Msaada wana JF wenzangu, nina msongo wa mawazo

Msaada wana JF wenzangu, nina msongo wa mawazo

Napitia mfululizo wa matukio yakunikatisha tamaa kabisa.
Nmejariwa kusoma but sijawahi kupata kazi.
Kinacho niumiza zaidi nlikua nmeachiwa gari 2 za home coaster kufanya biashara.
Nlikata TLB ya special hire nmefanya kama miezi sita fluently gari zinazingua nikajikuta nakua na madeni makubwa Ili niweze ku handle kuendesha biashara.
Kikubwa zaidi this week gari zote zimepata ajali na kuisha kabisa yaani ni scraper zote ata kukata haziwezekani.
Maisha yangu yamekua magumu ndani ya muda mchache tu Kila napojaribu kutafuta msaada naambulia patupu mwanamke kanikimbia na mtoto nahisi maisha yangu yamejaa nuksi na mikosi tu nakosa raha ya maisha kabisa.
Hizi changamoto zako ni za kawaida sana. Hivyo huna sababu ya kuwaza mambo ya kipuuzi kichwani. Umiza kichwa kutafuta namna bora ya kuzitatua/kuzishinda! Na siyo kujiua.
 
Napitia mfululizo wa matukio yakunikatisha tamaa kabisa.
Nmejariwa kusoma but sijawahi kupata kazi.
Kinacho niumiza zaidi nlikua nmeachiwa gari 2 za home coaster kufanya biashara.
Nlikata TLB ya special hire nmefanya kama miezi sita fluently gari zinazingua nikajikuta nakua na madeni makubwa Ili niweze ku handle kuendesha biashara.
Kikubwa zaidi this week gari zote zimepata ajali na kuisha kabisa yaani ni scraper zote ata kukata haziwezekani.
Maisha yangu yamekua magumu ndani ya muda mchache tu Kila napojaribu kutafuta msaada naambulia patupu mwanamke kanikimbia na mtoto nahisi maisha yangu yamejaa nuksi na mikosi tu nakosa raha ya maisha kabisa.
Pole sana kwa yote unayopitia. Ni vigumu sana kupitia kipindi kama hiki cha changamoto. Kumbuka, hata kama mambo yanaweza kuonekana kuwa magumu sasa, kuna mwangaza mwishoni mwa kila kiza.

Usikate tamaa na endelea kushikamana. Kuhusu mali hizi ulizoachiwa, ni muhimu kufanya uchunguzi ili kujua asili yake, namaanisha kama ni za halali au la!. Pia, tafuta msaada wa kitaalamu ikiwa unahitaji ushauri zaidi. Tutaweza kusonga mbele kupitia haya yote. Endelea kuwa imara.
 
Kabisa mkuu, kila mtu anapambana na vita wapo.. Wanaopambana na kubwa zaidi ila wana ustahimilivu mkubwa zaidi na kuna wale wenye mitihani midogo ila ustahimilivu sifuri. Ndio maana ninalolipuuza mimi, wewe linaweza kukuua na lile unalolistahimili pengine linaweza kuniua pia..

Ndio maana huwa simcheki au kumdhihaki mtu pale anaponisimulia kitu kinachomsumbua hata kama kwangu ni kidogo maana najua ustahimilivu wake ndipo ulipoishia.
Yaah sure kiwango cha uvumilivu tumetofautiana sana.

Mimi navumilia sana dharau, huwa napuuza tu ila kuna washkaji zangu wakiona tu viashiria vya dharau panakua hapatoshi hapo.
 
Fikiria na jiulize tu kua unapotaka kwenda unapajua? Una uhakika kua patakua salama zaidi ya hapa ulipo?

Sidhani kama unapowaza kwenda utapokelewa vyema kwa njia hii unayotaka kutumia kwenda.

Shukuru kwa zawadi ya maisha na endelea kuyafurahia bila kujali magum unayopitia kwani sio ya kudumu
 
Kule kijijini kwetu kuna mtu alikutwa anataka kujitundika. Watu wakamshusha na kumpa kipigo cha mbwa mwizi kwanini anataka kujiua... nikajiuliza hawa jamaa wanatatua tatizo au wanaliongeza?
 
