Msaada: Wanaotoa magari bandarini kwa kukopesha malipo ya kodi

Manjagata

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2012
Posts
13,942
Reaction score
15,371
Wadau salama hapa ndani? Niliwahi kusoma uzi hapa JF kwamba kuna raia wanaosaidia kutoa gari bandarini hata kama huna pesa ya kulipia TRA mnaingia makubaliano ya kulipia kidogo kidogo baada ya yeye kulipa. Hii imekaaje? Hakuna utapeli ndani yake?

Nina mpunga kidogo hapa ambao unatosha tu kulipia gari mpaka kuifikisha bandarini, sasa nataka nipate hao wadau ili tufanye biashara. Naomba ushauri wenu wa kitaalam wakuu, maana matapeli mayo yametamalaki kila kona nisije nikapigwa!
 
Mkuu kumiliki gari ni anasa. Wazee wetu walikuaga wanatembea sanana hawakuniliki magari hawakupungukiwa na kitu na mambo yalienda. Kutembea pia ni mazoezi kuna Magonjwa mengi ya kizembezembe sasa hivi kama kisukari na presha yanaepukika tu ukiwa unatembeatembea kuliko mda wote unaendesha gari.
 
Ni bora zaidi ukasubiri hadi upate mpunga wa kutosha kuliko kuanza kwa mkopo wenye riba kubwa!
 
Kwanini usisubiri upate hela yote?

Suala unalosema labda itokee kama dharula, pengine mambo yaharibike wakati umeshaagiza, ya nini kuanza kujipa riba bila sababu za msingi kwani una haraka gani?

Kama umeshaagiza, then ikatokea umekwama kuna bonded warehouse linakaa huko na kila mwezi unalipia around 200k, ila usirogwe ukaacha gari bandarini, malimbikizo utakayoletewa utalikimbia gari lako.
 
Mkuu kumiliki gari ni anasa. Wazee wetu walikuaga wanatembea sanana hawakuniliki magari hawakupungukiwa na kitu na mambo yalienda. Kutembea pia ni mazoezi kuna Magonjwa mengi ya kizembezembe sasa hivi kama kisukari na presha yanaepukika tu ukiwa unatembeatembea kuliko mda wote unaendesha gari.
Ukumbuke babu zako hawakutumia simu kufikisha ujumbe. Walikuwa wakitembea umbali mrefu hta kama taarifa ni muhimu. Pia hawakutumia fedha kuuza au kununua, ishi kama wao bila FB wala WhatsApp.
 
Kuagiza gari Ni sawa na kujiunga CHADEMA. Unatakiwa uwe na roho ngumu. Kuagiza na kulipia Ulaya si kazi. Kazi iko hapo mtoni kwetu.
Import duty.
Railway levy
Excise duty
Excise duty due to age
VAT
Import declaration fees
Handling
Wharfage
Number plate
Insurance
VAT on handling
VAT on wharfage
Agency fees
PETROL
Ukiona mtu anaendesha gari lake binafsi usimlaumu akikunyima lift.
 
Kifupi usiagize gari kama huna hela ya kulipia kodi. Ni uzwazwa.

Kama bei, bima na usafiri ni 10M kwa mfano, uje kodi zote ni 10M nyingine.
 
Kumiliki gari kwa kulazimisha ni Kujiongeze stress, umaarufu utageuka majuto.
 
Kuagiza gari Ni sawa na kujiunga CHADEMA. Unatakiwa uwe na roho ngumu. Kuagiza na kulipia Ulaya si kazi. Kazi iko hapo mtoni kwetu.
Import duty.
Railway levy
Excise duty
Excise duty due to age
VAT
Import declaration fees
Handling
Wharfage
Number plate
Insurance
VAT on handling
VAT on wharfage
Agency fees
PETROL
Ukiona mtu anaendesha gari lake binafsi usimlaumu akikunyima lift.
Nimegundua kwanini watanzania wengi wakiendesha magari yao wananuna,yaani wanakuwa kama wana hasira flani hivi, sasa kosa umgonge hasira zote anakumalizia wewe.
 
Kwa zama hizi kama unataka kupiga chenga unaweza poteza yote mkuu
Hapana chezea mitano tena
 
Kama haujawa tayari kumiliki gari ni vyema ukaendelea kujichanga kuliko hilo unalolitafuta.
 
Usithubutu kufanya hiyo arrangement ya kuchukua hela ya kulipia ushuru kutoka kwa loan sharks. Wanachofanya, gari ikitoka wewe unachukua file la document gari analichukua aliyekukopesha.

