Msaada: Wapi nitapata mpunga kwa wingi wa kununua kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa?

Msaada: Wapi nitapata mpunga kwa wingi wa kununua kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa?

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,623
Reaction score
8,442
Salamu wajasiriamali,

Kama mada inavyojieleza.

Ninaishi mkoa mmoja wapo wa Kanda ya Ziwa. Nina kahela kidogo nafikiria niingie vijijini wanakolima mpunga kwa wingi nikanunue magunia kadhaa niyahifadhi.

Sasa changamoto sijui niende sehemu gani ndani ya mikoa iliyopo ndani ya kanda ya ziwa ambako nitaweza kupata mpunga wa kutoka kutoka kwa wenyeji.

Mwenye ufahamu wowote juu ya hili anijuze hapa kwenye comment.

Asanteni.

Tujilinde dhidi ya Covid-19 inaua
 
Mkuu njoo Chato maeneo ya kazunguti.
Mpunga upo mwingi sana
 
Kuna sehemu nilipita mkoa wa Mara gunia la debe sita tsh.45, 000. Lakini uzalishaji wao si mkubwa.
 
Njoo sehemu moja inaitwa Burige,,,mpunga mwingi,42,000.
 
Maswa - Simiyu, Gunia la debe 4 ni 32000 hapo wilayani, ukiingia vijijini ni pungufu na hapo.
 
Kuna gunia la debe 4 mkuu.? Nielimishe kidogo hapo

Gunia la mpunga yapo ya aina 2, la Kwanza Ni Gunia lenye ujazo wa debe nne na Gunia la pili Ni Gunia lenye debe 6, hivyo unachagua unataka lipi na kwa Kila debe la mpunga linauzwa Tsh 8000
 
Duh.... Ila biashara ya kununua mpunga ni kujivika vesti ya mabomu.

Nakumbuka nilikwenda kununua magunia ya mpunga 22 mwezi wa pili, ile kwenda kuyaanika yakapungua na kuwa 18,kuja kuyakoboa duuuh nusu ya mzigo ukawa ni hasara......

Yaaani pumba ni nyingi, chenga ni nyingi mchele ukakatika katika ikawa ni hasara bini sifuri..... Nikakoma.....
 
Duh.... Ila biashara ya kununua mpunga ni kujivika vesti ya mabomu.

Nakumbuka nilikwenda kununua magunia ya mpunga 22 mwezi wa pili, ile kwenda kuyaanika yakapungua na kuwa 18,kuja kuyakoboa duuuh nusu ya mzigo ukawa ni hasara...... Yaaani pumba ni nyingi, chenga ni nyingi mchele ukakatika katika ikawa ni hasara bini sifuri..... Nikakoma.....
Tatizo hapo ulininua mpunga mbichi, siku nyingine hakikisha unanunua mpunga uliokauka vizuri.
 
Gunia la mpunga yapo ya aina 2, la Kwanza Ni Gunia lenye ujazo wa debe nne na Gunia la pili Ni Gunia lenye debe 6, hivyo unachagua unataka lipi na kwa Kila debe la mpunga linauzwa Tsh 8000
Gunia la mpunga lipo la debe 10 wanaita shanga 2 na la debe 7 ambayo likijazwa vizuri inaingia debe 8. Mchele ndio kuna debe 6. Kwa uzoefu wangu mbeya na nyanda za juu kusini kote.
 
Duh.... Ila biashara ya kununua mpunga ni kujivika vesti ya mabomu.

Nakumbuka nilikwenda kununua magunia ya mpunga 22 mwezi wa pili, ile kwenda kuyaanika yakapungua na kuwa 18,kuja kuyakoboa duuuh nusu ya mzigo ukawa ni hasara......

Yaaani pumba ni nyingi, chenga ni nyingi mchele ukakatika katika ikawa ni hasara bini sifuri..... Nikakoma.....
Ukitaka kununua mpunga lazima ujue kwanza nature ya biashara na zao lenyewe, mpunga huwa unaijarbu kabla ya kununua na kama ni mzigo mkubwa unatakiwa upeleke kwenye machine za kisasa za kukobolea mpunga ambayo inatenganisha pumba na chenga yasn inatos GRADE 3. grade 1,2,3 na chenga za kuku a vitunbua.
 
Back
Top Bottom