Msaada-Watoto wetu(ndugu)wametiana mimba

Dah...Mungu hauhusiki kwa lolote hapo....Kama aliwaumba kwanza Adam na Eve pekee....wakapata watoto...na wakapata wajukuu...jiongeze[emoji41]
 
tukubaliane kutokukubaliana me kwangu zygote ana haki zote kama binadamu mtarajiwa kama ambavyo kidole kina haki ya kuishi kwenye mkono (endapo hakina kansa) ila kukikata sababu watu walifanya sex zao nao ni ndugu sijakubaliana ila ndo hivyo maoni mbalimbali
 


Sawa mkuu, lakini tafakari sana juu jambo hilo, Zygote siyo mtu tupilia mbali binadamu, naam waweza sema "mtu mtarajiwa" na mtu mtarajiwa bado hajawa mtu bali anatarajiwa kuwa mtu hapo baadaye.

Aborting a zygote out of any reason, either good or bad is not a murder offence.

Na siku zote yanafanyika hayo kuokoa maisha ya mama, (in favour of mother life and not in favour of Zygote life).
 
mkuu unaongelea upande wa kuokoa maisha ya mama, huko sina neno napo ni sawa napo kabisa ila kwa swala la kaka na dada wamepeana mimba waachwe wazae tu maana wataona njia nyepesi ni kutoa tu na wataendelea mifano tunayo kwenye jamii
 
mkuu unaongelea upande wa kuokoa maisha ya mama, huko sina neno napo ni sawa napo kabisa ila kwa swala la kaka na dada wamepeana mimba waachwe wazae tu maana wataona njia nyepesi ni kutoa tu na wataendelea mifano tunayo kwenye jamii


Wewe ni lazima ufikiri jambo hilo kama "gentle man" and wise man (mwanamume mwenye busara).

Mtu kutembea na dada yake ni incest lakini mtu kuzaa na dada yake ni much more incest kwa sababu kutembea inaweza kuwa siri lakini kuzaa inakuwa siyo siri tena, mbaya zaidi kuna nafasi ya kuzaa mtoto ZOMBIE ambaye anaweza kuwa na maisha ya dhiki na pia akawapa shida hao wazazi katika malezi na pia anakuwa ni mtu asiye na faida kwa taifa kwa ujumla licha ya kutokuwa na faida kwa wazazi.

Unatakiwa uliangalie hilo jambo katika mtazamo huo na siyo mtazamo finyu kama huo wako. Mtazamo wa ubinafsi na wa "SHAURI YAO"
 
nimewaza kibinafsi sababu hiyo idea yote ya dada kupewa mimba na kaka haijakaa sawa ina ukakasi mno ila nimejaribu kufikiria kuangalia logic yako, ni vibaya sana kutoa mimba lakini adhabu yake sio kifo kama ambayo mtu ambaye ameshazaliwa angeuwawa, na hili wazo la kuwa hii ni kitu immoral ni kweli tumeitoa kwenye dini hasa torati ila kuna sehem adhabu ya mume aliyempiga mkewe na kusababisha abortion imewekwa kuwa tofauti na adhabu ya mwanamume amempiga mkewe na kusababisha abortion na kifo cha mama kuwa auawe na yeye (nadhani wanahesabu binadamu baada ya kuzaliwa), i think a belief that "a human being exists at conception" is a matter of faith, not fact - pamoja mkuu!
 
Du chances hapo wote wa nusu ya genes za mama zao, si sawa na baba mmoja mama mmoja. Anyway yameshatokese. Kimila mnatakiwa kuchinja mnyama kwenye kaburi la babu ili kuua undugu ili waweze kuoana.
yapa makabila haitawezekama zaidi ya kutambika wa kiume atafukuzwa kijijini ila akija huku pwani kwa wazigua freshi tu wanaona
 
i think a belief that "a human being exists at conception" is a matter of faith, not fact - pamoja mkuu!


You just "think",!!, ,you have to check out and come out with evidence. No where can you find in any religious books such notion.
 