Kifuatacho baada ya hapo uhakikishe unapata pesa ndani ya mwezi mmoja baada ya kupewa pesa ili ulipe deni na 10% au 15% au 20% au 25% au 30% kama riba kutegemea makubaliano yenu. Ikipita mwezi mmoja riba inapandiana na waweza jikuta unadaiwa pesa zitakazokulazimisha kuacha gari na wewe kuambulia kupewa pesa kidogo tu ukipigiwa hesabu ya kiasi ukichonunua gari! Inasemekana watu hawa wanatumia hata ushirikina ili ushindwe kukomboa gari lako
 
Kwa zama hizi kama unataka kupiga chenga unaweza poteza yote mkuu
Hapana chezea mitano tena
Hivi Watanzania huwa mnasoma contents kwenye habari mkazielewa kweli? Kwenye maelezo yangu kuna mahali nimesema nataka kukwepa kodi? Maana yangu ya kuuliza, nilizungumzia habari ya kununua gari tena humu humu JF, ubaya ule uzi nimeukosa. Kuna mdau mwenye kampuni ya clearing and forwarding akanikomalia kwamba hata kama huna hela ya kulipa kodi kwa sasa hivi wao katika kampuni yao huwa wanaingia makubaliano wanalipia gari inatoka. Ndiyo maana nikauliza hii imekaaje?
 
Usithubutu kufanya hiyo arrangement ya kuchukua hela ya kulipia ushuru kutoka kwa loan sharks. Wanachofanya, gari ikitoka wewe unachukua file la document gari analichukua aliyekukopesha.

Kifuatacho baada ya hapo uhakikishe unapata pesa ndani ya mwezi mmoja baada ya kupewa pesa ili ulipe deni na 10% au 15% au 20% au 25% au 30% kama riba kutegemea makubaliano yenu. Ikipita mwezi mmoja riba inapandiana na waweza jikuta unadaiwa pesa zitakazokulazimisha kuacha gari na wewe kuambulia kupewa pesa kidogo tu ukipigiwa hesabu ya kiasi ukichonunua gari! Inasemekana watu hawa wanatumia hata ushirikina ili ushindwe kukomboa gari lako
Sawa sawa kabisa mkuu! Ushauri murua kabisa huu! Jamaa alinikomalia mno mpaka nikashangaa! Ndiyo maana nikaja hapa jukwaani kuulizia kama kuna mdau alishashiriki hii biashara haramu! Hapo umesema kweli mkuu na nimekuelewa vizuri kabisa!
 
Usithubutu kufanya hiyo arrangement ya kuchukua hela ya kulipia ushuru kutoka kwa loan sharks. Wanachofanya, gari ikitoka wewe unachukua file la document gari analichukua aliyekukopesha.

Kifuatacho baada ya hapo uhakikishe unapata pesa ndani ya mwezi mmoja baada ya kupewa pesa ili ulipe deni na 10% au 15% au 20% au 25% au 30% kama riba kutegemea makubaliano yenu. Ikipita mwezi mmoja riba inapandiana na waweza jikuta unadaiwa pesa zitakazokulazimisha kuacha gari na wewe kuambulia kupewa pesa kidogo tu ukipigiwa hesabu ya kiasi ukichonunua gari! Inasemekana watu hawa wanatumia hata ushirikina ili ushindwe kukomboa gari lako
Loan sharks wabaya sana. Siku ya mwisho ikifika kabla riba haijaongezeka wanazima simu zote na mjini wanahama.
Wanajitokeza siku ya tatu au nne na kuanza kukulaumu kwanini hujalipa. Hapo hapo riba inaongezeka Mara dufu.
 
Hivi Watanzania huwa mnasoma contents kwenye habari mkazielewa kweli? Kwenye maelezo yangu kuna mahali nimesema nataka kukwepa kodi? Maana yangu ya kuuliza, nilizungumzia habari ya kununua gari tena humu humu JF, ubaya ule uzi nimeukosa. Kuna mdau mwenye kampuni ya clearing and forwarding akanikomalia kwamba hata kama huna hela ya kulipa kodi kwa sasa hivi wao katika kampuni yao huwa wanaingia makubaliano wanalipia gari inatoka. Ndiyo maana nikauliza hii imekaaje?
Tusiandikie mate wino upo.
Ingia mkataba na hao watu.
Angalizo.
Wataandika riba Ni asilimia kumi, lkn hawasemi Kama Ni kwa mwaka. siku ya kulipa wstakuambia hiyo asilimia kumi Ni kwa mwezi, hapo ndio jasho litakutoka
 
Kifupi usiagize gari kama huna hela ya kulipia kodi. Ni uzwazwa.
Kama bei, bima na usafiri ni 10M kwa mfano, uje kodi zote ni 10M nyingine.
Mbona Sibonike na wewe unatembelea gari la mkopo? Kwa hiyo na wewe ni Zwazwa?
 
Back
Top Bottom