posts
311
Reaction score
126
Habari zenu wana jamvi hasa wajasiriamali wenzangu. Mimi nafanya biashara ya vipodozi pamoja na saloon ya kike lakini kadiri siku zinavyoenda sioni maendeleo na duka lipo sehemu nzuri ya biashara, ninavyoona ni kama niliyemueka pale dukani ananiibia sasa naomba ushauri wenu pia naomba kuelekezwa namna yakupiga mahesabu ya thamani ya vitu vilivyopo ili nijue nina hasara kiasi gani.
Nawasilisha msaada wowote nitashukuru.
 
Inabidi uwe unafanya stock taking kila baada ya miezi 6. yaani kwa mwaka mara 2.
ila kama unahisi mambo sio sawa jitahidi kuweka msimamizi wa dukani makini.
 
mkabidhi duka.

hesabu kila kitu weka na bei halafu muachie ukiwa unajua bei ya kununua na kuuza,idadi ya bidhaa,faida inayopatikana katika kila bidhaa halafu mwambie aendelee kila matumizi anayofanya akuandikie na kila anachouza akiandike utagundua kama unauza kwa hasara au kuna faida imefichwa.
 
Ilishaletwa mada hapa Jf mtu mmoja analalamika kwamba kwa nini mahoteli yetu ya kitalii hayaajiri watanzania ila huajiri wakenya kwa wingi. Mtu mmoja akajibu kwamba watanzania hawaajiriki kwa sababu ni wavivu,na wadokozi.
Kwa udokozi na wizi kwa kweli watanzania ni wataalamu, mpaka jambia la IGP wamelikwapua! Kwa hiyo ndugu yangu wa duka la vipodozi, kama huwezi kukaa huko dukani mwenyewe, basi imekula kwako. Hata umweke ndugu wa damu au sijui nani, atakuchomoa tu!
Mimi binafsi ilinibidi nifunge hoteli yangu baada ya kuandamwa na wizi/ udokozi wa niliowaajiri. Wa kaunta alidokoa hela za mauzo, wa jikoni ndo kabisaa walijichotea mavyakula na kupeleka nyumbani.
Ukimkamata mmoja, anavyopiga magoti na kuomba! Nikaona isiwe shida nikafunga hoteli!
 

Hiyo ni theory tu, practically haisaidi best wangu! Not with a tanzanian.
 
Inabidi uwe unafanya stock taking kila baada ya miezi 6. yaani kwa mwaka mara 2.
ila kama unahisi mambo sio sawa jitahidi kuweka msimamizi wa dukani makini.
Weye! stocktaking za muda mrefu hivyo? Ukifanya hivyo utakuta tu mavumbi kwenye shelves na hela haionekani
 
Weye! stocktaking za muda mrefu hivyo? Ukifanya hivyo utakuta tu mavumbi kwenye shelves na hela haionekani

Wamejaribu, wameweza wanasonga mbele kwa biashara ya madawa ya kulevya!
Tehe tehe tehe tehe.....

 
jaribu kupata nafasi ya kuuza mwenyewe mwezi mzima
 

Mie nigependa kujua ni nani huwa ananunua stock mpya? Na niwafanyakazi wangapi ulio ajili? Make sure kila kitu its on paper , record all trasaction, purchase, sales nd daily expense hii itakusaidia kujus kama unapata faida ama hasara na vilevile hii ndo uvivu wetu wengi wajasilimari wadogo kwani hufikiri ni big company tu zipasavyo kufanya. By the way nani husimamia duka lako? Acha uvivu its your money
 


wewe saloon na vipodozi unalia kuwa unaibiwa, sasa IGP mwema asemeje? kwani yeye kapigwa jambia la dhahabu ujazo wa kilo 3 l.
yaani biashara nzuri ni ile wewe ukiwa una usimamizi wa karibu kwa namna moja ama nyingine, lasivyo itakuwa karagha bao kwani kila siku utakuwa unalia lia tu :help: me pls, :help: me pls.
 
Unatakiwa kila siku jioni pitia fanya stocking na chukua mauzo kabidhi hela ya mahitaji ya kesho au nunua kabisa. Mara moja kwa wiki kaa wewe pia uone siku ktk biashara yako inakuwaje usijekuwa unalaumu bure. Hakuna biashara ya kufanyiwa siku zote lazima nawe uwepo
 
Reactions: BAK
mkuu hebu tuwasiliane nikuonyeshe software ambayo itakurahisishia kazi ya kuweka stock,kujua mauzo ya siku,wiki,mwezi,kujua madeni kiasi gani unadai au kudaiwa,malipo yamefanyika lini na nani kafanya malipo,nani kauza na kauza nini na tarehe ngap kwa sh ngapi...kama upo dar tuwasiliane 0714281313,kuonyeshwa ni bure kabisa.
 

Ninaomba jina LA software
 
we co Mchaga ndo mana biashara ni wewe co mtu mwingne . ukitaka biashara yako ikue kaa dukan au mweke mkeo mwenye uchungu na maendeleo yako co mtu wa pembeni . huyo anapita 2 tena anajua ukimfukuza anaenda kufungua yake keshapata uzoefu na kaiba na taji wa kuanzia. Pita kwenye maduka ya wachaga uone ujifunze hakai mtu anakaa mwenye mali babaangu.
 
ki ukweli biashara ya rejareja inasumbua kuna vitu kama chuma ulete.mtu anakuja na hela akishanunua anaondoka na hela zingine kimazingara akili kichwani kwako dada utafukuza wafanyakazi wengi kwa mtaji huo
 

Very good advice. Biashara zote zifungwe zibaki zinazo ajiri mwenye mali pekee. In other words. kila mtu ajiajiri. Au?
 
Una akili sana Mama Joe. Stock taking haina haja ya kusubiri miezi sita kama umeshastuka unaibiwa inabidi uifanye kila siku hii itakusaidia kugundua wizi haraka na hivyo kupunguza hasara yako, ukisubiri kufanya stock taking baada ya miezi sita hasara yako inaweza kuwa kubwa sana.

 
Last edited by a moderator:
kama umeajiriwa nakushauri uchukue likizo japo ya mwezi mmoja then kwa kipindi hicho usimamie biashara kwa kuwepo mwenyewe. hapo utajua hali halisi ya biashara yako na utapata akili uchukue hatua zipi baada ya hapo. otherwise jiandae kufilisika, kama ulikopa mkopo jiandae kufilisiwa kwa kuuziwa nyumba. na usishangae wanaokuuzia biashara zako baada ya muda ukawaona wamefungua biashara zao na wamekukimbia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…