Miwani ya macho hasa hiyo ya kupima ni dawa tosha ya macho. Niakujibu kwa lugha nyepesi na si ya kitaalamu kwa ajili ya uzoefu wangu kwa kuwa nimevaa miwani tangia pr schl na sijaona madhara yoyote yapata 40 yrs sasa.
Waweza kuvaa hata kwa miaka 20 bila ya kubadili namba ya miwani.
Jinsi macho yanavyoimarika, ukianza kuona jozi uitumiayo haioni vizuri, basi rudi kwa daktari wa macho kupima.
Waweza kukuta toka hiyo 3.5 ilishashuka hadi 0.5, hapo elewa afya ya macho inaimarika na huenda ukashauriwa kuacha kutumia kwa kuwa umepona na hauhitaji kuvaa tena.
Lakini ukiona namba zinaongezeka, basi na tatizo linaongezeka pia.
Ni vema kila uonapo badiliko la uonaji, rudi haraka hospitali kwa wataalamu kupima, usinunue miwani ya macho mitaani, labda iwe kwa kipimo chako sahihi.