Msaada wana tatizo la uzazi

Msaada wana tatizo la uzazi

Akatanyukwire

Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
35
Reaction score
27
Habari wana MMU.

Naomba mnisaidie mawazo: Nimeoa miaka 7 iliyopita maisha na wife ni ya furaha kwa ujumla japo mara moja moja magomvi kidogo ila furaha kwa sana.

Tatizo langu wana MMU sijabarikiwa kupata mtoto, kila my wife akipata mimba zinatoka, kila mara mpaka sasa nahisi mwenzangu anakata tamaa, tumepima muhimbili (Mirija ya uzazi iko ok, cervix iko ok na nk, vipimo vyote vya damu vipo ok, doctor bingwa wa akina mama anakili kuwa wife hana tatizo lolote lakini ndio hivyo zinatoka).

Mpaka sasa ni zaidi ya mimba 8 zimetoka katika umri tofauti zingine miezi zaid ya 5, nyingine miezi miwili tu, zingine zinatoka ndani ya mwezi mmoja.

Nimehangaika vya kutosha mpaka wa waganga wa jadi tatizo liko pale pale sasa nimeona nililete kwenu wana MMU maana najua hapa kuna watu wengi wanajua mengi. naomba msaada wenu.

juzi nilikuwa naongea na wife mambo mengine ya maisha nikamwona kakata tamaa kwenye hili la kupata mtoto na alikuwa anataka kuniambia kitu nikawa nahisi anataka kuniambia kitu ambacho sipendi kukisikia kutoka kwake nikawa nimejibaraguza pale ili asikiseme nahisi ni kibaya.

Mimi sijawahi kumpa mimba msichana yeyote tofauti na yeye na sitaki kufanya hivyo nataka nikomaa na wife mpaka tuone la mwisho.

Nisaidie nifanyaje
 
pamoja na alosema Munkari, naomba uni pm nitakusaidia na Mungu akipenda basi mimba zitakuwa na mtoto atazaliwa.
 
Last edited by a moderator:
Wife wako alitoa mimba sana enzi hamjaoana mpaka kizazi kimelegea.
 
Mimba zaidi ya miezi mitano kutoka bila tatizo la kiafya?
Hapana kuna jambo nyuma ya pazia kama mnaimani ya kweli fanyeni maombi,
 
Umeeleza habari za hosp na waganga,ushawahi enda kwenye maombezi? Hakuna lishindikanalo mbele za mungu!!

umesema kweli yupo dada mmoja namfahamu naye kila mimba ilikuwa inatoka akaombewa sasa ni ana watoto,kwa sababu nia yake ni kupata mtoto ajaribu kila njia mojawapo hii ya kwenda kuombewa"................humweka nyumbani mwanamke aliye tasa awe mama wa watoto wengi,".."mimi niletaye wana karibu na kuzaliwa nisizalishe? mimi nizalishaye nilifunge tumbo? asema Bwana wa Majeshi. Isaya 66:9-.
 
naona maelezo yako yote ni hospital na kwa waganga kwa Mungu je Ushawahi? tuanzie hapa!
 
^^
Pole sana Mkuu kwa mapito magumu, kama madaktari bingwa wanaona hakuna tatizo !! unaonaje ukitafuta wastani wa mimba kutoka mf. Kama huwa zinatoka mwezi wa 5 na kuendelea! Akipata mimba, muda huo ukikaribia unamuweka BED REST mpaka atakapojifungua?
^^
 
  • Thanks
Reactions: Luv
mh!@Munkari ameshauri vizur iko nguvu mbele za Mungu wetu alie hai na ni mpango wake tuijaze dunia mwambie anaweza yote.
 
km hutojali ni PM
kwa msaada zaidi nakwambia atakuzalia watt
biblia inasema 'hakutakuwa na tasa wala mwenye kuharibu mimba. ....
 
gfsonwin ungemshauri kupitia hapa si ungesaidia wengi na wale ambao siyo member wanatupia macho yao hapa?
na hii ndio advantage ya kuwa memba hapa......kwani imeandikwa si busara kuwapa mbwa chakula cha watoto ingawa mbwa anaweza kuokota makombo chini ya meza ya bwana wake.
 
kwa maelezo yake hajawahi kutoa mimba. vipimo halivyofanyiwa vinaonesha kizazi kiko sawa
 
Habari wana MMU.

Naomba mnisaidie mawazo: Nimeoa miaka 7 iliyopita maisha na wife ni ya furaha kwa ujumla japo mara moja moja magomvi kidogo ila furaha kwa sana. tatizo langu wana MMU sijabarikiwa kupata mtoto, kila my wife akipata mimba zinatoka, kila mara mpaka sasa nahisi mwenzangu anakata tamaa, tumepima muhimbili (Mirija ya uzazi iko ok, cervix iko ok na nk, vipimo vyote vya damu vipo ok, doctor bingwa wa akina mama anakili kuwa wife hana tatizo lolote lakini ndio hivyo zinatoka).

Mpaka sasa ni zaidi ya mimba 8 zimetoka katika umri tofauti zingine miezi zaid ya 5, nyingine miezi miwili tu, zingine zinatoka ndani ya mwezi mmoja.

Nimeangaika vya kutosha mpaka wa waganga wa jadi tatizo liko pale pale sasa nimeona nililete kwenu wana MMU maana najua hapa kuna watu wengi wanajua mengi. naomba msaada wenu.

juzi nilikuwa naongea na wife mambo mengine ya maisha nikamwona kakata tamaa kwenye hili la kupata mtoto na alikuwa anataka kuniambia kitu nikawa nahisi anataka kuniambia kitu ambacho sipendi kukisikia kutoka kwake nikawa nimejibaraguza pale ili asikiseme nahisi ni kibaya.

Mimi sijawahi kumpa mimba msichana yeyote tofauti na yeye na sitaki kufanya hivyo nataka nikomaa na wife mpaka tone la mwisho.

Nisaidie nifanyaje

pole sana. kuna ile kitu wataalamu wanaijua inahusika na rhesus factors in blood group..upime hiyo kitu..mi sina utaalam bali nina idea tu, yaani unaambiwa kama hizo chembechembe zenu haziendani piga ua hapatikani mtoto hapo. ikitoke ni mmoja tu kwa bahati. usimuache mkeo mnaweza ku adopt watoto.
 
  • Thanks
Reactions: Luv
Pole kiongozi' lakini hongera sana kwakuwa na moyo wa ujasiri na uvumilivu' huo ndo uanaume mkuu!!

Pamoja na maombi' lazima ukumbuke imani inaanza nawewe na mkeo' maana hata mkafunga miaka mia kwa maombi kama imani yako ni haba itakuwa ni sawa na bure.! Hivyo amini kwamba hakuna jambo linaloshindikana kwa muumba, na kwakufanya hivyo next time utakuja na habari nzuri hapa jukwaani.

Kila lakheri ndugu!
 
^^
Pole sana Mkuu kwa mapito magumu, kama madaktari bingwa wanaona hakuna tatizo !! unaonaje ukitafuta wastani wa mimba kutoka mf. Kama huwa zinatoka mwezi wa 5 na kuendelea! Akipata mimba, muda huo ukikaribia unamuweka BED REST mpaka atakapojifungua?
^^
ntajaribu nione
 
Back
Top Bottom