Msaada: Wanauchumi nitawezaje kusave mshahara wa laki moja na ishirini, ili nami niwe na mafanikio?

Msaada: Wanauchumi nitawezaje kusave mshahara wa laki moja na ishirini, ili nami niwe na mafanikio?

Hili suala nahitaji ushauri wa Wanauchumi

Ninafanya kazi/kibarua sehemu fulani huku jiji la kanda ya ziwa

Nimepanga chumba nalipia Kodi 30k per month,.bill ya umeme na maji pia

Natumia nauli kwenda na kurudi kibaruani

Sasa nataka mwaka ujao nianze kuweka akiba Ila najiuliza kwa pesa hii nitaweza kusurvival mwezi mzima bila kukopa sehemu

Lengo langu nianze kutunza fedha kuanzia 2020 ,Sasa Wanauchumi nipeni mbinu za kufanikisha jambo hili kwa salary ya 120K

Asanteni
Hapo cha kufanya,
Tafuta mchumba kisha mchumbie ili awepo nyumbani awe anakutunzia kibubu chako,

Apo utaona mwenyewe savings zako zinaenda vizuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa mama ntilie, mimi na wadada wangu wa biashara wote tunakula hapo hapo na faida ipo na msingi upo.
Kwetu pia mama ntilie ndo biashara iliyonilea na kunisomesha na bajeti ya kula wote hapo hapo.
Mimi nakumbuka tunatembea kwa miguu na wanafunzi wenzangu tunawahi kwetu kula ukoko na maharage, aiseee hawasahau mpaka kesho ulivyokuwa mtamu.
Aiingii akilini kula unachouza!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Laki 5 ya robota la mashati utampa kaka?
Mkuu hongera kwa uamuzi wa kuanza kusave swala la kuweka akiba ni tabia au culture ambayo ni natural blessed au mtu unaweza kujifunza na kujizoesha..Kama hauna utamaduni wa kuweka akiba ata upate million 5 kwa mwezi Ni ngumu kuweka akiba...Kingine ni lazima kuwe na strong purpose ya kufanya saving bila hiyo utakosa passion ya kusave na utachoka. Fanya utafiti ni biashara gani ya mtaji wa laki tano unayoweza kufanya ukitoka kazini tumia opportunity ya kuwa lake zone biashara zinafanyika holela..laki tano inatosha kupata robota zuri la mashati ya kiume weka kwenye racket ukitoka kazini Mwaga mzigo ata nje ya Bank hakuna shidda.. muhimu kitambulisho Cha machinga saa 10 mpaka saa 12 utakosa wateja.. huo mshahara wako ni mkubwa Sana unaweza save nusu yake tsh-60.. sacrifice for your future..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unatakiwa ufanye maamuzi magumu.
Kama hiyo kazi ya kufundisha ni kazi ya ndoto yako endelea nayo huku unatafuta shule nyingine, lakini muhimu utafute nyumba karibu na eneo la kazi gharama ya nauli uepuke kama shuleni kwenu wanaruhusu biashara ndogondogo tafuta sehemu wanapouza asikirimu kwa jumla chukua zako. Mara nyingi la. Kuwekea anakupa mwenye asikirimu ukichukua piece 100 hukosi 3,000 kwa siku, ukiuza piece mia mbili hukosi 6,000.
Kama kufundisha unafanya tu ili mradi mkono uende kinywani chukua maamuzi magumu yakiume haswa pokea mshahara wako acha kazi.
120,000 inatosha kuingia nayo mtaani kupambana kwa biashara ndogo ndogo funga moyo pambana aiseeee ujiajiri utatoboa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshahara wa 120k:

Tafuta chumba sehemu yakaribu; kama si mbali usafiri wa miguu unatosha sana (30000-natumaini bei itapungua maybe, usiangalie ubora wanyumba wewe sio mtarii bali mtafutaji)

Punguza milo, mlo mmoja unatosha sana na maji yakutosha (mchana) kama si kazi ngumu..2000*30= 60000/=Tsh
inabaki kama 30000/= Tsh
Toa 10000/=Tsh kama kusave

Then 20elfu inayobaki;
maji na umeme(10000/=Tshs)

10000/=Tshs: vocha kwa case maalumu tu,,, 1000/=Ths sms zamwezi kwa haloteli au1500/=Tshs sms mwezi halotel, 1500/Tigo au 2000/sms Vodacom {Maximum 2000) kwa mwezi.

