Msaada;wataalamu wa afya ya Miwani ya macho

Msaada;wataalamu wa afya ya Miwani ya macho

Pure Scientific

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2015
Posts
716
Reaction score
643
Habari wakuu...

mwaka 2014 nilipopoma macho CCBRT na kuanza kutumia miwani ya kuniwezesha kuona mbali yenye namba 3.5 baada ya hapo sijawahi fanya check up tena ila nimekuwa nikibadilisha mawani kwa machinga kariakoo...

Je kuna madhara ninaweza kupata kwa wataalamu wa macho maana sijawahi ONA TATIZO tangu nimeanza kutumia...???
 
Miwani ya macho hasa hiyo ya kupima ni dawa tosha ya macho. Niakujibu kwa lugha nyepesi na si ya kitaalamu kwa ajili ya uzoefu wangu kwa kuwa nimevaa miwani tangia pr schl na sijaona madhara yoyote yapata 40 yrs sasa.
Waweza kuvaa hata kwa miaka 20 bila ya kubadili namba ya miwani.
Jinsi macho yanavyoimarika, ukianza kuona jozi uitumiayo haioni vizuri, basi rudi kwa daktari wa macho kupima.
Waweza kukuta toka hiyo 3.5 ilishashuka hadi 0.5, hapo elewa afya ya macho inaimarika na huenda ukashauriwa kuacha kutumia kwa kuwa umepona na hauhitaji kuvaa tena.
Lakini ukiona namba zinaongezeka, basi na tatizo linaongezeka pia.
Ni vema kila uonapo badiliko la uonaji, rudi haraka hospitali kwa wataalamu kupima, usinunue miwani ya macho mitaani, labda iwe kwa kipimo chako sahihi.
 
Back
Top Bottom