Laana wametoa kwa wazazi wao hizo..

We fukuza tu hao wasitie najisi nyumba yako
 
Hao kwa mila ya kiislam, km ni mtoto wa baba mkubwa na baba mdogo wanayo haki ya kuonana
kabisaa mkuu, sasa nashangaa wanavyohangaika kutaka kudhulumu nafsi wakati upo uwezekano wa jambo hilo kufanyika wakaona na wakazaa watoto safi tu maisha yakaendelea, hizo habari za utaahira ni imani pofu(blind).
 
kabisaa mkuu, sasa nashangaa wanavyohangaika kutaka kudhulumu nafsi wakati upo uwezekano wa jambo hilo kufanyika wakaona na wakazaa watoto safi tu maisha yakaendelea, hizo habari za utaahira ni imani pofu(blind).



Usichanganye mila za waarabu na Uislamu, watu kuoana kaka na dadake, (watoto wa kaka au wa dada wa damu) ni mila za waarabu hata kabla ya Uislamu.

Ukiangalia historia ya waarabu moja ya mambo yaliyotamalaki miongoni mwao ilikuwa ni uadui kati ya koo na koo au kabila na kabila, hivyo basi uadui huo ulienda hadi kushindwa kuoleana, yaani kijana anataka kuoa lakini aoe wapi ilhali koo au kabila ambamo anataka kuoa ni maadui zao!!,, jambo jingine baya lililokuwepo miongini mwa waarabu ni majivuno ya kikabila au kiukoo, yaani koo fulani zilijiona ni bora kuliko koo fulani na kuoa katika koo hizo ilikuwa taabu sana au kijana kutoka katika koo "bora" ilikuwa ni laana au fedheha kuoa katika koo dhalili.

Kwa muktadha huo ndio maana ndugu wakawa wanaoana na kwa bahati mbaya mila hiyo ikaingizwa katika uislamu na wanatoa aya kuunga mkono kuwa jambo hilo halijakatazwa ndani ya Qur'an, lakini hebu waulize katika Qur'an imekatazwa wapi mjukuu kuoa bibi yake au babu kuoa mjukuu wake wa kike??😁😁.
 
hahaha hizi mambo ni shidaa
 
Unataka kutuambia qurun ilichachukuliwa?
Je upande wa biblia unasemaje kuhusu hili?
 
Ujumbe tumeelewa, ila tujitahidi kuframe vichwa vya habari.

Haizekani kabisa "watiane" mimba, bali mmoja amemtia mimba mwenzake au ametiwa mimba na mwenzake, naamini hivyo. "Kutiana" maana yake kila mmoja ametiwa mimba.
Naweza kurekebishwa kama nimekosea.

Ila kimsingi si jambo rahisi kulitatua Kwa hali yoyote ile. Maji yamekwisha mwagika. Asubiriwe ajufungue tu. Kama ni fedheha kwa kiwango kilichofikiwa hakina marashi wala sabuni yoyote ya kusafisha. Bahati mbaya Sana!!!!
 
Unataka kutuambia qurun ilichachukuliwa?
Je upande wa biblia unasemaje kuhusu hili?


Qur'an ipo makini sana katika kuainisha yupi anafaa kuolewa/kuoa.

-- kuhusu Biblia sijui kama ipo wazi kama ilivyo Qur'an, naomba wajuzi wa Biblia kwenye suala hili waje watufahamishe.
 
Yaani mtu na binamu yake? Wapeni tu hatiza ndoa, warabu na wahindi wangekuwa matahira maana wao ndo kawaida tena na zaidi ya hapo. Labda kama wote wana magonjwa ya kurithi
 
Yaani mtu na binamu yake? Wapeni tu hatiza ndoa, warabu na wahindi wangekuwa matahira maana wao ndo kawaida tena na zaidi ya hapo. Labda kama wote wana magonjwa ya kurithi
Magonjwa ya kurithi ni yepi?msaada tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…