...inabaki kama 8000/=Tshs (kilinda mfuko,pia kama mgonjwa mgonjwa hapa panadol vs dawa yabei rahisi).

NB;kama umeweza pata chumba eneo la karibu nabei pungufu pesa itayobaki utajazia sehemu zamatumizi kama mlo, nauli n.k kwa case yamuhimu na haraka.
 
Nilikuwa mama ntilie, mimi na wadada wangu wa biashara wote tunakula hapo hapo na faida ipo na msingi upo.
Kwetu pia mama ntilie ndo biashara iliyonilea na kunisomesha na bajeti ya kula wote hapo hapo.
Mimi nakumbuka tunatembea kwa miguu na wanafunzi wenzangu tunawahi kwetu kula ukoko na maharage, aiseee hawasahau mpaka kesho ulivyokuwa mtamu.


Sent using Jamii Forums mobile app
Huoni kwamba hayo yanaweza kua mazingira rafiki ya kujifilis?
 
Ndugu huo msaada zaidi ungeandika hapa ingekuwa jambo muhimu sana
Mdau nimeona una wazo zuri lkn kwa mshara huo ni ngumu sana kusave. Ila nikushauri kitu kimoja kama hutojali lkn, hapo mwanza kuna ziwa naomba uachane na hicho kibarua ukatembeze dagaa wabichi. Kama kweli una moyo wa kujiajiri utaleta mrejesho wako baada ya miezi kadhaa. Mie nakwambia hayo kwasababu baada ya kumaliza form 4 nilianza kusaka kazi ktk viwanda vya samaki pale ilemela pasipo mafanikio! Lakini nikapata wazo la kutembeza dagaa wabichi kwa baiskeli za kukodi sikujuta hata siku moja. ila badae niliachaga kwa sababu ya kuendelea na masomo. But kwa msaada zaidi namna ya kufanya biashara na kusave nichek pm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ku-save hiyo ni ngumu sana mkuu, kwa kipato cha milioni moja kwa mwezi unaweza ku-save angalau elf 50 kibishibishi, na hapo inategemea kama huna ndugu na marafiki wa kupiga mizinga.
Yaani kwa kipato cha 1M unasevu 50K tena kibishi kweli tunatofautiana mimi hapo nasevu 800K tena sio kibishi na hao wazazi nimewasaidia vilevile 800K ndani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Talking from Experience
nilishawai kuishi na 40,000/= kwa muda wa miezi 4...nilikuwa nakula 1200/= kwasiku siku nimefeli 1500/= siku nimefeli zaidi njaa kali 2000/= na udalaliudalali ukini boost.

1200/= ilikuwa simple 1000/= nilikuwa nanunua wali mchana then usiku nakula Scones 2 ambazo nanunua package 1000/= zinakaa 10 So nikila 2 inakuwa sawa nimetumia 200/=

So hapo mlo nilikuwa natumia 1200 kwasiku...Hii sio rahisi wewe unaweza kula Scones ×2 kwasiku asubui na usiku Sawa unatumia 1400/= kwasiku.


1400 × 30 = 42000/=

Kuhusu chumba 30000/= ni kutokuwa na nudhamu na pesa

Panga chumba cha 15000/= kalibu na kituo cha kazi.

42000(meal)+15000(kodi)= 57000/=

3000 ya mambo mengine


TZS 60,000/= SAVING

Ni miezi mitatu unakuwa na 300,000 mtaji

Miezi minne 4 ni 350,000/=

Ila pesa ndogo sana uwezo wangu wa mwisho wa kusevu.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe unaongea nadharia mimi naongelea hali halisi kabisaaaaa.
Na kwa taarifa tu mpaka sasa ninafanya catering na kulisha ofisi.
Hiyo ni order ya sahani nane za biriani ofisi fulani.
Na hapo na sisi tukapata mlo wa mchana na usiku.
Saaa huoni aibu kubishana nadharia zako kwa watu walioko kwenye marketing? View attachment 1307934

Sent using Jamii Forums mobile app
Heshima yako madam!
 
