Dah mkuu nimejarib kubana ili uishi bila kuchanganyikiwa lakini natoka patupu.Mbinu zangu zahitaj usiri wa hali ya juu ila.Mbinu yangu itakufaa ikiwa utahitaji kutoka kwenye iyo kazi yaani ujiajiri au upate chanzo kingine cha kukuongezea kipato.
*Kwa mshahara wako kubali urudi nyuma kapange nyumba iliyo jirani na kazini ili uende kwa miguu ofcn na kupunguza gharama za usafiri ikabid panga nyumba ya kiza kuondokana na gharama za umeme simu utachaj 200 vibandan.
*Punguza gharama za simu toka mb na dk utumie sms tu naamini haitazid 1500 kwa mwezi (kifurushi cha mwezi)
*Kula 1500 kwa siku yaani 1000 mchana uwapo kazini na 500 usiku Chai na kitafunwa (utapika nyumban mana chai mgahawani usiku utaonekana mchawi)
*Achana na habar zote za starehe ziache tu zikupite.
*Kuhonga iwe ni mwiko nalo hili ni gumu kuliko ila ukiwa karibu na mungu ukawa muumin hakika hili utalishinda.
kumbuka yote hayo unayoyafanya sio kuepukana na maden bali upate akiba sio yakuongeza thaman ndani au kubadil smartphone bali kubadili kazi kujiajiri au likawa gumu kujiajir basi kupata kazi ingine ya ziada itakayokuwezesha kuongeza kipato.
#Kwa mchanganuo hapo juu nimepata
Kod ya nyumba 30000 umeme na maji
#Chakula 1500*30=45000+ 5000(Sukar majani)= 50000
50000+30000=80000 ( yaweza kupungua ikiwa utapanga nyumba ya kiza)
80000+10000(vocha(sms)+sabuni+ usafir wa dharula nk)
90000 kwa mwezi.
120000-90000=30000
30000 ndiyo akiba ambayo utaitumia kutengeneza mtaji wa biashara ingine na dharula kama kuumwa nk)
Kama nakuona utakavyo taabika pia vibarua na vikazkaz vya mtaani usijivunge jichanganye.Binafsi nimeishi kwa gharama ya 60000 kwa mwezi.
Kod 20000+5000 umeme maji hayazid 1000(200 dumu)
Kula 1000 kwa siku amazing story (nilikunywa chai na maandazi au mara moja moja na kufunga swaum za Sunnah nakufutur msosi wa 1000 jioni) Sifanyi kazi ngumu.
26000+30000=56000/= Iyo 4000 hapo 1500 vocha sms ndio kuwasiliana no kupiga,2500 dawa mswak+ sabuni+mafuta.
Nikutie moyo nalipa kod 80000 (chumba na sebule) frem za kaz baada ya kuongeza mtaji now nalipa 200000 kwa mwezi (frem 3).Nabadili mlo nitakavyo sio tena chai maandazi na kufunga swaum.
Bado napambana na haya maisha so ubahili ndio maendeleo yalipo.
Mtangulize Mungu na Fanya mambo kwaajili yako usiseme watanionaje akina fulani niliosoma nao.
Kila la kher na afya ndio mtaji wako.
Sent using
Jamii Forums mobile app