Msaada wenu: Baba yangu mzazi anataka kunitimua kwenye nyumba ya babu yetu

Nachelea kukwita jina baya lakini ukweli ni kwamba wewe ni baradhuli.
Kwanza, urithi wa babu kwa mjukuu haupo. Ila kama babu kwenye uhai wake alikupa kama zawadi, tunu n.k hiyo inaweza kukubalika.
Kitendo chako cha kulalamika 'eti baba yako anakufukuza toka kwenye nyumba ya babu' ni aibu kwa kijana wa kiume mwenye umri wako. Inaelekea wewe ni wale akina 'kula kulala'
TAFUTA CHAKO KWA JASHO LAKO NA HATA IKIBIDI KWA DAMU YAKO
 
Kosa lako liko kwenye aya ya 5-7.
Kuna watu wengi wenye allergy na kitimoto.achana nayo hiyo kitu .maana baba ni bora kuliko hiyo kitu
 
Mie naungana na baba...kwasababu hata chuo kikuu chenyewe umeshindwa kujifunza kuandika sawia..karibu kila para kuna mazonge[emoji33]!au ni chuo gani hicho mkuu?
Baba ana akili na upeo mkubwa sana!
Kaazi kwelikweli...hatutafika hivi nakwambia...
 
Hili andiko jf halikuwa mahali pake labda kwenye wataup group la CCM nahakika utatukanwa humuuu ijapokuwa sijasoma hata comment moja
 
Kapange hata getto mwanaume gani chuo kikuu utakosa hata hela ya kula
 
Mzee yuko sahihi. Na akili zako zote hizo umesoma hakuna sera zozote za kueleweka zilizowekwa na serikali ya CCM kuhusu ajira. Huna kazi na unashabikia CCM.
Unakwenda nje ya mada na kama kazi anaweza hata kuuza karanga kama wanavyofanya wajasiria mali wadogo. Huyu jamaa ni mvivu, tegemezi na mlalamikaji. Nia aibu sana kwa kijana wa leo kuwa na mtizamo finyu wa maisha.
 
I doubt kama kweli una elimu ya chuo kikuu labda uniambie once upon a time ulipita maeneo ya chuo.
 
Dah! Imebidi nicheke kwanza maana ile naanza kusoma tu nilikuwa nishaingia miongoni mwa watia hasira
Kesi ya nyani umeileta kwa mkulima!

Acha nijiandae kusoma komenti watakutia hasira huku hadi ujikute unajuta kuandika uzi wako.
 
CCM CCM eeeeeeeeeeh heee chama cha mapinduzi CCM namba moja.

hata watoto wanajua CCM namba moja

hata baba ako anajua CCM namba moja

CCM CCM eeeeeh heee chama cha mapinduzi CCM namba moja.

nimemaliza na sina la kukushauri zaidi zaidi ntakwambia tu rejea AMRI YA NNE kwenye bible.
 
Ushauri mzuri sana [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Anakutishia!! Jichanganye kama hujayaoga hayo maji
Nyumba ni ya babu yangu, ananitisha eti akinikuta ndani atanimwagia maji ya moto, anasema nikaishi ukouko kwa mjumbe wa ccm
 
Muombe msamaa baba yako ndugu yangu. Kisha tulia tuli. Siku ukipata ajira au ukijiajiri na kupata kwako unaweza sasa ukaamua mambo yako. Kwa sasa upo chini ya himaya yake. Jifanye mjinga, hapo suala la siasa za CHADEMA na CCM sioni kama ndio chanzo. Shida ni kutoheshimu maamuzi na matakwa ya baba.

Leo ni masuala ya CCM kesho yataibuka mengine. Jifunze kuishi na mzee wako kijana.

Siku nyingine ukihitaji ushauri sema chanzo ni CHADEMA wanajamvi watakupa ushauri. Ukileta habari za CCM hapa huwezi kusaidiwa. Wengi ni wahanga na CCM humu. Nisiongee sana. Ushauri ndio huo
 
Nyumba ni mali za watoto sasa babu mtoto wake ni baba wewe nenda kwenye nyumba aliyo jenga baba
 
Mkuu unajua saa nyingine ukishagundua mtu hajitambui bora na wewe umshauri kile anachotaka kusikia. Kama ana akili atasoma katikati ya mistari.
Umempa ushauri mzuri msomi huyo.
mkuu kiuhalisia wengi hushindwa kuzibadili elimu kutengeneza fursa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…