Msaada wana JF wenzangu, nina msongo wa mawazo

Msaada wana JF wenzangu, nina msongo wa mawazo

MBULUKENGE jaribu kupita mahospitalini ambapo watu wanapambania maisha yao usiku na mchana halafu wewe unataka uyatoe kizembe kizembe tu.

Kaza wewe.
Kataa hilo shetani la kujiua.

Tafuta msaikolojia aliyekaribu nawe muda ambao unasubiri majibu ya wana jf.

Kama hujuani na wana saikolojia
Sema uko mahali gani tukutumie mawasiliano ya wanasaikolojia sehemu uliyopo.

Goodluck.
Kumbuka msaikolojia maarufu UDSM naye alijiua kwa msongo wa mawazo.
Kumbuka ni PhD wa masuala ya psychology.
Kwahiyo psychologist hawana umuhimu duniani. Useless
 
Binadamu wengi huwa tunadhani wote tuna kiwango sawa cha mapito au uwezo wa kuyastahimili. Kama huna kitu bora cha kusema ni kheri upite kimya, maana yawezekana mtu asidhamirie kufanya anachokisema ila tu ile njaa ya kutaka attention ya watu inadhihirisha emptiness aliyonayo ndani ya moyo wako

Mkuu, usidhani wote tunaopita humu au unaokutana nao kwenye maisha yako kila siku, maisha yao ni perfect, hapana mkuu

Kila mtu anapitia mazito ila tunayaficha kwenye tabasamu tu. So unaweza kuona wengine wanaishi na wewe unaishia ila kumbe wana mazito ambayo huwezi kuyabeba

Simaanishi ujilinganishe na circumstances za watu wengine ila uweze kuyaangalia maisha kwenye angle positive ili usije kufanya maamuzi permanent kwenye temporary situations..

Mungu akusimamie mkuu na usisahau kusali pia maana hizo roho zikiingia, huwa zinakutengenezea kiu inayokufanya utafute chochote negative ili uyachukie maisha yako zaidi kiasi cha kuhalalisha maamuzi yako.. Don't do that mkuu 🙏🏽
 
Anayetaka kujiua hanaga muda hata wa kupost ivi...Endelea na mapambano
Nakubaliana na wewe hii hali niliipitia nikiwa A level ambapo nilisoma boarding for the first time sikuwahi kupost wala kumwambia mtu yoyote, nilifake nipo normal japo ndani najijua mwenyewe lakini mwisho wa siku nikawa normal kweli na life ikasonga.
Huyu kuna mawili kama sio weak anayetaka kujustify weakness yake basi ni attention seeker
 
Binadamu wengi huwa tunadhani wote tuna kiwango sawa cha mapito au uwezo wa kuyastahimili. Kama huna kitu bora cha kusema ni kheri upite kimya, maana yawezekana mtu asidhamirie kufanya anachokisema ila tu ile njaa ya kutaka attention ya watu inadhihirisha emptiness aliyonayo ndani ya moyo wako

Mkuu, usidhani wote tunaopita humu au unaokutana nao kwenye maisha yako kila siku, maisha yao ni perfect, hapana mkuu

Kila mtu anapitia mazito ila tunayaficha kwenye tabasamu tu. So unaweza kuona wengine wanaishi na wewe unaishia ila kumbe wana mazito ambayo huwezi kuyabeba

Simaanishi ujilinganishe na circumstances za watu wengine ila uweze kuyaangalia maisha kwenye angle positive ili usije kufanya maamuzi permanent kwenye temporary situations..

Mungu akusimamie mkuu na usisahau kusali pia maana hizo roho zikiingia, huwa zinakutengenezea kiu inayokufanya utafute chochote negative ili uyachukie maisha yako zaidi kiasi cha kuhalalisha maamuzi yako.. Don't do that mkuu 🙏🏽
Nakumbuka kitaa walikua wanaona sisi wa kishua ila life la home tulikua tunalijua wenyewe tu😂😂😂.

Ukichangamana na watu ndo utajua kumbe hata wasanii unaowaona wanakula bata 24/7, ambao vijana wengi hutamani maisha yao kumbe wanatress hadi wanaangukia kwenye unga, ustaa wanaulipia gharama kubwa mno.

Furaha unayo mwenyewe na huzuni unayo pia.
 
Shida nini Mkuu?... Eleza hapa usaidiwe
Napitia mfululizo wa matukio yakunikatisha tamaa kabisa.
Nmejariwa kusoma but sijawahi kupata kazi.
Kinacho niumiza zaidi nlikua nmeachiwa gari 2 za home coaster kufanya biashara.
Nlikata TLB ya special hire nmefanya kama miezi sita fluently gari zinazingua nikajikuta nakua na madeni makubwa Ili niweze ku handle kuendesha biashara.
Kikubwa zaidi this week gari zote zimepata ajali na kuisha kabisa yaani ni scraper zote ata kukata haziwezekani.
Maisha yangu yamekua magumu ndani ya muda mchache tu Kila napojaribu kutafuta msaada naambulia patupu mwanamke kanikimbia na mtoto nahisi maisha yangu yamejaa nuksi na mikosi tu nakosa raha ya maisha kabisa.
 
Nakumbuka kitaa walikua wanaona sisi wa kishua ila life la home tulikua tunalijua wenyewe tu😂😂😂.

Ukichangamana na watu ndo utajua kumbe hata wasanii unaowaona wanakula bata 24/7, ambao vijana wengi hutamani maisha yao kumbe wanatress hadi wanaangukia kwenye unga, ustaa wanaulipia gharama kubwa mno.