Mbulukenge--Mawazo ya kujiua/kujiona hauna thamani/kukata tamaa haya yote yanatoka kwa shetani.Inakuwa kama sauti inaongea ndani yako kwamba wewe ni failure tazama kila kitu hakiendi,wenzako wamepiga hatua wewe upo upo tu,nk.Kipindi natafuta kazi yangu ya kwanza nilipitia kipindi cha kuchanganyikiwa ila kwa sala nilivuka salama na nilipata kazi(nilikuwa sina cv na wala transcript bado sijachukua chuo).Katika kusali kwangu nilikuwa nakumbwa na roho mbili,roho ya kwanza ilikuwa inaniambia utapata kazi (hapa nilikuwa nafurahi sana,ningeamka nikavaa kabisa kama naenda kazini mfano wa nimepata kazi).Roho ya pili ilikuwa inaniambia nanj atakupa kazi mtu ambae unajifungia ndani mda wote?huchanganyikani na watu,cv huna na vyeti vya chuo hauna?(hapa nilikuwa nalia sana hata kula nilikuwa nashindwa nabaki nimelala tu)Basi hali ikaendelea hivyo Mwisho nilimwomba mwenyezi Mungu ufunuo juu ya hii kazi itatokea wapi.Haikuchukua muda mama aliniambia nimeota umepata kazi na yale maneno yakatimia
Somo----Haijalishi hali yako ni mbaya namna gani mkabidhi Mwenyezi Mungu uone makuu atakayofanya.Tenga muda wako funga,sali sana(sali kila wakati yaani sali hata moyoni mwako ukiwa kwenye shughuli nyingine au ukipata muda kidogo),achana na dhambi hususani mitandao ya kijamii isiyo na staha ifute na dhambi nyingine zinazovunja mahusiano yako na Mungu achana nazo,samehe wote waliokukosea kutoka moyoni .Ukifanya hivi utarudi hapa kutoa ushuhuda Mwenyezi Mungu ni mwenye huruma sana
 
Dear Mbulukenge
You may not see it, but everything will work out in the End. Have Faith, pray & leave it to God… ❤️❤️
1 Peter 5:7 Casting all your care upon him; for he careth for you.
Sasa ndiyo umuite mwenzio Mbulukenge😃
 
Ujasiri wa kutaka kujiua unatoka Kwa mapepo ya MAUTI, yanakuambia jiue tu jiue!!!

Yaambie hivi,

SITAKUFA, BALI NITAISHI, ILI NIUONE WEMA WA BWANA MUNGU WANGU, KATIKA NCHI YA WALIO HAI.

Moto wa kuzimu hausimuliki, funza wa shimo lile hawafi, Afadhali uendelee Kupambana Hadi utatoboa.

UBARIKIWE 🙏
 
Kaonane na wataalam wa saikolojia,pili penda sana kwenda kwenye ibada
 
kabla ujajiua fikiria watu utakao waacha nyuma yako familia yako na marafiki wako

fikiria je ukifa hilo tatizo linalo pelekea upatwe na depression litakwishwa hakuna njia nyingine ya kulikabili? think

usione watu wana furahia maisha kwa ground kila Mtu kuna kitu kinamsumbua na kinampa depression kinouma ni Vile all human beings ni vinyonga tunajua ku pretend like everything is okay but Sio kweli

kila Mtu unae muona machoni kwako kuna failure ambazo Zina msonga kuna watu hawana kazi kuna watu ni wagumba kuna watu wanachapiwa nje kuna watu wamefeli na ndio tegemezi wa familia kuna watu tunanuka madeni tupo bankrupt mbaya mbovu kuna watu wana mgonjwa ukisimuliwa lazima upige goti umshukuru Mungu just know your not alone tupo wengi on the same boat

you know what Buda ingia bathroom oga vaa vizur toka home ingia mtaani head up chest out walk like king or like you don't give a fvck who is king
kutana na watu everything gonna be alright
Tembea na huu ushauri mkuu Mbulukenge
 
Changamoto tumeumbiwa wanadamu na zipo kwa ajili ya kukabiliana nazo na sio kuzikwepa.

Pole sana kwa unayoyapitia Mkuu, Sali na amini kwamba ni mapito tu.

KAZA MWANANGU.
 
Napitia changamoto za msongo wa mawazo, nafikiria kujiua tu.
Mkuu pole Sana watu wengi wanaweza wasi kuelewe.

Binafsi nishafanya majaribio matatu ya kujiua........) lkn nashukuru Mungu Kwa pumzi ii mpaka sasa.

Fahamu kila mtu ana changamoto Zake ambazo kwake ni kubwa mno lkn still bado wana pambana

Cha msingi kabisa toka sehemu iyo ambayo wanakujua wanajua historia yako nenda kaanze upya makazi mapya na sahau kila kitu

Una anzaje Kama huna matatizo yoyote ya viungo jichanganye Kwawana Ata vibarua vya kupata hela ya kula tu itakusaidia kuyaona Maisha Kwa picha nyingine.

Na badae akili ikikaa sawa unaweza ludi kwenye network yako ya Zamani ukaanza upya kuitengeneza Kwa upya
 
Changamoto tumeumbiwa wanadamu na zipo kwa ajili ya kukabiliana nazo na sio kuzikwepa.

Pole sana kwa unayoyapitia Mkuu, Sali na amini kwamba ni mapito tu.

KAZA MWANANGU.
Lemama
 
Yaah sure kiwango cha uvumilivu tumetofautiana sana.

Mimi navumilia sana dharau, huwa napuuza tu ila kuna washkaji zangu wakiona tu viashiria vya dharau panakua hapatoshi hapo.
Kabisa mkuu, wengi hawawezi kupuuzia matusi au dharau 👏🏾👏🏾
 
Back
Top Bottom