Msaada wana JF wenzangu, nina msongo wa mawazo

Hizi changamoto zako ni za kawaida sana. Hivyo huna sababu ya kuwaza mambo ya kipuuzi kichwani. Umiza kichwa kutafuta namna bora ya kuzitatua/kuzishinda! Na siyo kujiua.
 
Pole sana kwa yote unayopitia. Ni vigumu sana kupitia kipindi kama hiki cha changamoto. Kumbuka, hata kama mambo yanaweza kuonekana kuwa magumu sasa, kuna mwangaza mwishoni mwa kila kiza.

Usikate tamaa na endelea kushikamana. Kuhusu mali hizi ulizoachiwa, ni muhimu kufanya uchunguzi ili kujua asili yake, namaanisha kama ni za halali au la!. Pia, tafuta msaada wa kitaalamu ikiwa unahitaji ushauri zaidi. Tutaweza kusonga mbele kupitia haya yote. Endelea kuwa imara.
 
Yaah sure kiwango cha uvumilivu tumetofautiana sana.

Mimi navumilia sana dharau, huwa napuuza tu ila kuna washkaji zangu wakiona tu viashiria vya dharau panakua hapatoshi hapo.
 
Fikiria na jiulize tu kua unapotaka kwenda unapajua? Una uhakika kua patakua salama zaidi ya hapa ulipo?

Sidhani kama unapowaza kwenda utapokelewa vyema kwa njia hii unayotaka kutumia kwenda.

Shukuru kwa zawadi ya maisha na endelea kuyafurahia bila kujali magum unayopitia kwani sio ya kudumu
 
Kule kijijini kwetu kuna mtu alikutwa anataka kujitundika. Watu wakamshusha na kumpa kipigo cha mbwa mwizi kwanini anataka kujiua... nikajiuliza hawa jamaa wanatatua tatizo au wanaliongeza?
 
Mbulukenge--Mawazo ya kujiua/kujiona hauna thamani/kukata tamaa haya yote yanatoka kwa shetani.Inakuwa kama sauti inaongea ndani yako kwamba wewe ni failure tazama kila kitu hakiendi,wenzako wamepiga hatua wewe upo upo tu,nk.Kipindi natafuta kazi yangu ya kwanza nilipitia kipindi cha kuchanganyikiwa ila kwa sala nilivuka salama na nilipata kazi(nilikuwa sina cv na wala transcript bado sijachukua chuo).Katika kusali kwangu nilikuwa nakumbwa na roho mbili,roho ya kwanza ilikuwa inaniambia utapata kazi (hapa nilikuwa nafurahi sana,ningeamka nikavaa kabisa kama naenda kazini mfano wa nimepata kazi).Roho ya pili ilikuwa inaniambia nanj atakupa kazi mtu ambae unajifungia ndani mda wote?huchanganyikani na watu,cv huna na vyeti vya chuo hauna?(hapa nilikuwa nalia sana hata kula nilikuwa nashindwa nabaki nimelala tu)Basi hali ikaendelea hivyo Mwisho nilimwomba mwenyezi Mungu ufunuo juu ya hii kazi itatokea wapi.Haikuchukua muda mama aliniambia nimeota umepata kazi na yale maneno yakatimia
Somo----Haijalishi hali yako ni mbaya namna gani mkabidhi Mwenyezi Mungu uone makuu atakayofanya.Tenga muda wako funga,sali sana(sali kila wakati yaani sali hata moyoni mwako ukiwa kwenye shughuli nyingine au ukipata muda kidogo),achana na dhambi hususani mitandao ya kijamii isiyo na staha ifute na dhambi nyingine zinazovunja mahusiano yako na Mungu achana nazo,samehe wote waliokukosea kutoka moyoni .Ukifanya hivi utarudi hapa kutoa ushuhuda Mwenyezi Mungu ni mwenye huruma sana
 
Dear Mbulukenge
You may not see it, but everything will work out in the End. Have Faith, pray & leave it to God… ❀️❀️
1 Peter 5:7 Casting all your care upon him; for he careth for you.
Sasa ndiyo umuite mwenzio MbulukengeπŸ˜ƒ
 
Ujasiri wa kutaka kujiua unatoka Kwa mapepo ya MAUTI, yanakuambia jiue tu jiue!!!

Yaambie hivi,

SITAKUFA, BALI NITAISHI, ILI NIUONE WEMA WA BWANA MUNGU WANGU, KATIKA NCHI YA WALIO HAI.

Moto wa kuzimu hausimuliki, funza wa shimo lile hawafi, Afadhali uendelee Kupambana Hadi utatoboa.

UBARIKIWE πŸ™
 
Kaonane na wataalam wa saikolojia,pili penda sana kwenda kwenye ibada
 
Tembea na huu ushauri mkuu Mbulukenge
 
Changamoto tumeumbiwa wanadamu na zipo kwa ajili ya kukabiliana nazo na sio kuzikwepa.

Pole sana kwa unayoyapitia Mkuu, Sali na amini kwamba ni mapito tu.

KAZA MWANANGU.
 
Napitia changamoto za msongo wa mawazo, nafikiria kujiua tu.
Mkuu pole Sana watu wengi wanaweza wasi kuelewe.

Binafsi nishafanya majaribio matatu ya kujiua........) lkn nashukuru Mungu Kwa pumzi ii mpaka sasa.

Fahamu kila mtu ana changamoto Zake ambazo kwake ni kubwa mno lkn still bado wana pambana

Cha msingi kabisa toka sehemu iyo ambayo wanakujua wanajua historia yako nenda kaanze upya makazi mapya na sahau kila kitu

Una anzaje Kama huna matatizo yoyote ya viungo jichanganye Kwawana Ata vibarua vya kupata hela ya kula tu itakusaidia kuyaona Maisha Kwa picha nyingine.

Na badae akili ikikaa sawa unaweza ludi kwenye network yako ya Zamani ukaanza upya kuitengeneza Kwa upya
 
Changamoto tumeumbiwa wanadamu na zipo kwa ajili ya kukabiliana nazo na sio kuzikwepa.

Pole sana kwa unayoyapitia Mkuu, Sali na amini kwamba ni mapito tu.

KAZA MWANANGU.
Lemama
 
Yaah sure kiwango cha uvumilivu tumetofautiana sana.

Mimi navumilia sana dharau, huwa napuuza tu ila kuna washkaji zangu wakiona tu viashiria vya dharau panakua hapatoshi hapo.
Kabisa mkuu, wengi hawawezi kupuuzia matusi au dharau πŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…