Furaha unayo mwenyewe na huzuni unayo pia.
Kabisa mkuu, kila mtu anapambana na vita wapo.. Wanaopambana na kubwa zaidi ila wana ustahimilivu mkubwa zaidi na kuna wale wenye mitihani midogo ila ustahimilivu sifuri. Ndio maana ninalolipuuza mimi, wewe linaweza kukuua na lile unalolistahimili pengine linaweza kuniua pia..

Ndio maana huwa simcheki au kumdhihaki mtu pale anaponisimulia kitu kinachomsumbua hata kama kwangu ni kidogo maana najua ustahimilivu wake ndipo ulipoishia.
 
kabla ujajiua fikiria watu utakao waacha nyuma yako familia yako na marafiki wako

fikiria je ukifa hilo tatizo linalo pelekea upatwe na depression litakwishwa hakuna njia nyingine ya kulikabili? think

usione watu wana furahia maisha kwa ground kila Mtu kuna kitu kinamsumbua na kinampa depression kinouma ni Vile all human beings ni vinyonga tunajua ku pretend like everything is okay but Sio kweli

kila Mtu unae muona machoni kwako kuna failure ambazo Zina msonga kuna watu hawana kazi kuna watu ni wagumba kuna watu wanachapiwa nje kuna watu wamefeli na ndio tegemezi wa familia kuna watu tunanuka madeni tupo bankrupt mbaya mbovu kuna watu wana mgonjwa ukisimuliwa lazima upige goti umshukuru Mungu just know your not alone tupo wengi on the same boat

you know what Buda ingia bathroom oga vaa vizur toka home ingia mtaani head up chest out walk like king or like you don't give a fvck who is king
kutana na watu everything gonna be alright
Kama haelewi huu ushauri apate kisungura kwanza au k vant ndo asome tena
 
Screenshot_20240221-050406_Instagram.jpg

Usijiue ndugu iyo ni hali tu itapita , tafuta mwenza mtiane moyo
 
Napitia mfululizo wa matukio yakunikatisha tamaa kabisa.
Nmejariwa kusoma but sijawahi kupata kazi.
Kinacho niumiza zaidi nlikua nmeachiwa gari 2 za home coaster kufanya biashara.
Nlikata TLB ya special hire nmefanya kama miezi sita fluently gari zinazingua nikajikuta nakua na madeni makubwa Ili niweze ku handle kuendesha biashara.
Kikubwa zaidi this week gari zote zimepata ajali na kuisha kabisa yaani ni scraper zote ata kukata haziwezekani.
Maisha yangu yamekua magumu ndani ya muda mchache tu Kila napojaribu kutafuta msaada naambulia patupu mwanamke kanikimbia na mtoto nahisi maisha yangu yamejaa nuksi na mikosi tu nakosa raha ya maisha kabisa.
Brother mim niliwai kua na biashara na maisha mazuri sana, nikiwa mdogo tu, nilipoanza kufaidi matunda ya biashara yangu niliibiwa kila kitu dukani, sijui tukio lilitokea muda gani
Baada ya miez kadhaa kodi ya nyumba ikaisha na ilikua pesa nyingi sana.
Nikauza tv yangu tena niliiuza humu humu jf, kwa laki tisa na nilivompumbavu ile pesa nikaenda kulipa kodi sehem nyingine ikaisha, nikaanza kutafuta kazi huku na huko sipati,nikakonda nilibaki kongoro,
Nikapambana sana nikapata kazi duka la spear za magari, nikafanya badae nikafukuzwa kisa nilimtukana boss alinipapasa kalio.

Nikaanza kutafuta kazi upya na sikupata, badae nikawaza niuze viwanja vyangu lakin roho ikasema hapana kuuza uza vitu tena, Nikapambana, pambana na kupambana leo niko hapa maisha yangu naona mwanga tena japo si sana lakini naona mwanga.

Sijaweza kuandika mambo mengi lkn bro pambana pambana achana na upuuzi wa kutaka kujiua, shukuru Mungu amekupitisha kweny shida kwanza kabla ya raha.

Watu wanastory nyingi sana na za kuhuzunisha lkn leo wapo wanamaisha mengine.
 
Napitia changamoto za msongo wa mawazo, nafikiria kujiua tu.
Pole sana Comrade Mbulukenge! 🙁

Badala ya kuwaza kujiua, ni bora hata ungewaza kufanya soo lolote tu lile ili uende zako jela ukale ugali wa bure, kama maisha ya kitaa yanakuchanganya!

Kinyume na hapo, unatakiwa kupambana. Na ndiyo maana umeumbwa mwanaume. 💪 Wanaume tumeumbiwa mateso. Hivyo hatutakiwi kukata tamaa hovyo.
 
Napitia changamoto za msongo wa mawazo, nafikiria kujiua tu.
umefanya jambo zuri na la maana sana kuja humu Jukwaani kuchota ushauri, maarifa na uzoefu wa kutoka kwenye hali hiyo mbaya ya kiwango cha juu sana cha kukata Tamaa 🐒

kwa hakika kuendelea kujiuliza na kujijibu mwenyewe matokeo yake huwa ni hicho ulichokua unakifikiria, ni mbaya sana 🐒

bado fursa ya kurjea back on track unayo, ni wew tu kuamua na kukubali kwamba jambo fulani umeshindwa au huna na kwahiyo kujaribu jingine. Na kile ulichoshindwa kuwa kama fusra ya kujiimarisha zaidi zaidi ile mengine uyafanye kwa umakini, weledi na umahiri mkubwa zaidi...

Fanya yote uwezayo kwa bidii na bila kukata tamaa na Mungu Mwenyezi atakuonyesha njia na kukufanyia wepesi kuyafikia matarajio yako mema kwa uhakika zaidi 🐒
 
Back
Top Bottom