Yaani kwa kipato cha 1M unasevu 50K tena kibishi kweli tunatofautiana mimi hapo nasevu 800K tena sio kibishi na hao wazazi nimewasaidia vilevile 800K ndani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah! hiyo laki 2 na sometimes hadi laki 4 ndo nawasaidia wazazi na bado wanadai haiwatoshi, nikiamua kuendesha gari langu kwenda kazini kila siku ni laki 3 hiyo, hapo bado matumizi ya familia ya kila siku. kuna kipindi nilikuwa nalipwa viposho ambavyo ukiunganisha na salary inafika kama ml.4 kwa mwezi ndo nikajifaragua kujenga kakibanda ambako hadi leo kanadai finishing. Inaweza ikawa pesa nyingi kwa maisha ya chini na huna presha ya kusaidia wazazi na hawa ndugu wengine, mara utaambiwa mpwa wako shule zinafunguliwa toa pesa ya ada na matumizi. Nafikiri wazungu walifanikiwa hili swala la extended families, kila mtu anafanya kazi kwa ajili ya familia yake na serikali zao zinatoa social security za kueleweka. Wazee wakipoteza uwezo wa kufanya kazi wanapelekwa kutunzwa kwenye makambi. Ngozi nyeusi ukifanikiwa kidogo hata ka-salary ka 800K kwa mwezi utaandamwa na ndugu waomba misaada hadi utajuta..
 
Dah! hiyo laki 2 na sometimes hadi laki 4 ndo nawasaidia wazazi na bado wanadai haiwatoshi, nikiamua kuendesha gari langu kwenda kazini kila siku ni laki 3 hiyo, hapo bado matumizi ya familia ya kila siku. kuna kipindi nilikuwa nalipwa viposho ambavyo ukiunganisha na salary inafika kama ml.4 kwa mwezi ndo nikajifaragua kujenga kakibanda ambako hadi leo kanadai finishing. Inaweza ikawa pesa nyingi kwa maisha ya chini na huna presha ya kusaidia wazazi na hawa ndugu wengine, mara utaambiwa mpwa wako shule zinafunguliwa toa pesa ya ada na matumizi. Nafikiri wazungu walifanikiwa hili swala la extended families, kila mtu anafanya kazi kwa ajili ya familia yake na serikali zao zinatoa social security za kueleweka. Wazee wakipoteza uwezo wa kufanya kazi wanapelekwa kutunzwa kwenye makambi. Ngozi nyeusi ukifanikiwa kidogo hata ka-salary ka 800K kwa mwezi utaandamwa na ndugu waomba misaada hadi utajuta..
Mkuu hayo unayoishi sio maisha siku ukisimamishwa kazi tu utaona maisha machungu.

Wazazi wanafunguliwa biashara yao hawasaidiwi cash endapo itatokea ×chache ila ukiwangulia inakupa unafuu.

Gari kuwa nalo si dhambi ila hapo inapokulia nshahala wako ili kulihudumia jitathmini maisha rahisi ukiwa na mikakati.

Mimi ningekuwa na salary hiyo I can't imagine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawaza tu mkuu:

1. Nunua mahindi debe 1, kasage upate unga dona Tsh. 24,000/=

2. Nunua Kilo 5 mchele Tsh. 10,000/=

3. Mwanza hapo dili na dagaa standard/samaki wadogo, mboga weka Tsh. 30,000

4. Vocha ni vifurushi vya chuo tu weka Tsh. 5,000/=

5. Nauli weka ya kwenda tu Tsh. 15,000/=

Jumla Tsh. 69,000

NB: Haya mahitaji muhimu TU! Kwa sasa, habari ya wanawake na pombe au starehe weka kando kidogo au tafuta mwanamke mmoja.

Muhimu zaidi tafuta Bima rahisi ipo kila kata Tanzania kakate ni kama Tsh. 50,000/= kwa mwaka

Save bank/kwenye simu Tsh. 35,000/= kila mwezi ila baki na pesa ya dharura mkononi.

INAWEZEKANA KABISA UKIAMUA TU



VIIXCCCL GrandLodge,ARUSHA
 
Dah mkuu nimejarib kubana ili uishi bila kuchanganyikiwa lakini natoka patupu.Mbinu zangu zahitaj usiri wa hali ya juu ila.Mbinu yangu itakufaa ikiwa utahitaji kutoka kwenye iyo kazi yaani ujiajiri au upate chanzo kingine cha kukuongezea kipato.

*Kwa mshahara wako kubali urudi nyuma kapange nyumba iliyo jirani na kazini ili uende kwa miguu ofcn na kupunguza gharama za usafiri ikabid panga nyumba ya kiza kuondokana na gharama za umeme simu utachaj 200 vibandan.

*Punguza gharama za simu toka mb na dk utumie sms tu naamini haitazid 1500 kwa mwezi (kifurushi cha mwezi)

*Kula 1500 kwa siku yaani 1000 mchana uwapo kazini na 500 usiku Chai na kitafunwa (utapika nyumban mana chai mgahawani usiku utaonekana mchawi)

*Achana na habar zote za starehe ziache tu zikupite.

*Kuhonga iwe ni mwiko nalo hili ni gumu kuliko ila ukiwa karibu na mungu ukawa muumin hakika hili utalishinda.

kumbuka yote hayo unayoyafanya sio kuepukana na maden bali upate akiba sio yakuongeza thaman ndani au kubadil smartphone bali kubadili kazi kujiajiri au likawa gumu kujiajir basi kupata kazi ingine ya ziada itakayokuwezesha kuongeza kipato.

#Kwa mchanganuo hapo juu nimepata
Kod ya nyumba 30000 umeme na maji

#Chakula 1500*30=45000+ 5000(Sukar majani)= 50000

50000+30000=80000 ( yaweza kupungua ikiwa utapanga nyumba ya kiza)
80000+10000(vocha(sms)+sabuni+ usafir wa dharula nk)
90000 kwa mwezi.
120000-90000=30000
30000 ndiyo akiba ambayo utaitumia kutengeneza mtaji wa biashara ingine na dharula kama kuumwa nk)

Kama nakuona utakavyo taabika pia vibarua na vikazkaz vya mtaani usijivunge jichanganye.Binafsi nimeishi kwa gharama ya 60000 kwa mwezi.
Kod 20000+5000 umeme maji hayazid 1000(200 dumu)
Kula 1000 kwa siku amazing story (nilikunywa chai na maandazi au mara moja moja na kufunga swaum za Sunnah nakufutur msosi wa 1000 jioni) Sifanyi kazi ngumu.
26000+30000=56000/= Iyo 4000 hapo 1500 vocha sms ndio kuwasiliana no kupiga,2500 dawa mswak+ sabuni+mafuta.
Nikutie moyo nalipa kod 80000 (chumba na sebule) frem za kaz baada ya kuongeza mtaji now nalipa 200000 kwa mwezi (frem 3).Nabadili mlo nitakavyo sio tena chai maandazi na kufunga swaum.

Bado napambana na haya maisha so ubahili ndio maendeleo yalipo.

Mtangulize Mungu na Fanya mambo kwaajili yako usiseme watanionaje akina fulani niliosoma nao.
Kila la kher na afya ndio mtaji wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Anachotakiwa kufanya ni kukata shauri tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maamzi yako kwako uamue njia njia ya kusevu

hii ni mbinu ya kininja

Nenda mtandao wa simu unao tumia sajili line mpya halafu hiyo line utaongea na wenye mtandao wataifunga kwa muda unao taka wewe kusevu hela yako na kwa hiyo hela unayo pata unaweza kusevu


30,000 kila mwezi na ukaweka malengo ya kuwa ikifika kiasi fulan nitaenda kuifungua hiyo line

Ya pili u aweza kuwa unanunua vitu ambavyo unaweza kuja kuviuza baadae
Mkuu hilo la line ni kitu practical??
Kwamba kuna mtu kashawah kujaribu??
Maana wasije wakafunga line halaf wakaigawa namba kwa mtu ikawa majanga
 
Back
Top Bottom